WanaJF nisaidieni, naomba mnisaidie | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WanaJF nisaidieni, naomba mnisaidie

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Feb 15, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Nawaombeni kama watu wenye uwezo wa kufikiri mnisaidie kufikiri. Tafadhalini sana nawaomba mnisaidie katika hili. I believe this is a noble task.

  Mimi ni kiongozi wa wanachi. Ni Diwani. Kata ya Mabogini kwa tiketi ya Chadema. Ni wakili wa kujitegemea. Wengi wanaamini ni kijana kutokana na kuzaliwa wakati vyeti vya kuzaliwa vinatolewa!

  Nawaomba mnisaidie kufikiri kuhusu haya yafuatayo;

  1. Kata yangu ina shule 2 za sekondari za kata. Matokeo ya kidato cha nne mwaka huu Div Zero ni 70 kwa 76 shule zote mbili.

  2. Kuna shule ya primary, Fredrik Sumaye ina watoto wa darasa la 1 na la 2 zaidi ya 100 lakini ina jengo la darasa moja. Leo hii!

  3. Shule zote za primary kwenye kata yangu hazina vyoo vya uhakika. Vimejaa. Walimu na wanafunzi wanatumia vyoo kwa pamoja. Shule ina wanafunzi 500 ina matundu sita ya choo.

  4. Kata yenye wananchi zaidi ya elfu kumi na tano haina ward ya kujifungulia kina mama. Dispensary moja ina chumba kina 'ward' haina sink la kunawa mikono, choo ni cha nje cha kuchuchumaa. Kipo zaidi ya hatua ishirini!

  5. Zimetengwa mil 60 kujenga kituo cha afya. Kwa mfano tuseme sawa zinatosha kujenga jengo la OPD, wodi za watoto, kina mama na wanaume je watakaolazwa wakizidiwa usiku inakuwaje? Kuna vituo vya afya kibao havijalaza mgonjwa kwa zaidi ya mwezi! Ila serikali inataka kila kata iwe na kituo cha afya.

  6. Serikali za vijiji haziitishi mikutano mikuu ya vijiji. Wananchi hawajui chochote kuhusu mapato na matumizi! Sheria inasema mkutano mkuu wa kijiji angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu.

  7. Upungufu wa walimu. Shule ina walimu 9 wa primary. Wanafunzi wako kati ya 450 na 700. Tatizo ni shule zote.

  8. Kila mtoto anatakiwa kuchangia sh 9500 kwa ajili ya mlinzi, uji/ugali maharage mchana na mpishi. Wazazi wanaomba wapewe muda mpaka tarehe 15 kupata hiyo hela! Hawana.

  9. Asilimia 90 ya wananchi wa kata yangu ni wakulima. Mvua ndio hizo. Kama hakuna mvua then hakuna kilimo. Wanakuwa kina nani?

  10. Maji ya kunywa ni shida. Kuna visima vichache ila wamekatiwa umeme. Hawana uwezo wa kulipa bill.

  11. Kuna dispensary (yenye wodi isiyo na sink na choo ndani) bila choo cha nje as first phase. Second phase ndio ujenzi wa choo unaoendelea. Choo ni cha kuvuta so wanahitaji pump ya maji na tenki! Havipo kwenye bajeti. Kwa kuanzia wabebe maji na ndoo. Lakini pia, wamekatiwa umeme toka oktoba wanadaiwa laki 120. Hapo hawakuwa na pump ya maji.

  Na mengine mengi, mengi tu.

  Mimi binafsi inaniuma sana. Hiyo ndio hali ya huko walipo wananchi ambao hii ni nchi yao. Mbunge leo anachukua mkopo wa milioni 90.

  Nisaidieni kufikiri. Mfikirieni mwananchi wa Mabogini kama kielelezo cha wananchi katika kata na mitaa yetu. Mfikirie mtanzania masikini. Mfikirie anayepanga. Mfikirie Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri au Manispaa. Mfikirie Waziri, mfikirie Raisi.

  Fikiria siasa za nchi hii. Fikiria viongozi na wasomi wa nchi hii. Nisaidieni kufikiri.

