Wanajamvi naomba tujadilini kuhusiana na kasi JPM

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,774
3,460
Wanajamii wenzangu,

Tukaeni kama kikao kwenye uzi huu kuhusiana na kiongozi wetu watananiaz wa awamu ya tano, mwenye ushauri aweke hapa kwa vile raisi wetu amekuja kuwakomboa wananchi wake naamini vigogo wanaojilimbikizia mali za wananchi watakua hawako tayari na hawatopenda kuona raisi huyu na watakua tayari kumshambulia iwe shambulio la moto au baridi, kutokana na utendaje wake mzuri wa kazi.

Ushauri wangu ni kwamba! awe karibu na ulinzi wa JWTZ kwa maana hawa ni tofauti na ulinzi mwengine USALAMA wao wawe na kazi ya kuwachunguza majasusi ambao Magufuli atawatumbua majipu au wewe mwenzangu unashauri vipi?
 
Pia asirudishe mizigo kwny baraza la mawaziri.
Na serikali ihamie rasmi dodoma..
Mahakama ya mafisadi iundwe haraka na pia aendelee na ziara za ambushi maeneo mengine kukamata walanguzi
 
Arudishe serikalini nyumba za umma zilizouzwa..
Zile za masaki ostabei na mikocheni na zingine zote nchini ili mchechu ajenge maghorofa ya umma
 
Vyombo vya ulinzi kama ilivyo mihili ya dola, vina mgawanyo wa majukumu. JWTZ, TIS na Polisi vina mafunzo tofauti kwa kazi tofauti ingawa sometimes hushirikiana lakini majukumu ya msingi yanatofautiana
 
Vyombo vya ulinzi kama ilivyo mihili ya dola, vina mgawanyo wa majukumu. JWTZ, TIS na Polisi vina mafunzo tofauti kwa kazi tofauti ingawa sometimes hushirikiana lakini majukumu ya msingi yanatofautiana

Sijakuelewa mkuu fafanua kidogo.
 
Naomba na iwekwe sheria Kali ya kuwaukumu mafisadi na ifwatwe kama sheria zingine wasiwafumbie macho na kingine mungu amlinde raisi wetu jpm
 
Ulinzi namba moja tuombe kwa MUNGU,wa pili wote tunaokerwa na dhuluma ulinzi wake uwe wajibu wetu sote,na mwisho vyombo vya dola viwape jukumu hilo walio waaminifu. Ugonjwa wa wizi umesambaa mbo kwa watanzania. Tuombe na kutimiza wajibu wetu.
 
ikiwezekana asirudushe waziri yeyote wa awamu ya nne, na matajiri wote wenye mali ambao ni viongozi wachunguzwe na hatua ichukuliwe
 
Pia asirudishe mizigo kwny baraza la mawaziri.
Na serikali ihamie rasmi dodoma..
Mahakama ya mafisadi iundwe haraka na pia aendelee na ziara za ambushi maeneo mengine kukamata walanguzi

Hiyo ya pili mkuu ni kiboko na ndio mambo yatakayoipa tofauti serikali ya JPM na zilizopita.
 
sasa hivi sio muda was kujadili kasi tunataka ukurasa wa katiba unaotaka rais aongoze mihura miwili uondolewe.
 
Ninataka pia waajiri wa nchi hii wachunguzwe maana ni wanyonyaji saana ktk mishahara. Unakuta mtu anafanya kazi kiwanda flani au kwa tajiri flani aisee mshaara anaoupata ni mdogo saana tena anakwenda bila mkataba ilhali tajiri anaingiza faida kubwa. Serikali pia isisahau vilio vya walimu,madaktari,mayaya na watu wengine wa pembezoni. Afute cheo cha mkuu wa wilaya na vyeo vingine visivyo na tija ili mishaara yao iwahudumie wananchi. Ashughulikie swala la wahamiaji haramu wanaotubugudhi sana mfano Wamalawi,Wakenya,Warundi nk. Atatue kero za wananchi kwa nguvu zote kwa kupambana na ujinga,umasikini na maradhi.Ahakikishe katiba ya Warioba tunaipata na pia mikataba ya rasilimali zetu kama madini na watu ipitiwe upya. Awaondoe Wahindi wote kwenye magorofa yetu mijini kwa kuwawekea kodi kubwa maana hawa watu wanalipa kodi ndogo kuliko hata ninayolipa hapa Bunju. Iwe ni sheria kama ni shule ya Wahindi au mgeni yeyote pawe nusu kwa nusu idadi ya wanafunzi weusi na wa Asia maana unaweza kwenda shule flani unakuta ni Wahindi tuu hakuna mswahili hata mmoja. Ashughulikie swala la Zanzibar kwa umakini mkubwa. Ashughulikie masakata yaliyolighalimu taifa hili kama Richmond na Esrow na walo hatia wafungwe na kufilisiwa. Mwisho lakini si kwa umuhimu aishi vizuri na mke wake,ajenge umoja wa kitaifa na kimataifa. Huu ni ushauri kwa Rais wetu kutoka kwangu mimi mwananchi wa kawaida kawaida kabisaa.
 
Kwa ushauri wangu awe mbali na viongozi wenye vichembechembe vya vya TEAM"jk"na temaLOWASSA
 
Wanajamii wenzangu tukaeni kama kikao kwenye uzi huu kuhusiana na kiongozi wetu watz wa awamu ya tano, mwenye ushauri aweke hapa kwa vile raisi wetu amekuja kuwakomboa wananchi wake naamini vigogo wanaojilimbikizia mali za wananchi watakua hawako tayari na hawatopenda kuona raisi huyu na watakua tayari kumshambulia iwe shambulio la moto au baridi, kutokana na utendaje wake mzuri wa kazi. Ushauri wangu ni kwamba! awe karibu na ulinzi wa JWTZ kwa maana hawa ni tofauti na ulinzi mwengine USALAMA wao wawe na kazi ya kuwachunguza majasusi ambao MAGUFULI atawatumbua majipu au wewe mwenzangu unashauri vipi?

kasi unaipimaje?
 
Back
Top Bottom