WanaJF nisaidieni, naomba mnisaidie

WanaJF nisaidieni, naomba mnisaidie

WanaJF,

Nawaombeni kama watu wenye uwezo wa kufikiri mnisaidie kufikiri. Tafadhalini sana nawaomba mnisaidie katika hili. I believe this is a noble task.

Mimi ni kiongozi wa wanachi. Ni Diwani. Kata ya Mabogini kwa tiketi ya Chadema. Ni wakili wa kujitegemea. Wengi wanaamini ni kijana kutokana na kuzaliwa wakati vyeti vya kuzaliwa vinatolewa!

Nawaomba mnisaidie kufikiri kuhusu haya yafuatayo;

1. Kata yangu ina shule 2 za sekondari za kata. Matokeo ya kidato cha nne mwaka huu Div Zero ni 70 kwa 76 shule zote mbili.

2. Kuna shule ya primary, Fredrik Sumaye ina watoto wa darasa la 1 na la 2 zaidi ya 100 lakini ina jengo la darasa moja. Leo hii!

3. Shule zote za primary kwenye kata yangu hazina vyoo vya uhakika. Vimejaa. Walimu na wanafunzi wanatumia vyoo kwa pamoja. Shule ina wanafunzi 500 ina matundu sita ya choo.

4. Kata yenye wananchi zaidi ya elfu kumi na tano haina ward ya kujifungulia kina mama. Dispensary moja ina chumba kina 'ward' haina sink la kunawa mikono, choo ni cha nje cha kuchuchumaa. Kipo zaidi ya hatua ishirini!

5. Zimetengwa mil 60 kujenga kituo cha afya. Kwa mfano tuseme sawa zinatosha kujenga jengo la OPD, wodi za watoto, kina mama na wanaume je watakaolazwa wakizidiwa usiku inakuwaje? Kuna vituo vya afya kibao havijalaza mgonjwa kwa zaidi ya mwezi! Ila serikali inataka kila kata iwe na kituo cha afya.

6. Serikali za vijiji haziitishi mikutano mikuu ya vijiji. Wananchi hawajui chochote kuhusu mapato na matumizi! Sheria inasema mkutano mkuu wa kijiji angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu.

7. Upungufu wa walimu. Shule ina walimu 9 wa primary. Wanafunzi wako kati ya 450 na 700. Tatizo ni shule zote.

8. Kila mtoto anatakiwa kuchangia sh 9500 kwa ajili ya mlinzi, uji/ugali maharage mchana na mpishi. Wazazi wanaomba wapewe muda mpaka tarehe 15 kupata hiyo hela! Hawana.

9. Asilimia 90 ya wananchi wa kata yangu ni wakulima. Mvua ndio hizo. Kama hakuna mvua then hakuna kilimo. Wanakuwa kina nani?

10. Maji ya kunywa ni shida. Kuna visima vichache ila wamekatiwa umeme. Hawana uwezo wa kulipa bill.

11. Kuna dispensary (yenye wodi isiyo na sink na choo ndani) bila choo cha nje as first phase. Second phase ndio ujenzi wa choo unaoendelea. Choo ni cha kuvuta so wanahitaji pump ya maji na tenki! Havipo kwenye bajeti. Kwa kuanzia wabebe maji na ndoo. Lakini pia, wamekatiwa umeme toka oktoba wanadaiwa laki 120. Hapo hawakuwa na pump ya maji.

Na mengine mengi, mengi tu.

Mimi binafsi inaniuma sana. Hiyo ndio hali ya huko walipo wananchi ambao hii ni nchi yao. Mbunge leo anachukua mkopo wa milioni 90.

Nisaidieni kufikiri. Mfikirieni mwananchi wa Mabogini kama kielelezo cha wananchi katika kata na mitaa yetu. Mfikirie mtanzania masikini. Mfikirie anayepanga. Mfikirie Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri au Manispaa. Mfikirie Waziri, mfikirie Raisi.

Fikiria siasa za nchi hii. Fikiria viongozi na wasomi wa nchi hii. Nisaidieni kufikiri.

