Wanahitajika vijana 20 wenye ujuzi wa Microsoft Powerpoint & Word

MOSintel Inc

JF-Expert Member
Mar 24, 2016
812
585
👥 WANAHITAJIKA VIJANA 20

1. Wenye stadi, uzoefu na ujuzi katika kutumia "MICROSOFT POWERPOINT" na "MICROSOFT WORD"

2. Wenye muda wa ziada wa masaa matatu(3) hadi manne(4) kwa siku.

3. Wenye kazi kuanzia 2 hadi 4 za "Microsoft PowerPoint Presentation" walizowahi kufanya hapo awali.

4. Wenye uwezo wa kufanya kazi wakiwa katika makazi/ofisi zao na kuwasiliana kwa kutumia njia ya mtandao.

5. Wenye uelewa au uelewa kiasi wa majukwaa mbalimbali ya kazi za mtandaoni.

6. Pia wenye uwezo maridadi wa kuwasiliana kwa njia ya lugha ya Kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha.

Ikiwa vigezo hivyo unavyo au Kuna mtu unayefahamiana naye ana vigezo tajwa hapo juu usisite kuwasiliana nasi uki/aki-ambatanisha kazi zako/zake mbili (2) za "Microsoft PowerPoint Presentation" kupitia Barua pepe .

KWA MAWASILIANO:

Barua pepe(Email) :
milenniostudio@outlook.com

Simu(Kupiga):
+255-787-454-580

WhatsApp:

----KARIBUNI SANA----
 
Halafu hii Tabia Ife yaani wewe unaweka vigezo vya ujuzi unaotafuta Ila unaogopa kuweka ulicho nacho kwa huo ujuzi. Weka salary mbona wenzetu hii ishu sio Siri hakuna kurogana. Weka na wewe ujielezee Kama unavyoelezea ujuzi unaoutaka.

Mtu anahangaika baadaye anakuja kugundua anachopewa hakimstahili.

Yaani anahangaika,anapoteza mental energy kuwaza, financial resources, anasitisha Mambo mengine, anapoteza time resources.

Please naombeni waajiri tubadilike tuthamini our fellow human beings resources
 
Wanatakiwa kufanya kazi gani, wanafanya kazi na taasisi au mtu binafsi, taasisi/mtu huyo yuko mkoa/ nchi gani? Na je ni lazima wao wawepo eneo hilo kwa maana ya mkoa huo ili waweze kuifanya hyo kazi? Offer ulionayo ni sh ngapi kwa hao vijana?

Mnawatesa madogo wanaotafuta kazi. Kwani kuweka hizo hints wazi kuna tatizo gani?
 
Alafu watu wanaokuja na maneno meengiii na vigezo kibao utadhani wanakata tiketi ya kwenda mbinguni hawanaga kitu! Ni malofa na wababaishaji! Sasa PowerPoint ndo kitu gani kuhitaji mtu mwenye ujuzi! Mtu yeyote layman akielekezwa anafanya! Hii nchi ngumu sana!
 
I hope hakutakuwa na zile kauli za 'umechaguliwa hii kazi sasa tuma 83,750/= ya registration au umebahatika kupata hii kazi unatakiwa kutuma 57,325/= ya kuwezeshwa uwe activated au nimepitia hizi kazi zako 2 za power point uko vizuri sana sasa tafuta 50,000/= tumpe jamaa anae select watu'
 
Back
Top Bottom