Wanaharakati walalamikia vurugu za mchina Songea

Wanaharakati walalamikia vurugu za mchina Songea

wafanyabiashara ya usafurishaji songea ni wapuuzi,wabnafsi na wanajiona wameiweka serikali mfukoni!
 
MADONGA-NYANI na BJB Wakuu acheni ushabiki wa K.ijinga watu wa Songea wanahitaji huduma bora habari ya Omarry kanyimwa kununua zong tong km za New Force ni uongo km Super feo alikuwa anataka ushindani wa huduma bora china kuna basi nzuri zaidi ya ya za New force mbona matajiri wote wa Tz walikuwa hawaruhusiwi kuagiza Yu tong kiwandani mpaka mpaka upitie kwa benbross ajent lakini ni Super feo peke yake alikuwa anaagiza gari kiwandani mbona hakuna mmiliki yoyote aliyelalamika na hakuna aliyemfanyia fujo Super feo?.najua mmemshindwa mchina kumpa maajari aanguke mchina mnaanza vurugu maana mabasi ya Songea ni uchawi tu.hapo hakuna kulalamika ni ligi tu nenda ruti zote mchina hafanyiwi vurugu kwa nini iwe Songea tu acheni huduma iongee acheni kulialia naijua hiyo biashara ya Songea toka enzi za Rajani Motor ways Kiswere na Specia Sleeping video Coach hapo kwa mchina mtatulia hatutaki maneno tunataka huduma
 
Siku ya hiki kisa nilikuepo na nilikua naelekea Dar lkn kwa ufupi Feo hawajui biashara kwani mchina alilipia ule muda hvo akawa na kibali na feo ndo walianza kumfanyia fujo mchina asitoe gari wakati kaulipia ule muda , nilichojifunza Feo biashara za ushindani hamtoweza na NF atawatoa barabarani sio muda mrefu kwani ana magari mengi
 
wafanyabiashara ya usafurishaji songea ni wapuuzi,wabnafsi na wanajiona wameiweka serikali mfukoni!

Dr hao vibaraka wa Omarry ni wajing.aa wanauzi sana matajiri wa Songea wakiona bus jipya linasumbua na linajaza watalifanyia visa uchawi watalichongea kwa matrafiki na Sumatra hadi mmiliki ataacha kupeleka bus atatoka Songea sasa Polisi wa Songea na Sumatra tumechoka tunahitaji ushindani wa kibiashara sio kubebwa waache abiria wachague huduma bora sio kubebwa na Serikali na Kisiwa kama umepigwa nenda Polisi sio ndio wanawafanya mnakuwa wapuuzi hamtaki ushindani kazi uongouongo tu.na bado kwa Mchina lazima mtulie
 
hakuna sababu ya msingi hapo kinachotakiwa gari za dar zote zitoke muda mmoja,,haiingii akilini gari inayoenda mbeya itoke saa kumi na mbili na ya dar itoke saa 1230.labda kama kampuni husika imeomba kuwa na ruti ya dar kwa muda huo lakini kama vinginevyo kuna kitu nyuma ya pazia
 
Safi sana mchina kwa kutembeza kipigo kwa Super feo maana wamezidi kulinga. sasa dawa yao imepatikana tunapanda newforce
 
Mnalalamika kila kitu, muda wote.Wakati mikono na miguu mnazo!! Ina maana hapo standi vijana wote mchina mmoja tu anawapiga wote? Kila kitu POLISI POLISI POLISI POLISI. Nyie hamuwezi hata kesho kuanzisha vurugu na kumhamisha hapa Tz? Wanaume mmekuwa kama wanawake!!! Ndio maana vitu vingine JK anajinyamazia tu!!
 
mchina kawakamata pabaya sana mana mbeya express mlisema hataweza ligi coz ana yutong sita na nyie mna zaidi ya 30 but huyu mchina hamtamuweza mana na yeye ana gari zisizo na idadi ni mwendo wa ligi mwanzo mwisho.kwa soko la mabasi mkitaka muwaweze hawa wachina nawashauri nyie team feo nunueni scania new model kwa hapa bongo hazipo ila niliziona mtandaoni zinapiga ruti ya zimbabwe to south africa hapo hakuna basi itakayotia mguu na mtaweza kukompiti hata ruti nyingine ndefu kama za tunduma,kyela,kigoma nk.lakini kwa yutong na zhongtong hapo ni bilabila.
 