Nimeona ni bora niombe msaada wenu kufikiri. Najiuliza, kama Diwani niko sehemu sahihi na elimu yangu? Je walioniambia 'Albert kagombee ubunge una maslahi' au 'Albert bungeni utatuletea maendeleo kwetu' walikuwa sahihi? Ni wangapi wametelekeza kata na vijiji vyao kwa ajili ya maslahi na kuamini kwamba ndio njia ya kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia Bunge?

Kwa hali hii tutafika? Nini tufanye wanaJF, wasomi, viongozi, wanaharakati nk!

Sio lazima upost fikra zako hasa zikiwa za matusi au kejeli. Wafikirie walio kwenye kata yako. Jifikirie mwenyewe!

Albert hayo matatizo yako yote ukitulia kama diwani na kuwachukulia watu kama resource na siyo mzigo ama sehemu ya tatizo kuya solve at 50% ndani ya muda wako wa udiwani ni rahisi. Abert usisolve matatizo ya wananchi wako kwa kuangalia selfishness ya wachache ambao hata hivyo kwa mfumo wetu lazima waendelee kuwepo mpka tutakapo kubali/lazimika kubadili mfumo; dawa ni kuwa onyesha njia ili hatimaye na wao wakuunge mkono kwa kuona unawavua nguo hazarani...how by being creative na kuwa action oriented. Cash is a good facility to solve problems hata hivyo by itself has never been able to solve problem.

Najitolea kukusaidia kimawazo at individual level jinsi ya kuondoa hizo problems permanantly ili uwe na legacy hapo Mabogini; Moshi ni partly nyumbani kwetu so nitegemee siku yeyote nitakutembelea.
 
LAT, nakushukuru sana sana. Nafarijika mno ninapoona kwamba wapo watu ambao wako tayari kusaidia maendeleo ya nchi yetu.

Tuliobahatika kupata elimu tuna moral obligation ya kusaidia regardless ya itikadi.

Naamini kama wanaJF tukiamua kuchangia maendeleo hata kwa kujitolea muda wetu italeta mabadiliko.

Nimeandaa utaratibu wa 'jumamosi ya diwani' kwa wanafunzi wa darasa la saba na form four. Lengo ni kuzungumza nao as a brother and friend. Make them believe kwamba inawezekana regardless ya mazingira magumu. I did it kwenye mazingira kama yao.

Nakuhakikishia the impact is massive. Watoto wa shule ya msingi are my friends and you should see their faces when promising me to perform. I abruptly step in a school during break time and all will come running showing me their books.

I wish some JF members could make these trips. Nchi yetu ina umasikini wa fikra lakini tunaweza kujikwamua kwa kufanya mambo madogo ambayo hayahitaji fedha wala uwezo mkubwa!

