onjwayo
JF-Expert Member
- Apr 8, 2020
- 1,346
- 1,303
Pita pita na mikiki mikiki ya Makonda Kila kukicha ni kuivua uchi serikali ya Chama chake. Ni kama huko ndani ya serikali ni uonevu na dharau dhidi ya kada ya chini. Malalamiko ya wananchi ni mengi mnoooooo. Zaidi ni madai ya kudhulumiwa na kunyanyaswa either na vyombo vya Dola au watendaji wenye dhamana ndani ya serikali.
Kuna maeneo wanyonge wamedhulumiwa ardhi, sehemu nyingine wazabuni hawalipwi baada ya kazi walizopewa na halmashauri za Manispaa au wilaya. Kwingine ni vilio juu ya gharama za tiba kwenye baadhi ya Zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya na mkoa ambazo maelekezo yake hutolewa Bure lakini wananzengo wanatozwa fedha. Manung'uniko ni mengi mnoooooo.
Hii yote huonyesha utendaji mbovu kiasi kwamba nchi Sasa inamhitaji one man show kushughulika na kero za wananchi na siyo eti serikali Iko kazini. Pengine tuseme mama Yuko kazini ila anapishana na watendaji wake. Mfano hai ni katibu huyo mwenezi kudiriki kuwahoji baadhi ya mawaziri na wakuu wa mikoa na wanausalama (polisi).
Kama Hali ya wananchi ndiyo hii....malalamiko Kila Kona basi tutegemee Chadema kuzoa wafuasi wengi maana kwenye maandamano Yao wamebeba maudhui ya kero lukuki ambazo wananchi wanapitia. Na Sasa ni dhahiri katiba mpya haikwepeki. Ni mjinga tu anaona aende kwa Makonda kulalamika wakati kama katiba ingeyagusa baadhi ya maeneo Umungu watu ungeisha na watu wangewajibishwa kwa matendo Yao ya kutokujali na ulevi wa madaraka.
Siku moja hiki Chama kitang'ooka na baadhi ya watenda maovu watawajibishwa. Mungu aingilie akili za Watanzania tuweze kujitambua kuwa wanachokitaka kina Lissu siyo tu madaraka Bali ni dira na uelekeo wa kupata haki Kila mahali. Katiba mpya ni Sasa.