Super feo wekeza kwenye customer care! Watumishi wako wanajisikia na wana lugha mbovu
Kwa hili nakubaliana na wewe maana kama wale akina dada wa Makambako ni ovyo kabisa pamoja na madereva wake, kuna wakati gari yake imegonga bajaj pale Ilangamoto Makambako dereva wa bajaj akafariki na mama mmoja akawa mahututi kwani hata kuzika walifika au kwa mgonjwa hata kwenda kumwona hawakukanyaga, kwa namna nyingine wacha waondoke kwani mbona Muhongo na PHD yake kaachia madaraka naye aachie Newforce Njia si vinginevyo. Mr. Omari nakushauri uende Mbalache utafute eneo upande miti tu biashara ya Magari ndio mwisho umewadia kwani akina Special, Kiswele, Summry na wengine wako wapi? Kibaya hata nyumba ya kuishi naambiwa amejenga mwakajana. Hivi wakinga wenzio hawajakwambia uza mabasi jenga hata gorofa moja Kariakoo.
 
Tena bado, akileta magari Color Star njia hiyo lazima ile kwako. Tunaomba Newforce muanzishe Route ya Songea Dodoma.
 
mchina kawakamata pabaya sana mana mbeya express mlisema hataweza ligi coz ana yutong sita na nyie mna zaidi ya 30 but huyu mchina hamtamuweza mana na yeye ana gari zisizo na idadi ni mwendo wa ligi mwanzo mwisho.kwa soko la mabasi mkitaka muwaweze hawa wachina nawashauri nyie team feo nunueni scania new model kwa hapa bongo hazipo ila niliziona mtandaoni zinapiga ruti ya zimbabwe to south africa hapo hakuna basi itakayotia mguu na mtaweza kukompiti hata ruti nyingine ndefu kama za tunduma,kyela,kigoma nk.lakini kwa yutong na zhongtong hapo ni bilabila.

Mkuu kwa TZ Scania haitalipa eti bei iko juu nauli ni ileile eti, Ukiona Abood au Shabiby ananunua Yutong ndio Omar/Super feo ataweza? Wa badili biashara tu.
 
Super feo wekeza kwenye customer care! Watumishi wako wanajisikia na wana lugha mbovu

Nami pia nimesafiri mara nyingi na mabasi ya kampuni hizi mfano mwaka jana dar-mbeya,songea-dar,dodoma-songea,iringa-mbeya-songea n.k.Wadau yote mnayosema mimi siyaelewi bali mimi ni msafiri mbobezi nayeishi dar.Ushauri wangu kwa wamiliki wa kampuni hizo wakae chini na kuelezana tofauti zao ili kuishi kwa amani na upendo,tofauti kibiashara ni kitu cha kawaida,bali muhimu ni amani na kufuata sheria za usafirishaji.Kama ikiwezekana nyie wamilki tafuteni watu wenye busara hata utawala wa mkoa ili suluhu ipatikane na upendo uwepo.Kugombana na kushughulikiana haina tija sana.Bwana Omary Msigwa una mabasi mazuri,mapya na yenye kiwango.Najua kuwa usimamizi umemwachia mtu,ila wewe fanya kitu wazungu wanaita "Management by walking around"(MBWA) ili kuangalia kama kuna customer care kwa wafanyakazi wako.Kiukweli baadhi ya wafanyakazi wako wana lugha mbaya na majivuno,wengine wanajiona kama wamiliki wakati sio.Hili lifanyie kazi ili biashara isonge mbele vinginevyo wateja watahamia kwa wachina,hasa wadada wameridhika sana hii ni tofauti na wachina.:yawn:
 
NINACHOKIJUA MIMI TOKA NDANI KABISA YA HUU UGOMVI ni kwamba super feo ana time table ya saa 6:00am na 6:10am kutoka songea na gari zake zote za dsm zipo ndani ya muda huo wakati huo huo mbeya na iringa na dom ana gari za saa 6:00am na 6:20am katika hali hii super feo inabidi atoke saa kwanza ndiyo new force afate saa 6:30am sasa inapoonekana super feo zinatoka zote kwa mara moja inaonekana kuna upendeleo kwake lakini si kweli ana vigezo vya kutoka muda huo sasa kilichofanyika hapa karibuni ni kwamba new force alipewa muda wa saa 6:10am na sumatra kwa madai kuwa super feo hana gari semi luxury ikabidi super feo alalamike kwanini iwe hivyo yeye pia ana semi luxury katika muda huo sumatra wakaingilia kati na kuamua kila kampuni ikae katika muda wake yaani super feo saa 6:00am na new force saa 6:30am sababu ikumbukwe kuwa mbeya express muda wake ni saa 6:20am ingawa hayupo kwa sasa!

