Wanaharakati walalamikia vurugu za mchina Songea

Wanaharakati walalamikia vurugu za mchina Songea

Mnalalamika kila kitu, muda wote.Wakati mikono na miguu mnazo!! Ina maana hapo standi vijana wote mchina mmoja tu anawapiga wote? Kila kitu POLISI POLISI POLISI POLISI. Nyie hamuwezi hata kesho kuanzisha vurugu na kumhamisha hapa Tz? Wanaume mmekuwa kama wanawake!!! Ndio maana vitu vingine JK anajinyamazia tu!!

Hata mie nashangaa kawatembezea kichapo masaa sita, hii noma. huyu atakuwa na vinasaba vya bruce lee. katika biashara gorrilla strategy mara nyingi huwa haifanikiwi. Police na sumatra tumieni busara waiteni hawa watu muwasuluhishe kabla hawajaanza kupigana pasi barabarani.
 
huyo feo ametunyanyasa sana abiria. wacha wanaojua costumer care watupe huduma. sipandi tena super feo ng'oo
 
Kwa heri super feo kazoeshwa kuamini kuwa yeye hana mpinzani kwa dar-songea, kupewa sifa za kijinga na wapiga debe, kutumia mamlaka za umma vibaya (polis, sumatra) badala ya kuwekeza kwenye customer care. Please omar ninakufaham wewe ni mtu fresh sana lkn hao mameneja wako wana jeuri, unyanyasaji na ndio waliokufikisha kulalamika hapa JF. Chukua hatua fanya SWOT analysis uweke strategy za kuhimili competition sio kulia lia humu naamini unaweza
 
Mtoa taarifa ni mwehu. Unafikiri sisi abiria wa Songea tuna maindi uzawa? Huduma mbovu kabisa za Superfeo halafu unataka tuendekeze ujinga? Mimi ni mmoja wa waliokataa kupanda Superfeo. Siangalii uzawa. Naangalia huduma. Lugha chafu kabisa mnanzo Superfeo. Na wewe Stephano na ulemavu wako wa mwili na akili basi uandishi wenu ni njaa tu. Hapa Songea mnachukua hela za Superfeo ili kumpamba kwa ujinga. New Force ndio suluhisho la usafiri kwa sasa mkoa wa Ruvuma. Nyie mnalinga kisa Uzawa? Acheni ujinga wenu. Tunajua sana kama Superfeo katoa hela kuwahonga SUmatra na Polisi ili kumkandamiza New Force. Bado hata New Force akitoka saa 12.30 anawakuta Iringa tu pale. Hili nimelishuhudia mara kibao. Tunakuwa wa mwisho kutoka lakini Dar tunakuwa wa kwanza kuingia. Mmechoka. Mwambie bosi wenu awalipe tena kuandika haya uliyoandika. Wewe na Francis Sengo ndio mnajidai maafisa habari wa superfeo. Hapa Songea kwa mwenye akili timamu lazima apande New Force. Gari zuri, huduma nzuri, lugha nzuri hata ukichelewa hasa siku hizi za masika bado ata consider tiketi yako. Lakini nyie mtu akichelewa hata kwa tatizo la mvua inakula kwake. Huu ni uungwana? Acheni ujuha kabisa. Naendelea kuhamasisha wengine wapande New Force. Nyie mmechoka na mnalinga. Mjifunze
 
Mtoa taarifa ni mwehu. Unafikiri sisi abiria wa Songea tuna maindi uzawa? Huduma mbovu kabisa za Superfeo halafu unataka tuendekeze ujinga? Mimi ni mmoja wa waliokataa kupanda Superfeo. Siangalii uzawa. Naangalia huduma. Lugha chafu kabisa mnanzo Superfeo. Na wewe Stephano na ulemavu wako wa mwili na akili basi uandishi wenu ni njaa tu. Hapa Songea mnachukua hela za Superfeo ili kumpamba kwa ujinga. New Force ndio suluhisho la usafiri kwa sasa mkoa wa Ruvuma. Nyie mnalinga kisa Uzawa? Acheni ujinga wenu. Tunajua sana kama Superfeo katoa hela kuwahonga SUmatra na Polisi ili kumkandamiza New Force. Bado hata New Force akitoka saa 12.30 anawakuta Iringa tu pale. Hili nimelishuhudia mara kibao. Tunakuwa wa mwisho kutoka lakini Dar tunakuwa wa kwanza kuingia. Mmechoka. Mwambie bosi wenu awalipe tena kuandika haya uliyoandika. Wewe na Francis Sengo ndio mnajidai maafisa habari wa superfeo. Hapa Songea kwa mwenye akili timamu lazima apande New Force. Gari zuri, huduma nzuri, lugha nzuri hata ukichelewa hasa siku hizi za masika bado ata consider tiketi yako. Lakini nyie mtu akichelewa hata kwa tatizo la mvua inakula kwake. Huu ni uungwana? Acheni ujuha kabisa. Naendelea kuhamasisha wengine wapande New Force. Nyie mmechoka na mnalinga. Mjifunze

