WanaJamiiForums nakuja kwenu kukiri maisha ni magumu, naomba mnisaidie nipate kazi

elim ya bongo kama huna konekisheni ni ushubwada mtupu, kuna jamaa yangu ana degree ya sheria kama wewe bt anacheza kamari tu kitaa
 
Ulikosea kufikiri tangu mwanzo. Ungefikiri kuishi maisha yaliyosawia na kipato chako ungesogea mbele zaid. Dar imekuponza. Pambana au hama
 
Uko sahihi. Nimepeleka mtoto shule fulani. Wanafunzi wote wanatakiwa waondoke angalau na ufundi stadi wa aina fulani. Ukizembea unakamatwa hata ukipata A zote masomo ya darasani. Huyu wa kwangu kaamua kujifunza kuwa dentist assistant na tayari anakwenda kufanya interns huko kwenye maofisi ya madentist na wengine wanamlipa. Jirani yangu hapa mtoto wake amejifunza ufundi magari. Wamefundishwa oil change, brake system na matatizo mengine ya juu juu. Ameongezea na welding. Wengine wanajifunza ufundi umeme. Vyote mkazo ni practicals. Nimependa sana utaratibu huu. Wakati wa kukaririshana nadharia peke yake umepitwa na wakati...

hii ni hapahapa Tanzania?
 
mwanao akiwa anasoma sekondari, jitahidi ajifunze kimoja katika hivi kwenye muda wa ziada.

1. Motorvehicle mechanics.
2. Welding and fabrication.
3. fitter and turner.
4. jitahidi awe na leseni ya udereva na cheti cha
NIT.
5. Computer and cell technician.
6. Constr and mining equipment operator.

Pia huko shule ajifunze kuongea kiingereza kifupi kuwasiliana kwa kikristo, msidanganywe na wanasiasa muandae watoto kadili inavyofaa..
Mwanao akimaster kimoja kwenye hivyo hata amalize chuo kikuu atajua namna ya kuishi huku anaangalia mambo mengine..
 
Pole sana najiona mimi anyway kaza kwa sababu hata mimi nilipitia hayo ila leo nilipo ni patamu ila siwezi kupasema ila nakula maisha hata mida hii ya Corona
badala ya kutoa msaada unabaki kujisifia, pumbavu sana
 
Hiv
mwanao akiwa anasoma sekondari, jitahidi ajifunze kimoja katika hivi kwenye muda wa ziada.

1. Motorvehicle mechanics.
2. Welding and fabrication.
3. fitter and turner.
4. jitahidi awe na leseni ya udereva na cheti cha
NIT.
5. Computer and cell technician.
6. Constr and mining equipment operator.

Pia huko shule ajifunze kuongea kiingereza kifupi kuwasiliana kwa kikristo, msidanganywe na wanasiasa muandae watoto kadili inavyofaa..
Mwanao akimaster kimoja kwenye hivyo hata amalize chuo kikuu atajua namna ya kuishi huku anaangalia mambo mengine..
hivyo vyote ni mlengwa uleule wa kuomba ajira au kujiajiri locally...nafiri kumuwekea akiba mtoto ndio akiri skills zingine atajifuanza mwenyewe ila huku akiwa na pesa ya kujifunza bila stress na kugharamia kila kinachotakiwa.

Imagine mtoto umemuandaa kwa skills za graphicsdesign, Online business nk huku akimaliza chuo anapesa yake kwa account hata 7M.
 
Pole sana najiona mimi anyway kaza kwa sababu hata mimi nilipitia hayo ila leo nilipo ni patamu ila siwezi kupasema ila nakula maisha hata mida hii ya Corona
Hua napenda kusikia shuhuda Kama hizi.zinatia Sana moyo...hongera mkuu
 
Mkuu usirudi home pambana hapa mjini vibarua vinapatikana ukizunguka mitaani

marufuku kukata tamaa
 
Back
Top Bottom