CHANZO CHA UGOMVI SASA! super feo baada ya kuona kuna ushindani mkubwa baina yake na new force na magari wanayotumia ni tofauti yaani zhongtong newforce na yutong super feo,super feo akaenda kwa newforce ambae zamani alikua ni ajent wa yutong kwa sasa ni ajent wa zhongtong ili auziwe gari kama za newforce lakini new force akakataa kumuuzia gari hizo yaani zhongtong na hata super feo alipojaribu kuagiza gari hizo moja kwa moja kiwandani alikataliwa na wachina kununua gari hizo kwa kumwambia kuwa arudi kwa ajent wao wa TZ ambae ni new force ambae anamkatalia kununua gari hizo kwa hofu ya ushindani kuzidi ona Mtanzania huyu anavokandamizwa na mchina

KILICHOTOKEA SIKU YA TUKIO!baada ya sumatra kuwaondoa new force katika muda wa saa 6:10am ambao ni wa super feo newforce siku ile alitaka kutoka katika muda huo ndipo mfanyakazi wa super feo alihoji kwanini watoke katika muda huo wakati muda wao ni saa 6:30am ndipo mchina alipoanza vurugu na bwana kisiwa alipokwenda kuamua yakamkuta yale yaliyomkuta.

MASWALI YA KUJIULIZA
1>ni kweli uwekezaji wa mabasi umewashinda wazawa mpaka aje muwekezaji wa kichina
2>kama wazawa kama huyu watadidimizwa na mchina kwa kuendelea kukataliwa kununua gari zenye ushindani ajira za watanzania waliopo kwenye makampuni haya ya wazawa zitakuaje?
3>tusaidiane ni kweli wachina nauli wanazotoza zinaingia kwenye akaunti za benk zilizopo hapa kwetu au wanapeleka kwao
4>inasemekana kuwa hayo mabasi wanakopeshwa huko kwao je wanalipaje au ndo wanahamishia uchumi wetu kwao?

Mkuu ufafanuzi wako nimeuelewa kwa kina na ni mzuri sana, bado sijajua upo upande gani kwa maana ya conflict of interest ingawa naona kwa mbaaali umeegemea upande wa super feo labda sababu ya uzalendo lakini kama ni steak holder ni bora unge declare mapema ili wadau tujue.
BACK to the point....!!
Binafsi simfagilii mgeni mbele ya mzawa mwenzangu lkn swali..ni je nafaidika vipi na uwepo wa huyo mzawa? Hivi unaijua super feo vizuri wewe.? Jamaa ni jeuri kupindukia na hawana nidhamu kabisa kwa abiria,we ukitaka kunyanyaswa panda super feo afu wana wivu wa kijinga sana,huwa hawataki kampuni nyingine ilete mabasi kwenye route wanazopita, eti utasikia wanasema hii ni njia yangu....utafikiri ana hati miliki ya hiyo njia. Nitatoa mfano..!! Kuna kampuni ya Tonda express walianzisha route ya iringa-songea kuondoka ni 1asbh na 5asbh..! Super feo alimpiga vita kwa kumuwekea mabasi mengine kwa muda huo huo..! At last Tonda akatoka barabarani,kumbe wachina (tonda) walikuwa wanausoma mchezo na effects zake ni hii new force.
Kuhusu uajent: super feo ni agent wa yutong sijui kama kavuliwa au la na new force ni agent wa zongh thong buses ambaye ana uwezo wa kuzuia mtu mwingine hasiuziwe buses kutokana na pesa aliyolipa na mkataba waliosaini..ni kama ilivyokuwa kwa sumry na Nissan diesel. Ukiwa agent mkuu huwezi kukubali kuuza basi kwa mshindani wako hata siku moja..! Zhong Thong bus ni gari iliyokamilika kuliko yutong..mfano ni zhong thong ya saibaba tunduma-dar.
 
Mchina hana longolongo kwenye deal zake!!!amkeni watanzania hizo fursa chache ulizokuwa nazo na mnajisahau mchina akipata nafasi tu hakika lazima ile kwako!!!
 
