wanaJf embu tuweka mambo tunayoyataka kwenye katiba mpya

Wizzo

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
723
255
1. Rais apunguziwe madaraka
2.mawaziri wote wasiwe wanasiasa
3.wakuu wa mikoa na wilaya wawe wenyeji wa eneo husiku na wasiteuliwe bali wachaguliwe na wasiwe wanasiasa
4....tuendelee
5.
 
1. Rais apunguziwe madaraka
2.mawaziri wote wasiwe wanasiasa
3.wakuu wa mikoa na wilaya wawe wenyeji wa eneo husiku na wasiteuliwe bali wachaguliwe na wasiwe wanasiasa
4.vipindi vya ubunge viwe vi2 tu miaka mitano mitano
5.matokeo ya uchaguzi wa rais yathibitishwe na mahakama ya rufaa au mahakama ya katiba

6.mikataba yote ya serikali ijadiliwe na bunge
7.wagombea wote wa kiti cha urais watakaopata asilimia tatu wawe wabunge
 
8.viti maalum viondolewe 9.ili kuwepo usawa kati wanaume na wanawake Majimbo ya uchaguzi kila mkoa yagawanywe kwa mfano mkoa wa Arusha una majimbo sita basi matatu yawe ya wanaume na matatu yawe ya wanawake Kama wabadilishane kila baada ya miaka mitano 10.umri wa kupiga uanzie miaka 16 Na kuendelea 11.mwanachama wa chama chochote aruhusiwe kuhamia chama chochote bila kuathiri wadhifa atakaokuwa nao 12.katiba isibadilishwemara kwa mara 13. katiba itamke kuwa lugha ya kiswahili ndio lugha ya Taifa na viongoz
 
Katiba itamke waz kuwa nichi yetu ni ya ujamaa au ubepari. 2. wananch wamilikishwe ardhi yao. 3. Madaraka ya Rais yapunguzwe mfano asipewe nafas ya kufanya uteuzi katika taasisi kama Takukuru e.t.c. 4. Uhalali wa kumshtaki raisi anapo maliza muda wake wa utawala. 5. Viongozi wasishike nyadhifa zaidi ya moja mfano Ubunge na uwazir kwa pamoja. 6. Uhalali wawananchi kuwatoa kwenye madaraka wabunge wanapoona hawawajibiki. 7. Ububwa wa baraza la mawaziri udhibitiwe.
 
swali ni tutarekebishaje kile cha mwanzo tusichokijua hata ganda lake lina rangi gani tukimbilie kipya ila ni kweli kwamba yale yaliyoorodheshwa pia ni tatizo kunahitajika kutazamwa vizuri
 
Iundwe POLICE COMPLAINT COMMISSION, chombo huru chenye mandate ya kupitia mwenendo wa case yoyote ya Jeshi la Polisi itakayoletwa mbele yake ili kufanikisha dhana ya checks and ballances kwenye chombo hiki muhimu (Polisi) katika kuhakikisha haki za binadamu zinazotarajiwa kuboreshwa ktk katiba mpya.

Tusisaau kuwa kitu kimoja kikubwa kilichotusukuma kudai katiba mpya ni haki za Raia. Chombo hiki kiwajibike kwa Bunge moja kwa moja

Pia niombe wadau wote ktk kutoa maoni yetu tutoe maoni yetu yakiwa na kiini cha kuboresha utu wa mtu mmoja mmoja na utu wa taifa letu ili tupate people centred constitution
 
Back
Top Bottom