  Nimeona ni bora niombe msaada wenu kufikiri. Najiuliza, kama Diwani niko sehemu sahihi na elimu yangu? Je walioniambia 'Albert kagombee ubunge una maslahi' au 'Albert bungeni utatuletea maendeleo kwetu' walikuwa sahihi? Ni wangapi wametelekeza kata na vijiji vyao kwa ajili ya maslahi na kuamini kwamba ndio njia ya kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia Bunge?

  Kwa hali hii tutafika? Nini tufanye wanaJF, wasomi, viongozi, wanaharakati nk!

  Sio lazima upost fikra zako hasa zikiwa za matusi au kejeli. Wafikirie walio kwenye kata yako. Jifikirie mwenyewe!
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi issue sio Milioni 90 tu hata hizo 12 Million a month kama mshahara ni kubwa mno na wabunge ni wengi sana..., kwahiyo ushauri wangu ni kupunguza matumizi tuanzia kwenye mishahara yao hawa waeshimiwa alafu baadae itabidi hata viti maalumu viangaliwe upya..
   
 3. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Dah
   
 4. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  viti maalumu nalo neno.

  VoiceofReason nakubaliana nawe tujadili kuona je uwakilishi ni quality au quantity? Uwakilishi wa makundi katika nchi masikini kama yetu inakuwaje?
   
 5. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #5
  Feb 15, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mh. Diwani, nitatuma maoni yangu baadae kidogo.
   
 6. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mkuu upo sehemu sahihi kwa wakati sahihi...wanasiasa wenye kujali maslahi na kubeba mizigo ya mananchi ni mboni katika jamii zao...kuna mengi yanayoenda ndivyo sivyo ila ni nani wa kutufumbua macho km sio ninyi!...napata hasira sana naposikia kiongozi wa umma akiingia kwenye kashfa ya kuhujumu umma na bila aibu wala haya anajitokeza kwenye vyombo vya habari kubariki/kutakasa madudu yake!....sio lazima kuanza A kwenda Z wakati mingine unaweza kuanzia Z kuja A...upo sehemu stahiki mkuu Alberto!
   
 7. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Najaribu kuzifikiria kata nyingine. Uzembe, kutokujali, ubadhirifu, mipango isiyo na fikra, kutokujua nk si tu kwenye kata yangu. Ni kila mahali.

  Nitakupa mfano;

  Mganga wa wilaya, kijana na mtu ambaye anaonekana ni msomi wa umri wetu alisoma ripoti yake ya miezi mitatu. Amekagua vyoo elfu 22+. Akaisoma ripoti kwa madaha sana. Alipomaliza nikamuuliza, 'daktari, umetembelea choo cha halmashauri?' 'unaweza kusema hali yake ni nzuri, ya kuridhisha au duni kwa vigezo vyako?'...akakaa kimya. Mkurugenzi akaingilia kati akaomba msamaha na kuahidi kwamba choo cha halmashauri ambacho ndicho wanatumia watendaji kitafanyiwa marekebisho. The rest you can figure out. Huo ndio utendaji wetu!
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Mkuu Alberto ...Heshima kwanza.... mimi sina mengi zaidi ya action plan to rescue this situation ..... kwa busara zangu kidogo sana tafadhali anzisha mfuko maalum ambao utapata harambee kutoka kwa wanamapenzi wa maendeleo na kufuta umaskini tukianzia humu JF ambako tumetumia resource nyingi sana za kiakili kuleta chachu ya maendeleo katika jamii ya watanzania.. nikiamini pia wengi wetu humu JF pia wanauwezo angalau wa kujitolea chochote mifukoni.., huu mfuko utakuwa ni wa wananchi wote usiojali itikadi ... lakini utakua na msukumo mkubwa katika mafanikio kutoka kwa wana CDM nchi nzima... hii itakuwa ni set point ya mfano kwa nchi kwamba nguvu ya umma inaweza kuleta mapinduzi ya maendeleo ya jamii kwa nguvu ya mifuko yao na sio tu kuleta mapinduzi ya demokrasia ....serikali yetu sasa hivi ni rojorojo... huwezi itegemea hata kidogo..... mradi wa uwezeshaji wa shule hizi mbili utajitangaza nchi nzima na kutumika kama kurunzi ya mapinduzi ya elimu ya msingi

  shinning example, yes a shinning example... and will always be a shinning example
   
 9. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  LAT, nakushukuru sana sana. Nafarijika mno ninapoona kwamba wapo watu ambao wako tayari kusaidia maendeleo ya nchi yetu.

  Tuliobahatika kupata elimu tuna moral obligation ya kusaidia regardless ya itikadi.

  Naamini kama wanaJF tukiamua kuchangia maendeleo hata kwa kujitolea muda wetu italeta mabadiliko.

  Nimeandaa utaratibu wa 'jumamosi ya diwani' kwa wanafunzi wa darasa la saba na form four. Lengo ni kuzungumza nao as a brother and friend. Make them believe kwamba inawezekana regardless ya mazingira magumu. I did it kwenye mazingira kama yao.

  Nakuhakikishia the impact is massive. Watoto wa shule ya msingi are my friends and you should see their faces when promising me to perform. I abruptly step in a school during break time and all will come running showing me their books.

  I wish some JF members could make these trips. Nchi yetu ina umasikini wa fikra lakini tunaweza kujikwamua kwa kufanya mambo madogo ambayo hayahitaji fedha wala uwezo mkubwa!
   
 10. m

  mshewa Member

  #10
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naamini upo sehemu muafaka kwa mwanasiasa. kwamua tatizo moja kwa ufasaha zingatia muda wako wa uongozi, usije ukakosa cha kuwaambia wananchi kampeni zikianza. kumbuka muda ni mfupi sana.:msela:
   
 11. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Kwakweli hali ni mbaya na sio sehemu moja.
  Ubaya wa hawa watu wanakula halafu hatuoni wanachokifanya.
  Mimi nafikiri ingekuwepo sheria itakayowataka wabunge wachangie asilimia fulani za mishahara yao ambayo itatumika moja kwa moja kwa maendeleo ya majimbo yao huku wakiendelea kusubiria hizo bajeti.
  Kwa mfano kama mbunge anapoke 12m per month, akichangia let say 30%
  30% ya 12m = 3.6m
  kwa mwaka mzima 3.6m times 12= 43,200,000.
  Kwa kata kama uliyoielezea hizo 43.2m zinataweza kusaidia kuongezea madarasa na huduma zingine.
  Tukichukua hizo 43.2m tuzidishe kwa miaka yao mitano= 216m.
  Kwahiyo fungu lao kutoka serikalini na percent watakazochangia zitasaidia sana kupiga hatua katika majimbo yao.
   
 12. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Siasa ni kazi ya wito...mtu anapojitoa kuomba ridhaa ya kuongoza watu ni kwamba anajua na kutambua dhana ya uongozi...kwamba ameona mambo yanayotendeka ndivyo sivyo ama pasi ufanisi uliostahili dhidi ya jamii husika...Wazo la kufungua mfuko ni zuri ila nadhani yafaa zaidi kama viongozi mkawa na ushirikiano katika ngazi zote ili kufanikisha lengo kuu ambalo ni kumkwamua mwanachi wa kawaida
   
 13. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Alberto, utashangaa ukiinvest muda na uwezo wako kuijua bajeti ya halmashauri yako hayo matatizo yote utayatatua ndani ya miaka miwili tu bila hata kuomba michango kutoka kwa mtu yoyote. Lakini uwe tayari kweli kweli kupambana na wakuu wa idara, mkurugenzi na meya wako (ambaye umemshitaki). Usisahau mara zote kutanguliza wananchi mbele ili wakikuundia jungu basi wakutetee
   
 14. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama Diwani najiuliza kazi ya Mbunge ni nini? Kuleta maendeleo jimboni? Anayaletaje? Na kazi ya serikali ni ipi?

  Je kazi ya Mbunge si uwakilishi kama ilivyo ya diwani? Hizi gharama kubwa tunazoingia kuwalipa wabunge mishahara ya mil 12 (pamoja na marupurupu) ni za lazima? Kwa nini tusijiulize upya kama tuko sahihi?
   