Kweli mkuu
 
NA, STEPHANO MANGO,SONGEA

WANAHARAKATI wamelalamikia Kitendo cha Raia wa Nchi ya China Zhouguang Zheng (27)maarufu kwa jina la Dani Johnson Kumpiga na Kumsababishia Maumivu Makali Mfanyabiashara Maarufu Na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Kisiwa Sport, Kisiwa Kisiwa (40) na kumsababishia Kulazwa Siku Mbili katika Hospital ya Serikali ya Mkoa wa Songea na Wengine wawili walijeruhiwa katika Vurugu hizo

Wakizungumza kwa Nyakati Tofauti na Gazeti Hili jana Walisema kuwa Kitendo hicho ni kibaya sana kwani kimekiuka Sheria za Uraia na Uwekezaji, ingawa pia ni ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu na kinavuruga amani na Utulivu Miongoni Mwa Jamii

Hamis Abdala Ally alisema kuwa kitendo cha Mwekezaji huyo wa Kampuni ya Mabasi ya NewForce inayosafirisha Abiria kutoka Songea Kuelekea Jijini Dar Es Salaam kimevuka mipaka yake ya Uwekezaji na Ukiukwaji mkubwa wa Sheria na Taratibu

Ally Alisema kuwa ni kosa sana Raia wa Kigeni kwenye Nchi ya Watu kufanya Vurugu na Kusababisha Raia wa Nchi Husika kupata Maumivu Makali katika Mwili wake , kwani kitendo hicho kinaweza Kusababisha chuki na amani kuvurugika miongoni mwa Jamii
Alisema kuwa Tukio hilo linahatarisha uwekezaji wake, ushirikiano uliojengeka kwa kipindi kirefu kwenye jamii husika kwani mahusiano ya Watu yamepungua kutokana na Jambo hilo

“Tunalitaka Jeshi la Polisi Kutenda Haki Katika Jambo Hili la Mchina Kufanya Vurugu na Kusababisha amani kutoweka Katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi Songea kwa Zaidi ya Masaa sita na kuongezeka kwa Chuki Miongoni mwa jamii ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mabasi ya Super Feo na NewForce”Alisema Ally
Alieleza kuwa Wananchi wa Songea hatuna utaratibu wa kuwadhuru au kuwanyanyasa Raia wa Kigeni wawapo kwenye Shughuli zao lakini Tumeshangazwa na Mchina Huyu ambaye ameanzisha Utamaduni Mpya wa Kuwajeruhi Wazawa

Mukhtar Simba Alisema kuwa Wanaruvuma ni watu Waungwana na Wakarimu sana na kwenye Swala la Uwekezaji Kuna Sheria na Taratibu ambazo zinamuongoza Mwekezaji kufanya shughuli zake pia ana mipaka ya uwekezaji wake katika eneo husika

Simba Alisema Tunalaani na kushangaa Kumuona Mwekezaji Huyo bado anaendelea Kutamba Mitaani huku Mwenzake akiendelea na Matibabu ambayo yamesababishwa na Kipigo chake wakati sheria zipo wazi

Akizungumzia Tukio Hilo Mkurugenzi wa Kampuni ya Super Feo Omari Msigwa Alisema kuwa Kitendo alichokifanya Mchina Siku hiyo Cha Kumpiga Msaidizi wake Haruna Msigwa na Kisiwa Kisiwa na Kuifanya Stendi kuwa ni Uwanja wa Vurugu kimemshtua Sana kwani Hakukitegemea katika Sekta ya Usafirishaji Mkoani Ruvuma

Msigwa Alisema kuwa licha ya Jambo hilo kuwa ni Ukiukwaji Mkubwa wa Haki za Binadamu na Sheria za Nchi Lakini pia kimeleta picha mbaya sana Katika Sekta ya Usafirishaji kiujumla kwani Vurugu hizo zimetokea Mbele ya Abiria ambao hawajawahi kuona wala kutarajia vurugu katika Stendi hiyo

