cyrustheemperor
JF-Expert Member
- Mar 13, 2015
- 293
- 352
Nenda sumbawanga Kuna "Alot of fortunes out there"Mimi nikijana mwenye umri wa 25yrs, nimemaliza chuo mwaka jana na degree ya sheria kutoka chuo kikuu kimoja huko Arusha, Tangia nimalize chuo niliamua kuhamia dar na kujichanganya kwa vibiashara vya hapa na pale kama mnavyojua tatizo la ajira kwasasa, kweli nimejaribu sana kuuza hiki na kile km viatu, nguo, vyakula, ila kila ninachofanya nafeli mahitaji yanazidi kipato, mpaka muda huu ninavyo andika hapa ht ule mtaji kidogo nao nimelipa kodi,
Nimeuza karibia assets zote nilizonunua kipindi nipo chuo, nimebaki na kitanda na godoro tu na jiko navyo km maisha yataendelea kuwa hivi nitauza navo nirudi nyumbani tu, Sioni thamani yakusoma kabisa, najuta muda niliopoteza nisingeishi maisha mabaya km haya, Naomba mwenye connections ya kazi zifuatazo anisaidie japo nijiokoe nisiuze kitanda na godoro.
Utaniboy, Saidia fundi, kubeba zege, Viwandani, pia hata udereva naweza ingawa sina leseni ila naweza uza simu nikaipata, nisaidieni ndugu zangu, Vyeti vyote na ushahidi ninavyo. Nawashukuru sana mungu awabariki ndugu zangu.