Stephano Mango
Member
- Mar 23, 2012
- 64
- 13
NA, STEPHANO MANGO,SONGEA
WANAHARAKATI wamelalamikia Kitendo cha Raia wa Nchi ya China Zhouguang Zheng (27)maarufu kwa jina la Dani Johnson Kumpiga na Kumsababishia Maumivu Makali Mfanyabiashara Maarufu Na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Kisiwa Sport, Kisiwa Kisiwa (40) na kumsababishia Kulazwa Siku Mbili katika Hospital ya Serikali ya Mkoa wa Songea na Wengine wawili walijeruhiwa katika Vurugu hizo
Wakizungumza kwa Nyakati Tofauti na Gazeti Hili jana Walisema kuwa Kitendo hicho ni kibaya sana kwani kimekiuka Sheria za Uraia na Uwekezaji, ingawa pia ni ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu na kinavuruga amani na Utulivu Miongoni Mwa Jamii
Hamis Abdala Ally alisema kuwa kitendo cha Mwekezaji huyo wa Kampuni ya Mabasi ya NewForce inayosafirisha Abiria kutoka Songea Kuelekea Jijini Dar Es Salaam kimevuka mipaka yake ya Uwekezaji na Ukiukwaji mkubwa wa Sheria na Taratibu
Ally Alisema kuwa ni kosa sana Raia wa Kigeni kwenye Nchi ya Watu kufanya Vurugu na Kusababisha Raia wa Nchi Husika kupata Maumivu Makali katika Mwili wake , kwani kitendo hicho kinaweza Kusababisha chuki na amani kuvurugika miongoni mwa Jamii
Alisema kuwa Tukio hilo linahatarisha uwekezaji wake, ushirikiano uliojengeka kwa kipindi kirefu kwenye jamii husika kwani mahusiano ya Watu yamepungua kutokana na Jambo hilo
Tunalitaka Jeshi la Polisi Kutenda Haki Katika Jambo Hili la Mchina Kufanya Vurugu na Kusababisha amani kutoweka Katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi Songea kwa Zaidi ya Masaa sita na kuongezeka kwa Chuki Miongoni mwa jamii ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mabasi ya Super Feo na NewForceAlisema Ally
Alieleza kuwa Wananchi wa Songea hatuna utaratibu wa kuwadhuru au kuwanyanyasa Raia wa Kigeni wawapo kwenye Shughuli zao lakini Tumeshangazwa na Mchina Huyu ambaye ameanzisha Utamaduni Mpya wa Kuwajeruhi Wazawa
Mukhtar Simba Alisema kuwa Wanaruvuma ni watu Waungwana na Wakarimu sana na kwenye Swala la Uwekezaji Kuna Sheria na Taratibu ambazo zinamuongoza Mwekezaji kufanya shughuli zake pia ana mipaka ya uwekezaji wake katika eneo husika
Simba Alisema Tunalaani na kushangaa Kumuona Mwekezaji Huyo bado anaendelea Kutamba Mitaani huku Mwenzake akiendelea na Matibabu ambayo yamesababishwa na Kipigo chake wakati sheria zipo wazi
Akizungumzia Tukio Hilo Mkurugenzi wa Kampuni ya Super Feo Omari Msigwa Alisema kuwa Kitendo alichokifanya Mchina Siku hiyo Cha Kumpiga Msaidizi wake Haruna Msigwa na Kisiwa Kisiwa na Kuifanya Stendi kuwa ni Uwanja wa Vurugu kimemshtua Sana kwani Hakukitegemea katika Sekta ya Usafirishaji Mkoani Ruvuma
Msigwa Alisema kuwa licha ya Jambo hilo kuwa ni Ukiukwaji Mkubwa wa Haki za Binadamu na Sheria za Nchi Lakini pia kimeleta picha mbaya sana Katika Sekta ya Usafirishaji kiujumla kwani Vurugu hizo zimetokea Mbele ya Abiria ambao hawajawahi kuona wala kutarajia vurugu katika Stendi hiyo