Alieleza kuwa Sheria ziko wazi za Uwekezaji na za Kijinai hivyo ni Muhimu Mamlaka zinazohusika kuchukua Hatua Stahiki Katika Jambo hilo kwani kutochukua hatua madhubuti kutasababisha ulipizaji wa Kisasi miongoni mwa Jamii hizo

“Ili Kuepuka chuki hizo ni Vyema Mamlaka zinazohusika Zikatenda Haki kwa Kila Mmoja aliyeenda Kinyume cha Sheria na Taratibu katika Tukio hilo Kwani Kitendo cha Kumpendelea Mtu huku Ukweli wa Jambo ukiwa wazi kitaanzisha utamaduni mbaya ambao utaleta athari nyingi baadaye” Alisema Msigwa

Alieleza zaidi kuwa Siku za Nyuma Kulikuwa na Kampuni Nyingi za Usafirishaji Abiria kama Vile Sabco, Saibaba,Scandnavia,Ottawa, na Nyinginezo lakini hakuna Siku Hata Moja Wafanyakazi wake au Wafanyakazi wa Kampuni nyingine hizo Kupigana lakini leo Mwekezaji wa Kigeni Amempiga Mwekezaji wa Ndani hali ambayo inazua Mashaka sana

Akizungumza na Gazeti hili Nyumbani Kwake Kisiwa Kisiwa alisema kuwa Ni ukweli ulio wazi kuwa nimepigwa tena kipigo Kikali na Mchina hadi kulazwa Siku Mbili kutokana na Maumivu Makali Katika Sehemu mbalimbali za Mwili wangu

Kisiwa Alisema licha ya Kushonwa Nyuzi kumi na nne Mdomoni kutokana na Kipigo bado mwili wangu haujatengamaa na maumivu makali bado nayasikia na sijaanza kufanya kazi zangu za kila siku kama ilivyo ada

Alisema kuwa Mchina huyu amekosa Utu wala aibu Toka anisababishie Maumivu katika Mwili wangu ameshindwa hata kunijulia hali bali yeye amekuwa akiendelea na shughuli zake huku mie nikiendelea kuumwa

Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema Tukio hilo lilitokea Januari 13 Majira ya Saa 12:10 asubuhi katika eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi Kilichopo Msamala Mjini hapa , ambako ilizuka Vurugu kubwa baina ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mabasi ya Usafirishaji Abiria ya New Force na Kampuni ya Super Feo wakigombaniana ratiba ya kuondoa Mabasi yao kutoka Songea Kuelekea Jijini Dar Es Salaam

Msikhela Alisema kuwa Katika tukio hilo Watu watatu wamejeruhiwa ambao ni Zhouguang Zheng (27) ambaye ni Raia wa China, Danford Thomas (40) Mkazi wa Mfaranyaki na Abdurabi Kisiwa ambaye pia ni Mkazi wa Mfaranyaki na Mmiliki wa Mabasi ya Kisiwa Sports

Alieleza zaidi kuwa inadaiwa katika vurugu hizo vitu mbalimbali vimepotea zikiwemo Simu mbili aina ya Tecno ambazo thamani yake bado haijafahamika ambazo zilikuwa mali ya Kisiwa, simu moja ya IPhone 5s yenye thamani ya milioni 1.5 pamoja na fedha taslim shilingi milioni nne zimeporwa na watu wasiofahamika ambazo ni mali ya Zhouguang Zheng

Alisema kuwa kufuatia tukio hilo watu 14 wamekamatwa na Kuhojiwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha katika vurugu hizo na wapo nje kwa dhamana na kwamba Jarada la Uchunguzi Limefunguliwa na Kupewa namba SO/IR/ 189/015 Na kwamba upelelezi bado unaendelea kufanywa na kwamba ukikamilika Jarada hilo litapelekwa Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali ili kulifanyia kazi kabla halijaenda Mahakamani
MWISHO