 15. L

  LUMBAKALA Senior Member

  #15
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 147
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa mimi nimekupata na kwa vile umeomba msaada wa mawazo tutajaribu kukusaidia.Mkuu mi kwa mawazo yangu kwa vile wewe ni diwani,na umeyaona matatizo ya hizo shule cha kufanya ujitume kama mleta maendeleo kwa wananchi wako na kujenga jina la CHADEMA kwa ajili ya mwaka 2015.Waitishe wananchi wako mikutano uwaelezee mitizamo uliyoiona na natumaini hakuna jambo la kimaendeleo utakalo waambia wananchi watapinga sijui ila huo ndio muhimili wa maendeleo.Kama ulivyosema maisha ya watu wako ni duni basi itisha hata harambee za kuchangia mambo muhimu na fedha hizo za michango zifanye kazi kweli nasi ubadhirifu. Chapa kazi kweli kweli na kazi ikionekana Wananchi ndo wasema ukweli. Heshima hailetwi kwa kukaa tu bali heshima huletwa kwa kuchapa kazi.Huo ndo mtizamo wangu na msaada ulotuomba wana JF ahsante
   
 16. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mkuu Alberto tunataka viongozi wenye uthubutu wa mambo na wanaoweka maslahi ya umma mbele kwanza kabla ya kujiangalia wao....iliwagharimu maisha kina Abraham Lincolin,kina Garang, Machel Samora na wengi wengine walioweka uzalendo mbele....mkuu,natunza nyayo zako kuelekea ukombozi...usiache njia ya kweli...tunaopenda mabadiliko tuko nyuma yako,tutakukumbusha!
   
 17. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mh tunahitaji kwenda kijijini tulipotoka tukaangalie hali halisi maana huku town huenda hatujui ya kuhoko, Alberto umenifanya hivi vibia 2 ninavyokunywa nijifikirie mara mbili.
   
 18. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wazo zuri sana,tenaaa litakusaidia kuweza kuwasaidia wananchi wa kata yako kwa namna moja ama nyingine na piaaaaaaaa,....on the other side its a political uplift,....jiulize umewahi kusikia diwani anae vuma kwa kufanya jambo lolote?

  Try this,am sure ukielezea hali kama hizi kwa waandishi wa habari utapata harambee ya kutosha tu
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Jaribu kuongea na Mwl. Mkuu wa shule hiyo ili aweze kupanga siku maalum ambapo wanafunzi wote watashiriki katika uchimbaji wa vyoo vingine ili kukidhi haja ya shule hizo. Gharama za ujenzi wa kuta na paa unaweza kuitisha harambee kwa wakazi wa kata husika.

  Zaidi jaribu kuangalia bajeti ya mfuko wa maendeleo ya wadi yako inayotolewa na Halmshauri ya mji wako ina viupa umbele gani, unaweza kupata fedha humo ili kuondoa kadhia hiyo.

  Hili ni suala la kufuatilia tu, Hivyo panga siku ambayo utafuatilia suala hili kwa viongozi wa vijiji hivyo ili uweze kujua ni kwa nini mikutano hiyo haifanyiki.
   
 20. Madago

  Madago Senior Member

  #20
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Alberto mchakato ulioutoa ni mzito na nina uzoefu pia katika kata nilizowahi kukaa. Katika kata yangu nilichogundua kuna tatizo la kimfumo wa kifikra baina ya watendaji wa halmashauri na wananchi. hili nafikiri ni madhara ya partisan politics. Wale wanaokalia nafasi kujiona the people are at their mercy. Pamoja nakua halmashauri inajua ni wajibu wao wananchi hawana mwamko wa kudai kile kilichoainishwa kama matumizi ya halmashauri yao. Moja linalofanyika niku hamasisha wanachi wa wahold responsible watu wa halmashauri kwa kufuatilia bajeti na matumizi (budget tracking) ya hela katika kila activity ya halmashauri. Kunatakiwa kuwe na chombo cha kufuatilia ambacho hiki kikiona mapungufu kinaenda kushtaki kwa wananchi. lazima watumishi wa serikali za halmashauri wafanywe kuwa responsible kwa wanachi- na wananchi wawe empowered kudai huduma za jamii (social service delivery). Kwa wenzetu kama Afrika kusini ukifuatilia katika vyombo vya habari wananchi wa vitongoji mbalimbali wanafanya migomo na maadammano wakidai huduma za jamii zitolewe na councillors wanakua katika hali ngumu maana jamaa wanfikia hatua mpaka ya kuchoma moto nyumba zao. Ukikalia kiti cha ucouncilor mwenyewe unatia akili.
   
Loading...