Hapo ndipo ninapoungana na wewe kwa hili. Wahanga wa janga hili wawe ndio walengwa wa elimu unayotaka kutoa. Watoto wetu wakielimishwa wanaelewa ingawa walizoea kutwambia vijana taifa la kesho! na hata tunapokaribia nasi kuzeeka wao hawataki kuachia yaliyowashinda! Ajabu sana, mtu anajifikiria yeye tu wala haoni msururu wa wanajamii ulio nyuma yake.
Kwa kuanzisha JUMAMOSI YA DIWANI angalao utawapa mwanga vijana. Na hili linawezeka kabisa. Huwezi kunambia hata kama tungekuwa maskini kiasi gani tutashindwa kulipa shs 9500 kwa ajili ya elimu ya mwanetu. Mzazi aelewe tu 9500 ni chibuku ngapi za mbege! Akipata mwamko atachangia hata kwa kupeleka shs 1000 kila wiki na atamaliza deni. Nilikuwa shule fulani kule umasaini. Tena shule ya secondary, Mh Mwandri alikuwepo siku hiyo. Mkuu wa shule akasema wazazi wanashidwa kulipa ada ya watoto wao. Ajabu ni kuwa kumbe akina mama wa kimasai wanajua adha za waume zao, wakaahidi kila mmoja kuleta mbuzi ama kondoo au hata ngombe. Niliporudi siku chache pale nilikuta kundi kubwa la ngombe na mbuzi nikaambiwa ni za shule na sasa zimewazidi hivyo inabidi kuuzwa zipishe nafasi. Ilipotangazwa kuwa zitauzwa wanaume walewale wa Kimasai ndo walinunua ile mifugo! Fedha walipata wapi? Ni mwamko wa jamii husika ndo lengo kwanza. Kosa kubwa ni kuwa hawajaona faida ya watoto wao kusoma! Faida gani mzazi anauza mpaka kuku mtoto asome halafu anamaliza chuo kikuu na kufaulu vizuri lakini hana kazi! Ajira hakuna! hakuna mtu wa mfano wa kufananisha hapo kwao. Unajua watu nao wanatamani kuwa kama fulani! mfano mwone mtoto wa fulani kasoma mpaka chuo kikuu unaona maendeleo yake! kama anakunywa gongo utasikia faida gani kusoma halafu uishie kunywa gongo!
Viongozi walioko madarakani wanaogopa kupata wasomi wengi kwa kuwa ajira zao zitakuwa mashakani! Just 1 scenario na hili halina ubishi! Miaka ya nyuma niliwahi kuambiwa kuna kazi mahala fulani, nikapeleka applications zangu na vyeti pia. Kumbe boss wa pale kielimu nimempita mbali sana. Amini usiamini wala sikuambiwa njoo kwenye interview! Yule aliyenambia kuwa kuna kazi akanilaumu kwa nini siku- apply nikamwambia nilipeleka barua. Walipofanya uchunguzi wakabaini kuwa kuna mtu alizima barua yangu. Kwa kuwa walikuwa wanahitaji mtu wa aina yangu wakaniita kama board wakaniinterview. well nilipata kazi ila sasa ikawa vita yangu na ya meneja wa pale. Tifutifu la kiaina mbaya nilipokuja kuwa juu yake ndo akaanza kunitumia matisho.
Tuanze elimisha wanetu. Niko pamoja na wewe mkuu. Tutafutane kwa mawazo na ushauri pia. Niko Moshi mjini.
 
Wewe jamaa nakutamani nikupe knuckles za pua!! Nakwambia utatafuta pa kukimbilia kipenga kikilia.

Unaonaje ukini PM nikujulishe nilipo halafu tuonane uso kwa uso..usikimbia falangati ikianza dude..
 
unaweza anzisha mfuko na fungua account chini ya jina la kata yako "Mabogini" halafu weka hiyo account namba humu ndani tutaona jinsi ya kukusaidia hata $ 10 tutakusaidia

Hii ni falsafa ya ombaomba must end!

Hapo hapo alipo kuna pesa za kutosha kusaidia watu wake...achemsha akili aache kulialia na kuombaomba

Aangalia remittance zote kutoka serikalini kuu kwenda jimboni mwake, a-negotiate na local goverments namana bora ya kuendesha mambo
 
Najaribu kuzifikiria kata nyingine. Uzembe, kutokujali, ubadhirifu, mipango isiyo na fikra, kutokujua nk si tu kwenye kata yangu. Ni kila mahali.

Nitakupa mfano;

Mganga wa wilaya, kijana na mtu ambaye anaonekana ni msomi wa umri wetu alisoma ripoti yake ya miezi mitatu. Amekagua vyoo elfu 22+. Akaisoma ripoti kwa madaha sana. Alipomaliza nikamuuliza, 'daktari, umetembelea choo cha halmashauri?' 'unaweza kusema hali yake ni nzuri, ya kuridhisha au duni kwa vigezo vyako?'...akakaa kimya. Mkurugenzi akaingilia kati akaomba msamaha na kuahidi kwamba choo cha halmashauri ambacho ndicho wanatumia watendaji kitafanyiwa marekebisho. The rest you can figure out. Huo ndio utendaji wetu!

samahani Mkuu, Mhe Diwani kama nitakuhudhi, unisaheme sana nakushauri mambo uliyoongea na Mkurugenzi najinsi ulivyojibizana na watendaji sidhani ni vyema kuyalipoti wewe mwenyewe kwa staili hii uliyotumia, hasa kwa kwakusema fulani kasema hiki kufani kajibu hili tunapambana na Mfumo sio watu, huo ndio ushauri wangu kwa leo kama utaona unakufaa nitaendelea kukushauri kama unaona haufai basi ndio mwisho wangu wa kushauri maana umeomba ushauri.
 