Kwa hili nakubaliana na wewe maana kama wale akina dada wa Makambako ni ovyo kabisa pamoja na madereva wake, kuna wakati gari yake imegonga bajaj pale Ilangamoto Makambako dereva wa bajaj akafariki na mama mmoja akawa mahututi kwani hata kuzika walifika au kwa mgonjwa hata kwenda kumwona hawakukanyaga, kwa namna nyingine wacha waondoke kwani mbona Muhongo na PHD yake kaachia madaraka naye aachie Newforce Njia si vinginevyo. Mr. Omari nakushauri uende Mbalache utafute eneo upande miti tu biashara ya Magari ndio mwisho umewadia kwani akina Special, Kiswele, Summry na wengine wako wapi? Kibaya hata nyumba ya kuishi naambiwa amejenga mwakajana. Hivi wakinga wenzio hawajakwambia uza mabasi jenga hata gorofa moja Kariakoo.

Yupo Dada mmoja hivi pale Iringa yaani ana nyodo yule Dada sijapata kuona,sijui Omar anagonga papuchi pale au ni Dada yake. Yeye ndo alisababisha sipandi feo hata kwa dawa. Ovyo sana feo
 
Ni sawa, ila wazawa wakipata kidogo wanakuwa jeuri sana, hatuna adabu hata kidogo, yaani wafanyakazi wa gari za mikoani wanakosa utu mnno, inatakiwa abiria akishaksmilisha taratibu zote na akishaingia kwa basi ,asibugudhiwe tena kwa namna yoyote, utakuta sh 2000 ya kipasel inamtoa utu kondakta hadi unashangaa!!
 
Kwa hili nakubaliana na wewe maana kama wale akina dada wa Makambako ni ovyo kabisa pamoja na madereva wake, kuna wakati gari yake imegonga bajaj pale Ilangamoto Makambako dereva wa bajaj akafariki na mama mmoja akawa mahututi kwani hata kuzika walifika au kwa mgonjwa hata kwenda kumwona hawakukanyaga, kwa namna nyingine wacha waondoke kwani mbona Muhongo na PHD yake kaachia madaraka naye aachie Newforce Njia si vinginevyo. Mr. Omari nakushauri uende Mbalache utafute eneo upande miti tu biashara ya Magari ndio mwisho umewadia kwani akina Special, Kiswele, Summry na wengine wako wapi? Kibaya hata nyumba ya kuishi naambiwa amejenga mwakajana. Hivi wakinga wenzio hawajakwambia uza mabasi jenga hata gorofa moja Kariakoo.

Hao vibaraka wa Omary watafute mabasi mengine maana mwenye mabasi ameshasema hagombei tena ubunge.sasa tutaona nani atakutia tena kiburi na kwa mchina lazima ukae na Mr Liii anasema ataongeza nyingine ya Dar Mbinga na Songea Dar atatia 3 au 4 na ya Mbinga iwe ya 5.na km kawaida mchina amesema ruti ya Songea basi zitafanya miezi 6 tu anauza
 
Siku zote mkinga hawezi biashara ya ushindani anakimbilia kwenye vunja bei. ninachokijua super Feo ligi hawezi anategemea fitina ili kumtoa mpinzani barabarani. ili abaki peke yake aendelee kutanua. Angalia mby-songea. Iringa-songea. songea -dom. mbinga -dar. Huko kote kapita Bila kupingwa. Na sasa abiria wanakomaje na customer care mbovu. Usiombe yakukute. Sasa naona huyu Mchina anamtia wehu na kama asipojipanga kibiashara Kwa huyu Mchina atasanda. Newforce wako vizuri sana kaweza kushika njia ya Mbeya vizuri sana ambako Feo anaogopa kupeleka bus Ile hali ana tlb ya mby dar.
 
Yupo Dada mmoja hivi pale Iringa yaani ana nyodo yule Dada sijapata kuona,sijui Omar anagonga papuchi pale au ni Dada yake. Yeye ndo alisababisha sipandi feo hata kwa dawa. Ovyo sana feo
Kwa kesi ya wahudumu wa kike ni kweli ni 10% tu ya wahudumu wa kike Wana ustaarabu Kwa wateja na wengi kiumri pia ni wakongwe. Kama wale wamama wa pale dirishani songea wanajua jinsi ya kuongea na wateja na hii ni ksb washawahi fanya kazi na makampuni makubwa ikiwemo Scandinavia. ila hawa masista du wengine Wana jeuri sana sasa hatujui ni vinyumba ndogo vya bosi au wajomba. maana wanaona abiria kama washambawashamba.
 
Back
Top Bottom