WanaJF tungekuwa wakweli

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
10,759
18,595
Habari wapendwa!
Nimekaa nikatafakari kwa kutumia akili ya kawaida tu ( common sense), nikafikiri ambavyo ingekuwa vyema kama tungeishi maisha halisi humu,

Tungekuwa na uwezo wa kusaidiana kwa kupeana fursa na mipango mizuri ya kutuwezesha sisi kufanikisha mambo yetu kupitia network ambayo tungeitengeneza kupitia jamiiforums,

Mfano, kama mimi ni mkulima wa mahindi ningelikuwa na uwezekano wa kupata soko kwa watu wenye mashine za kukoboa au kupack nafaka na unga, wenye kampuni za ulinzi wangepata maeneo ya kutoa huduma hizo, wenye kampuni za udalali pia vivyo hivyo.

Tungekuwa na mahusiano yenye tija( mutual benefit) baina yetu wana jf, tungetengeneza jamii yenye kusaidiana kulingana na nafasi ya kila mmoja wetu.

Tatizo tunaishi fake life kiasi kwamba baadhi ya watu humu wameji brand hadhi fulani ambazo huenda hawana!

Kwa sisi wafugaji wa ng'ombe tungepata soko la maziwa na nyama hasa kwa walioko mijini hata kwa makubaliano maalumu ili wote tunufaike.

NB: Hii ingewezekana iwapo tungefahamiana physically, na kujiridhisha pasi na shaka kuwa wahusika mpo kwenye uhalisia ili kuepuka utapeli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama tungejiweka wazi, usingekuwa unapata baadhi ya taarifa /habari.

Nani ajiweke hadharani alafu aanze kumsema mzee baba au mwanaye? Hatma yake ni nini kama si kuuana au kuishia gerezani.

Japokuwa tu hatufahamiani lakini amini kuna watu wanatafutwa.

Tena yawezekana hata wazo lako tu, umelileta kwa kuwatafuta watu fulani.

Kama unataka live unahamia FB au Insta. Au kwenye ma-group ya WhatsApp.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio rahisi mkuu. JF kila mtu elimu yake chini ni shahada ya kwanza, kila mtu ana gari, kila mtu wazazi wake wamesoma, kila mtu hana shobo ya kuajiriwa amejiajiri mwenyewe, kila mtu... kila mtu...
Kweli kabisa! haya ndiyo matatizo yetu, ukweli ni kuwa kuna fursa nyingi sana zinapita kushoto kwa sababu ya kuwa na mahusiano yasiyo na faida yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina maana hiyo mkuu!
Kama tungejiweka wazi, usingekuwa unapata baadhi ya taarifa /habari.

Nani ajiweke hadharani alafu aanze kumsema mzee baba au mwanaye? Hatma yake ni nini kama si kuuana au kuishia gerezani.

Japokuwa tu hatufahamiani lakini amini kuna watu wanatafutwa.

Tena yawezekana hata wazo lako tu, umelileta kwa kuwatafuta watu fulani.

Kama unataka live unahamia FB au Insta. Au kwenye ma-group ya WhatsApp.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wapendwa!
Nimekaa nikatafakari kwa kutumia akili ya kawaida tu ( common sense), nikafikiri ambavyo ingekuwa vyema kama tungeishi maisha halisi humu,

Tungekuwa na uwezo wa kusaidiana kwa kupeana fursa na mipango mizuri ya kutuwezesha sisi kufanikisha mambo yetu kupitia network ambayo tungeitengeneza kupitia jamiiforums,

Mfano, kama mimi ni mkulima wa mahindi ningelikuwa na uwezekano wa kupata soko kwa watu wenye mashine za kukoboa au kupack nafaka na unga, wenye kampuni za ulinzi wangepata maeneo ya kutoa huduma hizo, wenye kampuni za udalali pia vivyo hivyo.

Tungekuwa na mahusiano yenye tija( mutual benefit) baina yetu wana jf, tungetengeneza jamii yenye kusaidiana kulingana na nafasi ya kila mmoja wetu.

Tatizo tunaishi fake life kiasi kwamba baadhi ya watu humu wameji brand hadhi fulani ambazo huenda hawana!

Kwa sisi wafugaji wa ng'ombe tungepata soko la maziwa na nyama hasa kwa walioko mijini hata kwa makubaliano maalumu ili wote tunufaike.

NB: Hii ingewezekana iwapo tungefahamiana physically, na kujiridhisha pasi na shaka kuwa wahusika mpo kwenye uhalisia ili kuepuka utapeli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona tunajuana humu mfano mdogo tu kama hawa members!

Nokia huyu tunamjua kama wewe humjui ni wewe tuu, yeye anafanya kazi ofisi nzuri anapanda lift kila siku ana saa nzuri kila siku mpya. Mweupe smart pia..mwangalie dp yake utajua, mtumie sms atakujibu hata ukitaka kumuona hana shida.

Sky Eclat
Huyu ni mdada ameenda age lakin ni mstaarabu tuu ukihitaj msaada wake utaupata mtumie txt tuu hana shida.

Wengine wengi tuu maarufu wako powa hata mimi pia(ingawa siyo maarufu)

Putin vladmir
Zero IQ
Miss Natafuta

Wote hawa wana roho nzuri wewe tuu kama unaogopa kuwafuata haya shauri yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa! haya ndiyo matatizo yetu, ukweli ni kuwa kuna fursa nyingi sana zinapita kushoto kwa sababu ya kuwa na mahusiano yasiyo na faida yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kupitia JF watu tunapata fursa ni wewe tu kuamua kuzitafuta kupitia majukwaa husika. Na huko unaweza kuweka taarifa zako upendavyo ukapata au kutumia fursa zilizopo na hatimaye kuweka mtandao mzuri wa kibiashara. Wengi wametumia majukwaa hayo na kufanikiwa.

Pia kupitia hii JF tunaweka na tunapata taarifa nyingi muhimu na nyeti. Kama tungekuwa tunaweka wazi taarifa zetu ingelikuwa ni ngumu sana kuweka, kupata au kuchangia kwenye hoja hizo labda kama utakuwa haujipendi. Hivyo ni suala la mtu binafsi kuamua.
 
Back
Top Bottom