Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,606
- 729,493
Hawa si maneno mageni kabisa miongoni mwetu...haya maneno ya kusema...
Usicheze na mimi nimeaga kwetu au
Mimi sio mwenzako nimeaga kwetu.
Mi majivuno ni majigambo ni sifa na tambo zinazochagizwa na kujiamini kwa namna yake 'kuaga kwao'
Unaweza kudhani ni maneno ya kawaida au mepesi lakini kwa sehemu kubwa wengi humaanisha kutokana na kile 'walichofanyiwa huko kwao'
Kimsimgi hakuna cha ziada walichofanyiwa zaidi ya ushirikina na mizimu, yaani kufanyiwa tambiko au madawa ya nguvu za giza za kukulinda popote uendapo, kusaini mkataba na shetani
Na kweli ukiwaangalia hawa watu wanapona kwenye mengi lakini yakiwa ya kujikweza na yaliyojaa u binafsi mwingi, tupia jicho kwa wanasiasa wetu walio wengi na hata baadhi yao waliothubutu kutamka wazi kuwa 'wameaga kwao' pamoja na tambo zote hizi lakini huishi katika maagano na mikataba na viapo vya siri ambapo hata iweje kuna mambo huwa hawaruhusiwi kufanya huku wakitakiwa kwenye vipindi vya mwaka kufanya tambiko na kutoa kafara ya vitu mbalimbali na kwa asilimia kubwa ikiwa ni tambiko ama kafara linahusisha damu.
Between ulinzi wa kweli na usio na madhara yoyote kwa sisi waamini hukota kwa Mungu mwenye enzi yote
Je na wewe umeaga kwenu? Kuwa makini yasiwe ni majigambo matupu, jamaa huwa wana tabia ya kujaribu kuona kama ni kweli ama la!