Navy S.E.A.Ls (SEa, Air and Land) a.k.a The Frog-men(jina wanalojipa baada ya kuhitimu mafunzo), Tadpoles(jina wanalopewa wale ambao bado wako mafunzoni).
Nay SEALs ni kikosi maalum cha jeshi la majini(Navy) na recruitment ni kipaumbele kwa wanamaji (Navy soldiers) wanaoweza fanya uingiliaji kutoka Baharini(sea), Angani(air) na nchi kavu(land) na ndo jina lao lilipopatikana hapo.
Yasemekana zipo Team 10, ila maarufu zaidi ni SEAL Team 6 (Official name; Navy Special Warfare Development Group (NSWDG), a.k.a DEVGRU), ambayo imegawanyika katika uniti ndogo ziitwazo "Squadron"(mfano; Gold squadron, Red Squadron), ambazo pia zimegawanyika katika uniti ndogo zaidi ziitwazo "Teams"(mfano; Alpha, Bravo, Charlie) ambapo kila team inaweza kuwa na wanakikosi("Operators") kati ya 6 mpaka 10, pamoja na wasaidizi(support structure/personnel) kwa kila "team". Team SIX wanachukua wanavikosi(operators) kutoka Team1, 2, 3, 4, 5, 7, 8, 9 na 10, wanawapeleka mafunzoni tena ndo wanachukuliwa na kupachikwa katika Squadron tofauti tofauti.
Pia Team SIX ipo chini ya United States Special Operations Command (USSOCOM) ambayo inadeal na vikosi vile vilivyonolewa na vikanoleka kweli kweli (mfano SEAL Team 6/DEVDRU, 75th Ranger Regiment, 1st Special Forces Operations Detachment-Delta(1st SFOD-D) a.k.a Delta force etc.)
Navy SEALs wengi wanatoka ndani ya Jeshi la majini(Navy), ni nadra sana kukuta Seal aliyetoka kikosi cha nje ya jeshi la majini.
TV series;
a)SIX
b)SEAL Team
Navy SEALs Motto: The Only Easy Day was Yesterday.
1st Special Forces Operations Detachment-Delta (1st SFOD-D) a.k.a Delta Force/The Unit
Kikosi chenye siri zaidi katika vikosi maalum vya majeshi ya marekani.
Kikosi hiki ndio kina utaratibu wa kuchukua wanavikosi(operators) kutoka katika kikosi chochote kile katika majeshi ya marekani ambaye wanaona anafaa kuungwa na kikosi hicho.
Delta foce ndio kikosi kinasemekana kilichomuua gaidi Osama Bin Laden, kikiwa kimeundwa na wanavikosi kutoka vikosi maalum mbalimbali ndani ya jeshi la marekani kama team 6, marine raiders, 75th ranger regiment etc., wakibebwa katika "helicopter" maalum za kikosi maalum cha misheni maalum cha jeshi la anga kiitwacho "Night Stalkers'.
TV series;
a)The Unit
Movies:
a)Delta force (imechezwa na Chuck Norris)
b)13 Hours; Secret Soldiers of Benghazi (humu wanaonekana karibia n mwisho wa movie wakiwa wawili katika kwenda kusaidia uokoaji na ulizi wa balozi)
1st Special Forces Operations Detachment-Delta Motto (kwa usiri wao motto yao yasemekana kuwa ni) : Silent Professionals