Wanakijiji wamkataa mwekezaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanakijiji wamkataa mwekezaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 4, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Burhani Yakub, Tanga​


  WAKAZI wa Kijiji cha Kwedikwabu, Kata ya Kwamsisi, wilayani Handeni, wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa kuingilia kati sakata la mwekezaji mmoja kutoka Dar es Salaam kuvamia eneo lao lenye ukubwa wa ekari 2,000.


  Akizungumza kwa niaba ya ujumbe wa wanakijiji hao waliofika ofisi za gazeti hili mjini hapa, Ramadhani Bakari alisema walishtuka baada ya kuona watu wakifyeka eneo kutayarisha shamba hatua iliyowalazimisha kuwafukuza.


  “Tulishtuka baada ya kuona kuna watu porini wakifanya kazi ya kufyeka, tulipowakamata walimleta mwekezaji huyo ambaye alijitetea kuwa, ameuziwa na mzee mmoja wa kijijini tukamwambia umetapeliwa kwa sababu hukufuata taratibu,” alisema Bakari.


  Alisema walipomfukuza alirejea Dar es Salaam, lakini baadaye alirudi tena kijijini na kuanza kufyeka huku akisisitiza kuuziwa eneo hilo.


  Bakari alisema baada ya kurejea tena kijijini, wananchi waliomba uongozi wa kijiji kuitisha mkutano mkuu ambao uliamua kumkataa mwekezaji huyo, huku akipewa amri ya kuondoka mara moja.


  Akizungumzia suala hilo kwa simu, Mtendaji wa kijiji hicho, Juma Shaaban alikiri wanakijiji kumkataa mwekezaji huyo katika mkutano huo kwa kupiga kura nyingi za kutaka aondoke.Shaaban alisema baada ya uamuzi wa mkutano mkuu wa kijiji aliwasiliana na Polisi Kituo cha Mkata, walipelekwa askari na kumuamuru aondoke kwani wanakijiji hawamtaki.


  “Mkutano mkuu wa kijiji ulifanyika Julai 8, mwaka huu wananchi walipiga kura nyingi za kumkataa, nikapeleka taarifa hadi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni,”alisema.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Hawa ndio Wanakijiji wanaojua kuwa Muungano ndio utakao linda Ardhi yao; Hawana Mchezo...

  Hawana Mchezo wamemuondoa Mwekezaji na Wamemuita Mkuu wa Mkoa kumueleza hayo, hii ndio inavyotakiwa

  People's Power; Wa Gezaulole wangeungana pamoja sidhani ardhi yao ingebwa kurahisi na Mabosi wa Serikali Kuu na

  Watoto Wao Wapendwa. Wakulima wetu wana NGUVU bado na wana kura sababu wengi bado wapo vijijini...
   
 3. zungupori

  zungupori Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  nahisi hili sakata halijaisha, sikilizia mwana hii nchi ni kupandisha dau tu. Iwapo huyo mwekezaji ana interest tosha na eneo hilo, wanakijiji itabidi wawe prepared for kiinimacho. Kwani huyu mwekezaji ni mzungu au mbongo? For the villagers sake I hope a mzungu is not involved sababu sarakasi mbili tatu watu weweee, unalose focus kabla hujajiju kihamba kimehamishwa
   
 4. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huyo si mwekezaji ni mwizi wa kawaida. Usishangae hata akawa rais au mawaziri wake hata mkuu fulani wa mkoa kama si mbunge au mfanyabiashara aliyewatia kapuni watawala. Walipaswa wamchome moto huyo sawa na wanavyowafanyia vibaka. Wanakijiji hakikisheni mnafunga hata barabara na kuhakikisha hamfanyiwi huo ujinga.
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Wananchi hawajamkataa mwekezaji, wamekataa kuibiwa ardhi yao! Huu ni upotoshaji wa habari.

  Taratibu za kuuza ardhi za kijiji inapaswa kuboreshwa. Na viongozi waache tamaa! Siku hizi hata hatua 20x20 shurti kijiji kihusike na kuna fees za kulipa. Ila mamlaka ya viongozi wa kijiji inahitaji limit. Isitoshe sheria inataka ununuzi na uwekezaji wa 50+ acres EPZA wahusishwe.
   
 6. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #6
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hapa wala hakuna kilichofanyika. Angekuwa ngozi nyeupe ninyi nyoooote mngeufyata tu na kuishia kulalama kwenye vyombo vya habari huku mtasha wa watu akiendelea kufyeka, kuvuna magogo, kuchimba mahandaki na kuondoka na wake zenu kwenda kustarehe nao fukweni. Pambaf nyie!!!
   
Loading...