Wanakijiji wafunga barabara kuu Tabora-Singida

supercharger GT

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
839
1,000
Wanakijiji wa kijiji kilicho ndani ya wilaya ya Igunga na kupakana na mkoa wa Singida wameamua kufunga barabara kwa kuweka mawe barabarani na kuzuia magari yote yanayotoka mkoani Tabora au kuingia mkoani Tabora wakishinikiza kuonana na Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa mkoa huku wakiwa na silaha za jadi ambayo ni mikuki na mishale!

Barabara hiyo imefungwa tangu saa mbili asubuhi mpaka sasa hivi. Juhudi za baadhi ya askari na watu mbalimbali kuwatuliza waruhusu magari hazijafinikiwa mpaka sasa!

Wanakijiji wenyewe wanadai Sababu ya wao kufanya hivyo ni kutokana na uonevu waliofanyiwa wenzao baadhi kwa kubomolewa nyumba zao na kuibiwa mifugo yao na watu wanaodai ni watu wenye nguvu serikalini
IMG_20190217_102119_8.jpeg
IMG_20190217_102927_3.jpeg
IMG_20190217_095552_5.jpeg
IMG_20190217_102132_4.jpeg
IMG_20190217_093003_4.jpeg
IMG_20190217_094604_2.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

supercharger GT

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
839
1,000
mbona barabara ipo wazi tu.polisi wapige mabom ya machozi watasepa wakasali leo jpil
Ogopa sana mtu ambaye anahisi ameonewa na ana silaha za jadi, wataoumia ni wananchi wa kawaida na wasafiri, wakiamua kurusha hayo mamishale yao na polisi wapige mabomu yao mkuu wataumia wasafiri wengi sana wasio na hatia hapa!

#NOTE: Hawa ni wanakijiji na sio wasomi wa mijini

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,003
2,000
Pi cha zote umezipiga kuanzia mida ya saa3 asubuhi,mbona zinaonekana kama umezipiga usiku wa mbalamwezi?
Kuna bw mdogo kasafiri leo nimeishia tu kumfananisha ajili ya mwanga hafifu wa hizo picha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ngorunde

JF-Expert Member
Nov 17, 2006
2,030
2,000
Barabara ni kiungo/kiunganishi muhimu sana kati ya sehemu moja na nyingine. Pia ni kichocheo cha maendeleo, huduma muhimu katika jamii. Kusafirisha dawa,vyakula,maiti,wagonjwa nk.

Kufunga barabara na kusababisha mateso kwa raia wengine kwa kisingizio/sababu yoyote ile ni kosa la jinai
 

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
15,745
2,000
Mpaka itumike nguvu nyingine ya ziada ndiyo raia tunasikilizwa, mmewekwa madarakani ili iweje sasa maana kero za raia hamzisikilizi
 

Imwase

JF-Expert Member
Jun 14, 2017
501
1,000
Ogopa sana mtu ambaye anahisi ameonewa na ana silaha za jadi, wataoumia ni wananchi wa kawaida na wasafiri, wakiamua kurusha hayo mamishale yao na polisi wapige mabomu yao mkuu wataumia wasafiri wengi sana wasio na hatia hapa!

#NOTE: Hawa ni wanakijiji na sio wasomi wa mijini

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi unadhani wana uwezo wa kushindana na polisi ?
Hivi polisi walipue mabomu ya machozi hao waandamanaji wataweza kurusha mshale au mkuki hata mmoia ?
Thubutu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom