WanaJF Lissu ni member mwenzetu, tumpe sapoti pia!!

Nyakageni

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
15,045
5,092
Amani kwenu wanabodi,

Tundu Lissu ni ni mwana chama mwenzetu. Ana kesi mahakamani ya kututetea wote humu ndani ili tuwe huru. Ni moja ya mawakili anayemtetea @Maxence Mello na Mike ambao ni mabosi wetu humu ndani kwa maana ya wakurugenzi wa Jamii Media (wamiliki wa Jamiiforums)

Kwa moyo safi na dhabiti tuoneshe Umoja wetu kwa kuwaomba wakurugenzi wetu Mike na Mello watoe mwongozo na ku stick uzi huu ili kila member apate nafasi ya kuchangia ili kuokoa uhai wa mwana JF mwenzetu Tundu Antipas Mughwai Lissu ambaye yuko katika wakati mgumu sana wa kupambana na uhai na pia kuepuka ulemavu

Nawaomba tusisubiri afariki (Mungu aepushie mbali) ili tubadili muonekano kama ilivyokuwa kwa Regia Mtema ((RIP) na kupamba jukwaa kwa pole.

Lissu needs us, nasi tumsaidie. Kwa ambao tumeshatoa kwenye njia zingine tuendelee tu kutoa ili kuokoa maisha ya mwenzetu na kuonesha Umoja wetu

Tusikae kimya kama tulivyokaa kimya kwa Ben Saanane (mwanachama pia) aliyepotea na Wana chama wenzake hatujachangia hata kumtafuta


Ningependa zoezi hili liratibiwe na Max pamoja Mike na baada ya kutuma pesa confirmation ya mlipaji iwe kwa kutumia haya majina yetu ya bandia na SI KAMA YANAVYOONEKANA MPESA TIGO PESA, HALO PESA NA AIRTEL MONEY

Binafsi nitafurahi sana kuona wanachama wetu kama @Mwanakijii, @Dr.W.P.Slaa,Josephine, Malisa GJ, Yericko Nyerere, Mwigulu Nchemba, Prof Tibaijuka, TCRA, John Mnyika @ wazee wa chit chat na MMU, FaizaFoxy, Zitto Kabwe, freeman Aikaeli Mbowe, @ Nape Nnauye, Humphrey Polepole, kahtaan, Kigwangalla, @Startimes, pascal Mayala, ONTARIO, CHIEF MKWAWA, na members wengine wote

Tahadhari : Taarifa ya kiasi na jina itumwe inbox ya wahusika au kwa njia za WhatsApp (haidukuliki)

Tuokoe maisha ya mpigania haki za wanyonge na jemedari wetu Tundu Antipas Mughwai Lissu

Nakaribisha maoni ya namna ya kuboresha zoezi hili...... Tulenge kujenga na si kuonesha umashuhuri wa tofauti zetu. United we stand, divided we fall


Mwisho naomba katika uzi huu tuache tofauti zetu za kisiasa na kusaidia kuokoa maisha ya mwenzetu Tundu Lissu ambaye ni wakili wa kesi zinazoikabili Jamiiforums pia

"Eeeeeeehhhh Mungu muweza wa yote tenda miujiza kwa kuokoa uhai wa mwana Jamiiforums mwenzetu Tundu Lissu ili apone haraka na kupona kabisa"

Na wote tuseme Amen



Nyakageni
 
imhotep hao Bakwata hawana utofauti na mafarisayo...mufti wake sidhani kama atakuwa na jipya,si ulimuona siku ya uapishwaji wa CJ?
Analinda kitumbua chake!
 
Mtusaidie hata sisi tulioko Chirundu border post namna ya kuchangia. Na hata wana JF walioko Auckland nao muwape muongozo namna ya kuchangia.

Ndondondo si chururu!
 
Tunakuombea Lissu na tutakuchangia pia...
tumblr_o7yqli810w1s94jl7o1_400.jpg
 
Nakubaliana na wazo hili. Nadhani ni vyema uongozi wa JF nao ukitupa mwongozo wa jambo hili.
Tundu Lissu ni mpigania haki ya uhuru wetu wakujielezana, sasa anatuhitaji sisi kama vile yeye alivyojitolea awali kutupigania bila malipo.
 
Back
Top Bottom