Shida ya watoa habari wengi wa hapa Bongo ni kutokujua namna ya kubalansi taarifa zenu. Bw Mango ulishindwa nini kwenda kumhoji na mchina badala yake umeenda kwa Kisiwa na kwa RPC huoni kama taarifa yako haijakamilika, au ndo yale yale ya bahasha? Halafu basi walau taarifa yako ingebainisha wazi nini sababu thabiti ya huyo Mchina kumtwanga mzawa mwenzetu naona na hili hakuna aliyeliezea waziwazi. Kuna ishu hapo imedokezwa kidogo kwamba Mchina alinyimwa kuondoka pamoja na Superfeo hata baada ya kuulipia huo muda, huoni kama hilo ni kweli kuna uonevu pia kwa hawa wawekezeji wa kigeni? Lakini changamoto nyingine ambayo binafsi naiona kwa upande wa polisi na SUMATRA hivi ni kwa nini msgari ya route ndefu yasiondoke pamoja yaelekeapo DSM kama ilivyo kwa UBT? Ni busara sana tena ni haki mabasi yote ya safari ndefu yaanze safari pamoja kwani mabasi karibuni yote huwa yako level seat na hivyo kutosimama simama njiani kwa ajili ya aidha kuchukua au kushusha abiria mpaka wanapikaribia kufika DSM. HUONI KAMA KUNA HUJUMA HAPO WANAFANYIWA HAO WASAFIRISHAJI WAGENI WA KUTOKA NJE YA SONGEA?
 
Madhara ya kubambikia wafanyakazi wake kesi Polisi! Leo kimemrudia!
Hivi Yule dogo aliomrundikaga Polisi na kumsingizia aliiba pesa za mkewe iliisha?
 
nyie superfeo wahuni kweli mnaweka pesa mbele kuliko utu

nakumbuka mwaka jana nilikua natoka songea kuja dar nilikata basi no 1 na nilikua napandia kituo cha njiani, sasa ile nafika tu kituoni basi nalo ndo linaondoka kwakua nilikua na begi la nguo wakasema hawawezi fungua buti nipande gari la pili

gari la 2 lilivyo kuja wao wakasema hawana seat hivyo nipande mpaka mizani na waombe gari la 3 walipo fika wakanichukua ila walikua wanalalamika kweli maana lenyewe ndolilikua na mizigo mingi kuliko hayo mengine na tulipo fika mizani tena tulizidi ikabidi wampigie simu yule wa no moja nilipo takiwa

tulipo fika aljazilah tukakutana nakutakiwa kwenda kwenye basi hilo nililo takiwa niwepo ambalo no 1 na kukuta seat yangu wamesha uza ili bidi wanitafutie seat nyingine. Yaani tangu siku ile walivyo nipiga danadana siwapandi tena hawa superfeo
 
I can't imagine mchina alivokua anatembeza kichapo..snake in the monkey shadow..duuh..!!nakumbuka alishawatembezea wamasai zaid ya watatu ambao walikua na kibur wanalisha ng'ombe kweny shamba la mchina jamaa alikua anashusha tsunami ya kung fu huku ana bounce kwenye migongo ya ng'ombe..!! fikiria panic ya wamasai alafu kichapo walichoangushia polisi mchina alikataa kuwaita kwani shughuli anaiweza..akaswaga na ng'ombe kwake walimlipa ng'ombe zaid ya saba...
 
kwakweli kama kuna sehemu ina manyanyaso kwa gharama ya hela yako ni usafiri mikoani,,,

hawa jamaa huwa wanajiona ni miungu watu,,,
 
mm n mkaz Wa songea na Mara nyng huwa na safar za Dar.sijui Sana kuhusu ugomv Wa new force na super feo but nlichokishuhudia asubuh moja ni kuwa super feo wanatumia ubabe Wa uzawa na kumnyima new force nafac za kufanya biashara.
kwa mfano super feo anataka gar zake zote ztoke sa 12 kamili Zen new force atoke nusu saa baadae.kumbuka Dar n mbali na abiria akichelew kufka kesho hapand tena new force.
cha kushangaza mpaka uongoz mkubwa Wa polic mkoa nliwaona sikuile stand wakihakksha new force hatoki.nkajiuliza mbona nkitoka Dar wote tunatoka kawaida tu.
nkajiuliza Kama kunasheria kwann zctende haki.kwamba superfeo atoe bac yake kwanza na new force atoe,la pili hvyovlhvyo na la Tatu pia ila sio super feo zote tatu kwanza then new force afuate.
pia mleta mada amejikita kwenye kumshutum mchna bla kueleza sababu ya ugomv .this show jamaa n mtu Wa superfeo.so kojoa kalale usilete unafki humu!!
ofcoz nmechangia tu but sihusk na yeyote Kati yao,bye!!

Nahisi umetumwa, na mtoto wa Mjomba wewe maana anahisa kwenye new force!
 
Mbona huelezi mini chanzo mpaka kufikia hatua mchina akawanyuka? Mi naona hapa unalalama tu
 
Back
Top Bottom