Wanakaragwe tuungane kumuwajibisha Mbunge wetu

Ti Go

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
882
848
Naandika kwa uchungu mkubwa juu uwajibikaji wa mbunge wetu wa kipindi cha 2015 - 2020. Tangu mbunge huyu apate ubunge mpaka wa leo hajaonyesha juhudi zozote za kusaidia maendeleo ya wilaya ya Karagwe kama alivyoahidi alipogombea ubunge. Aliahidi atakapopata ubunge, atashughulikia bei ya Kahawa. Mwanzoni mwa mwaka 2015 kahawa ilikuwa inauzwa sh 1,800, mpaka sasa hivi anamaliza kipindi, kahawa imeshuka bei kufikia sh 1,100.

kinacholeta hofu ni kuwa huyu Mheshimiwa amekuwa waziri wa biashara na viwanda, nafasi inayompa nafasi nzuri ya kushughulikia soko la kahawa (pamoja na mazao mengine). wakati wanaingia madarakani, ilisemekana walikuta kahawa inatozwa kodi 30+, wakazifuta. Ajabu badala ya kupanda bei, ndiyo kwanza inaporomoka. wakati huu anarudi kuomba tena kura. kwa zuri lipi tukuongezee muda wa miaka 5. utasaidia nini?

Naongelea zaidi zao la kahawa kwa sababu uchumi wa Mkoa wa Kagera, hususani wilaya za Karagwe na Kyerwa, umesimama juu ya zao la kahawa. Kahawa ikipanda bei, faida siyo kwa mkulima tu, bali pia mzunguko wa fedha unakuwa juu kiasi kwamba makundi mbali mbali yanafaidika. Wenye maduka vifaa vya ujenzi, boda boda, mama lishe, wajenzi, wamiliki wa baa za pombe/bia, kila mmoja anafaidika kwa namna yake.

Najua kuna sababu nyingi zinazosababisha zao hili kushuka bei na ambazo ziko ndani ya uwezo wake. Leo niongelee sera ya chama cha mapinduzi ya kulinda ushirika. tukubaliane kuwa ushirika ni muhimu kulindwa, kwa sababu ushirika ukifa, wanunuzi binafsi watawanyonya wakulima.

Ila sasa wahusika wameshindwa kuusimamia ushirika na badala yake, ushirika unanyonya mkulima. Ndani ya ushirika kuna ubadirifu wa kila aina (kuanzia kwa wapimaji, wasafirishaji, wasagaji, matumizi ya ofisi ya hovyo, madeni ya nyuma na kadhalika). Kwa mfano mdogo hapa niulize, deni la KDCU la takribani 800 milioni lililokuwa linadaiwa na CRDB lilipwa lini na fedha zilitoka wapi? kama zilikatwa kwa mkulima, waliosababisha hasara hiyo walifanywa nini? wapo na wanajulikana.

Nimeeleza upande mmoja wa sababu zinazo sababisha zao la Karagwe kushuka bei. Yapo mengi ambayo nasita kuyaeleza hapa amabayo yako ndani ya uwezo wa mbunge/waziri. Lakini hebu tuangalie ni kwa nini wenzetu uganda wananunua kahawa kwa bei ya juu. Kahawa ina faida nyingi zaidi tunavyoiangalia. Tumezoea kuiangalia tu coffee bean, lakini ina cha zaidi.

Maganda yake ni mbolea nzuri, maganda yake ni chanzo kizuri cha nishati hasa kutengeneza mkaa. Ukiritimba (kuzuia ushindani wa wanunuzi binafsi) unaowapo KDCU uwezo wa kununua zao hili peke yao. hakuna ushindani, bei wanayotangaza ndiyo mkulima analazimika kuuza

Lakini pia kodi nyingi za serikali kuu na serikali za mitaa zinasababisha bei ya kahawa kushuka kwa kuongeza makato.

Nashindwa kuongelea mengi ili nisichose msomaji. Bado kuna kazi kubwa ya kuwa na mbunge mwenye uchungu na maendeleo ya wilaya ya Karagwe.

Maendeleo ya Karagwe yanafungamana na maendeleo endelevu ya zao la Kahawa. Kwa mwenendo huu, Karagwe tutaendelea kuwa masikini kwa sababu ya kutokuwa na uongozi makini wenye mamlaka.

Tujadiri kwa pamoja, je ni sahahi kwa Mheshimiwa Innocent Bashungwa, Waziri wa biashara na viwanda kuomba tena ridhaa ya Wanyambo kuwawakilisha tena jimbonI?
 
Nshomire karibuni Huku mumsulubu Bashungwa anataka kuwachezea akili!
 
Mkoa mzima wa Kagera una wabuge vilaza. Anayebisha aje na jina la mbunge kisha ataje kafanikisha nini la maana kwenye jimbo.

Wote wapuuzi kabisa, wajinga wakubwa, washamba wala hawana exposure na uongozi sijui uwaziri wanapewa wa nini, wana akili chache kuliko hata darasa la saba mtaani, hawakai majimboni kwao, hawajawahi kuwa na impact kwenye bunge yani hutokaa usikie mbunge katokea Kagera katoa hoja. Wakija kutoa hoja ndo zile za cherehani nne ni kiwanda, kadri unavyotanua ndivyo wanazidi kutamani, na bangi nyinginezo.

Nasema hivi fukuza vichaa wote hao chagua mwenyeji wa jimbo husika na mwenye uwezo au anayeishi jimboni. Kule Ludewa Filikunjombe (R.I.P) alikuwa anaenda sana jimboni pamoja na kuwa na nyumba Kijichi, Sugu anaishi sana Mbeya, Prof. J anaishi sana Mikumi. Sasa haya mambumbumbu mengine hayana ofisi wala wawakilishi. Fukuza majambazi yote haya.

Hivi suala la kahawa nalo linataka kiherehere cha serikali? Si ni kuweka SERA tu zilizonyooka na kusubiri kodi. Hakuna mtu anataka pembejeo sijui mikopo kama wanavyopewa mazao mengine. Weka sera, simamia basi. Mi nadhani serikali kuu ina lengo rasmi la kuzuia maendeleo kimakusudi kwa wakulima. Na kazi ya mbunge ndo hiyo kutetea haki ya wapigakura. Vyama vya ushirika, bei elekezi, malipo, ubadhirifu, etc ni vya kupambana navyo.

On top of that: Kuwepo na utaratibu wa kufukuza vilaza wanaoshindwa kuwakilisha wananchi, kama PM anafeli si anapigiwa kura ya kutokuwa na imani. Hata mbunge wananchi wake wapewe uwezo huo.

Sema na nyinyi raia ni wanafiki wakubwa, kuleni jeuri yenu. Kwa mfano wale Nkenge eti walimchagua Dr. Kamala ambaye hata hajawahi kulala nyumbani kwao (hana kwake jimboni). Yani mbunge anakuja mchana anarudi jioni, once per year. Akipita road hasalimiani na mtu ni full tinted mpaka kwa mama yake, anakula lunch anapiga story na wapambe njaa kali na majirani wanapewa vizawadi njaa kisha anaondoka. Huyu naye eti alipewa kibali cha kuwawakilisha.
Hapa nimemtaja wa Nkenge tu, bado kuna huyo wa Bukoba Vijijini na majambazi wengine.
 
Back
Top Bottom