samahani Mkuu, Mhe Diwani kama nitakuhudhi, unisaheme sana nakushauri mambo uliyoongea na Mkurugenzi najinsi ulivyojibizana na watendaji sidhani ni vyema kuyalipoti wewe mwenyewe kwa staili hii uliyotumia, hasa kwa kwakusema fulani kasema hiki kufani kajibu hili tunapambana na Mfumo sio watu, huo ndio ushauri wangu kwa leo kama utaona unakufaa nitaendelea kukushauri kama unaona haufai basi ndio mwisho wangu wa kushauri maana umeomba ushauri.
Nenda kulala watu kama wanaongea wongo wanapaswa kuanikwa humu ndani hakuna mambo ya siri siri ndo maana tunaibiwa kila siku na mikataba feki!
 
Nenda kulala watu kama wanaongea wongo wanapaswa kuanikwa humu ndani hakuna mambo ya siri siri ndo maana tunaibiwa kila siku na mikataba feki!

Mbona wewe unanishauri mimi badala ya kumshauri aliyeomba ushauri!!; au ndio tuseme hujaelewa maada au?, au hujanielewa mimi Ushauri wangu! kwanini husiniulize nina maana gani kama unashida ya kujua kwanini nimeshauri hivyo unapachika maneno yako unayotaka wewe kuwa ndicho ninacho maanisha, hivyo kupotosha maana halisi ya Ushauri wangu, ningekutukana lakini Dini yangu na JF hairusu ila umepotosha maana ya Ushauri wangu kwa kuto kujua kwako!
 
Husniyo,

Sheria ya kodi ya mwaka 2004 ianaeleza vizuri kwamba mtu mwenye kipato cha zaidi ya sh 720,000 atatozwa kodi kama ifuatavyo


Kwanza atatozwa fixed amount ya 120,000/=

Kiasi hiki kitajumlishwa na tofauti kati ya mshahara wake baada ya kutoa makato ya NSSF kama sheria inavyoagiza na sh 720,000 ( makato haya ya mfuko wa jamii sio kwamba yamesamehewa kodi bali fodi yake imekuwa differed mpaka wakati wa kuchukuwa malipo ( Final with holding -pitia sec 86 ya Income tax act -2004 )

Hivyo basi kama wabunge wangekuwa wanakatwa kodi na kuchangia mifuko ya jamii basi salary slip yao ingeonekana hivi


Jina la Mbunge >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Figures in Tsh

Mapato Ghafi 12,000,000
Toa : Mchango mfuko wa jamii (10%) (1,200,000)
Salio linalotozwa kodi 10,800,000

Makato ya lipa unavyopata (PAYE) 3,144,000 ( formula= 120,000+(10,800,000-720,000)*30%

Salio la kwenda nalo home 7,656,000

Hivyo kama sheria hiyo ya kumkata mfanyakazi ingeenda hadi kwa wabunge basi kila mmoja angechangia taifa hili 3,144,00 kila mwezi na kwa wabunge 200 ni shilingi za kitanzania 628,800,000 kwa mwaka ni Tsh 7,545,600,000 hizi ukizegeuza vituo vya afya ukasema kila kituo cha afya kitajengwa kwa Sh milioni 60 then kwa mwaka mmoja tu utakuwa umejenga vituo vya afya 125,je kwa miaka 5? na kama utaamua kusema walipie na magari yao ushuru ni kitu kingine kabisa.Hata kama watapata excemtion ya import duty ambayo sheria inasema ni 25% na excise duty ya 10% kama wafanyakazi wengine wanavyopewa bado watalipa VAT ya 18% ambayo haina exception na hapa unaweza kuokoa mamilioni kadhaa ukayafanya huduma.

Hivyo mfumo wetu upo ovyo,wabunge hawalipi kodi yeyote kujenga nchi wakati mwalimu wa kima chini anasamehewa kodi kwenye Sh 100,000 tu kama kunakinchozidi hapo kinapigwa asilimia 14 kinarudi serikalini.Kwa hayo tuanapata kuona kazi tulionayo.kwamba wabunge wafike mahali waone wanaibia maendeleo ya nchi hii.waache tamaa ! wakubali kulipa kodi.La sivyo tutawapa kazi kubwa sana watendani wa ngazi ya chini kwani ndio wako karibu zaidi na wananchi.
 
Back
Top Bottom