Alieleza kuwa Sheria ziko wazi za Uwekezaji na za Kijinai hivyo ni Muhimu Mamlaka zinazohusika kuchukua Hatua Stahiki Katika Jambo hilo kwani kutochukua hatua madhubuti kutasababisha ulipizaji wa Kisasi miongoni mwa Jamii hizo
Ili Kuepuka chuki hizo ni Vyema Mamlaka zinazohusika Zikatenda Haki kwa Kila Mmoja aliyeenda Kinyume cha Sheria na Taratibu katika Tukio hilo Kwani Kitendo cha Kumpendelea Mtu huku Ukweli wa Jambo ukiwa wazi kitaanzisha utamaduni mbaya ambao utaleta athari nyingi baadaye Alisema Msigwa
Alieleza zaidi kuwa Siku za Nyuma Kulikuwa na Kampuni Nyingi za Usafirishaji Abiria kama Vile Sabco, Saibaba,Scandnavia,Ottawa, na Nyinginezo lakini hakuna Siku Hata Moja Wafanyakazi wake au Wafanyakazi wa Kampuni nyingine hizo Kupigana lakini leo Mwekezaji wa Kigeni Amempiga Mwekezaji wa Ndani hali ambayo inazua Mashaka sana
Akizungumza na Gazeti hili Nyumbani Kwake Kisiwa Kisiwa alisema kuwa Ni ukweli ulio wazi kuwa nimepigwa tena kipigo Kikali na Mchina hadi kulazwa Siku Mbili kutokana na Maumivu Makali Katika Sehemu mbalimbali za Mwili wangu
Kisiwa Alisema licha ya Kushonwa Nyuzi kumi na nne Mdomoni kutokana na Kipigo bado mwili wangu haujatengamaa na maumivu makali bado nayasikia na sijaanza kufanya kazi zangu za kila siku kama ilivyo ada
Alisema kuwa Mchina huyu amekosa Utu wala aibu Toka anisababishie Maumivu katika Mwili wangu ameshindwa hata kunijulia hali bali yeye amekuwa akiendelea na shughuli zake huku mie nikiendelea kuumwa
Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema Tukio hilo lilitokea Januari 13 Majira ya Saa 12:10 asubuhi katika eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi Kilichopo Msamala Mjini hapa , ambako ilizuka Vurugu kubwa baina ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mabasi ya Usafirishaji Abiria ya New Force na Kampuni ya Super Feo wakigombaniana ratiba ya kuondoa Mabasi yao kutoka Songea Kuelekea Jijini Dar Es Salaam
Msikhela Alisema kuwa Katika tukio hilo Watu watatu wamejeruhiwa ambao ni Zhouguang Zheng (27) ambaye ni Raia wa China, Danford Thomas (40) Mkazi wa Mfaranyaki na Abdurabi Kisiwa ambaye pia ni Mkazi wa Mfaranyaki na Mmiliki wa Mabasi ya Kisiwa Sports
Alieleza zaidi kuwa inadaiwa katika vurugu hizo vitu mbalimbali vimepotea zikiwemo Simu mbili aina ya Tecno ambazo thamani yake bado haijafahamika ambazo zilikuwa mali ya Kisiwa, simu moja ya IPhone 5s yenye thamani ya milioni 1.5 pamoja na fedha taslim shilingi milioni nne zimeporwa na watu wasiofahamika ambazo ni mali ya Zhouguang Zheng
Alisema kuwa kufuatia tukio hilo watu 14 wamekamatwa na Kuhojiwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha katika vurugu hizo na wapo nje kwa dhamana na kwamba Jarada la Uchunguzi Limefunguliwa na Kupewa namba SO/IR/ 189/015 Na kwamba upelelezi bado unaendelea kufanywa na kwamba ukikamilika Jarada hilo litapelekwa Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali ili kulifanyia kazi kabla halijaenda Mahakamani
MWISHO