WanaJamiiForums nakuja kwenu kukiri maisha ni magumu, naomba mnisaidie nipate kazi

GersonTz

Member
Jan 6, 2020
51
62
Mimi nikijana mwenye umri wa miaka 25,

Nimemaliza chuo mwaka jana na degree ya sheria kutoka Chuo Kikuu kimoja huko Arusha, lakini tangu nimalize chuo niliamua kuhamia Dar es Salaam na kujichanganya kwa vibiashara vya hapa na pale kama mnavyojua tatizo la ajira kwa sasa, kweli nimejaribu sana kuuza hiki na kile kama viatu, nguo, vyakula, ila kila ninachofanya kinafeli mahitaji yanazidi kipato, mpaka muda huu ninavyo andika hapa hata ule mtaji kidogo nao nimelipa kodi.

Nimeuza karibia assets zote nilizonunua kipindi nipo chuo, nimebaki na kitanda na godoro tu na jiko navyo kama maisha yataendelea kuwa hivi nitauza navo nirudi nyumbani tu

Sioni thamani yakusoma kabisa, najuta muda niliopoteza nisingeishi maisha mabaya kama haya, naomba mwenye connections ya kazi zifuatazo anisaidie japo nijiokoe nisiuze kitanda na godoro.
  1. Usaidizi wa kwenye magari ya mzigo,
  2. Saidia fundi, kubeba zege,
  3. Viwandani,
  4. Pia hata udereva naweza ingawa sina leseni ila naweza uza simu nikaipata, nisaidieni ndugu zangu
Vyeti vyote na ushahidi ninavyo.

Nawashukuru sana mungu awabariki ndugu zangu.
 
Mimi nikijana mwenye umri wa 25yrs, nimemaliza chuo mwaka jana na degree ya sheria kutoka chuo kikuu kimoja huko Arusha, Tangia nimalize chuo niliamua kuhamia dar na kujichanganya kwa vibiashara vya hapa na pale kama mnavyojua tatizo la ajira kwasasa, kweli nimejaribu sana kuuza hiki na kile km viatu, nguo, vyakula, ila kila ninachofanya nafeli mahitaji yanazidi kipato, mpaka muda huu ninavyo andika hapa ht ule mtaji kidogo nao nimelipa kodi,

Nimeuza karibia assets zote nilizonunua kipindi nipo chuo, nimebaki na kitanda na godoro tu na jiko navyo km maisha yataendelea kuwa hivi nitauza navo nirudi nyumbani tu, Sioni thamani yakusoma kabisa, najuta muda niliopoteza nisingeishi maisha mabaya km haya, Naomba mwenye connections ya kazi zifuatazo anisaidie japo nijiokoe nisiuze kitanda na godoro.

Utaniboy, Saidia fundi, kubeba zege, Viwandani, pia hata udereva naweza ingawa sina leseni ila naweza uza simu nikaipata, nisaidieni ndugu zangu, Vyeti vyote na ushahidi ninavyo. Nawashukuru sana mungu awabariki ndugu zangu.
Pole Mkuu.

Hebu jaribu kupita hapo.

Graduate ninayefanya kazi ya Ulinzi, niulize chochote kuhusu sekta hii
 
Asa hapa ndo umemshauri nini..ukiacha roho ya kwanini utafika mbali
Ulitaka nimshauri nini labda maana mi nimemtia moyo aondokane na roho ya kukata tamaa ambayo ni failure number one ambayo hupelekea watu kujiua au wewe ulitaka nimuunganishe na Don Laizer ili washiriki pamoja kwenye kutoa jiwe moja moja chumbani mwake na kujiita mwenye bahati sio?
 
mm nasemaga siku zote, Kazi za ufundi ni nzuri jamani. Jifunzeni ufundi jamani
Uko sahihi. Nimepeleka mtoto shule fulani. Wanafunzi wote wanatakiwa waondoke angalau na ufundi stadi wa aina fulani. Ukizembea unakamatwa hata ukipata A zote masomo ya darasani. Huyu wa kwangu kaamua kujifunza kuwa dentist assistant na tayari anakwenda kufanya interns huko kwenye maofisi ya madentist na wengine wanamlipa. Jirani yangu hapa mtoto wake amejifunza ufundi magari. Wamefundishwa oil change, brake system na matatizo mengine ya juu juu. Ameongezea na welding. Wengine wanajifunza ufundi umeme. Vyote mkazo ni practicals. Nimependa sana utaratibu huu. Wakati wa kukaririshana nadharia peke yake umepitwa na wakati...
 
umeamua vyema sana
 
Elimu ya bongo ni kukremu tu hakuna kitu...na shida ndo inapoanzia hapo

Graduates wanapata tabu sana aisee
 
Back
Top Bottom