Wanajeshi wa Afghanistan wanaajiriwa na jeshi la Urusi

Mrengwa wa kulia

JF-Expert Member
Mar 21, 2022
991
3,488
Wanajeshi wa kikosi maalum cha Afghanistan ambao walipigana pamoja na wanajeshi wa Marekani na kukimbilia Iran baada ya machafuko ya kujiondoa kwa MarekanI wanaajiriwa na jeshi la Russia kupigana huko Ukraine.

Hayo ni kwa mujibu wa majenerali watatu wa zamani wa Afghanistan waliozungumza na The Associated Press.

Walisema Warussia wanataka kuvutia maelfu ya makomandoo wa hali ya juu wa Afghanistan kwa ahadi za malipo ya dola 1,500 kwa mwezi na mahali pa usalama kwa ajili yao na jamaa zao ili waweze kuepuka kufukuzwa nchini humo kwa kile ambacho wengi wanadhania kingekuwa kifo mikononi mwa Taliban.

Jenerali mmoja alisema: "Hawataki kwenda kupigana lakini hawana namna.

Source: Associated Press, VOA

VIPI kwani wale Angry Mob wameisha mara hii? Au ndo mitego russia walioiweka pale lyman na kharkiv na kherson ndo hawa wanakuja kumaliza kazi?
 
Hao mabwana zenu wana propaganda za kifala sana, hivi si ndo hawa walituambia kuwa Urusi imeajiri maelfu ya wapiganaji kutoka Syria lakini mpaka sasa ni miezi sita hatujawahi kuona mpiganaji yeyote wa Syria nchi Ukraine.
 
Hata akiajiri wanajeshi toka Afghanistan au Libya au Somalia... Tatizo liko wapi?

Yaani wewe unaumia Nini kwa wenzako kuajiriwa na Jeshi la Russia?

Au kama vipi, nenda wewe ukaajiriwe.
 
wamefyekwa tayar utawaonaje? nenda front line bado wanaajiri huko.
 
Hata akiajiri wanajeshi toka Afghanistan au Libya au Somalia... Tatizo liko wapi?

Yaani wewe unaumia Nini kwa wenzako kuajiriwa na Jeshi la Russia?

Au kama vipi, nenda wewe ukaajiriwe.

alie kuambia kuna mtu ameumia nani?
 
Back
Top Bottom