Wanaharakati waijia juu smz

Marcossy A.M

Member
Aug 21, 2008
61
24
Wanaharakati walaani vurugu Zanzibar.
Wakiongea na vyombo vya habari, wanaharakati wa kituo cha sheria na haki za buinadamu wamekemea kwa ukali sana uvunjifu wa haki na kuteketezwa mali za wafanyabiashara wenye asili ya Tanganyika kulichofanyika Pwani Mchangani Zanzibar tarehe 7 Mei 2011.

Sehemu ya taarifa hiyo inasema..."Tumefuatilia, kugundua na kinasikitishwa sana na matukio ya uchomajimoto wa mabanda zaidi ya sabini na tatu yaliyokuwa yakitumiwa na wafanyabiashara wapatao mia moja na familia zao. Kitendo hiki kilifanywa na watu takriban sitini walifika katika maeneo ya wafanyabiashara wa vinyago, mama lishe na bar wakiwa na marungu,mapanga,visu,mashoka na chupa za petrol na kuanza kuchoma moto mabanda hayo bila kuwaruhusu waathirika kutoa mali zao, hata walipoomba, kutoa mali zao katika mabanda yao. Wafanya biashara hawa wana leseni za kufanya biashara na pia wamekuwa wakilipa kodi zinazotakiwa kihalali.Wakati wakiwa wanachoma vibanda hivyo walikuwa wanatamka kuwa hawawataki wabara warudi kwao na majina mengine wanayowaita watu wa bara kama ‘machogo'. Kitendo hiki kimeleta hasara inayokadiriwa kuzidi shillingi million mia mbili .

Kitendo hiki ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 17 inayoruhusu mtu kuishi katika sehemu yoyote ile aipendayo, Zanzibar ikiwa ni sehemu mojawapo.Ibara hii pia inapiga marufuku mtu kushurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.Ibara ya 22 inaruhusu mtu kufanya kazi yoyote ile halali na kupata ujira sawa na kazi yake, kuuza na kumiliki bar likiwemo.

Kitendo hiki cha uhalifu kwa minajili ya maeneo mtu atokako (Ubara/Tanganyika) na Udini (Ukristo wao) ni kitendo cha kibaguzi ambacho pia ni kinyume cha Ibara ya 13 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vitendo vya kibaguzi vya namna hii vinajenga mazingira yanayoweza kusababisha mauaji ya halaiki (Massacre) au mauaji ya kimbari (Genocide) kwa kuwa vinawabagua watu na kuwatendea kwa misingi ya dini zao, na sehemu walizotoka.

Mauaji ya Rwanda yalianza kwa vitendo vya namna hii vya kibaguzi. Serekali na wananchi waTanzania wasikubali kuruhusu na hata kuvumilia vitendo hivi hata kidogo".
 
WE WATU 60 WANAKUSANYIKA, WANACHOMA MAPANDA 100 NA USHEE HATA POLISI HAWAJUI? KUNA UKWELI HAPO? AU NDIYO UBAGUZI ALIOUTABIRI BABA WA TAIFA JK NYERERE? WAZENJ NI KWELI KABISA HAWAWAPENDI WATANGANYIKA, HATA VIONGOZI WAO WALIJUA HIZO NJAMA WAKALA POZI! TUTAWAFURUMUSHA NA SISI HUKU BONGO OOOh!!!!!
 
Polisi wa Zanzibar ni wanyanyasaji sana,sijui huku tukichoma nyumba za wapemba na maduka yao watatulaumu
 
Tuvute subira tuone serikali ya huko visiwani itakavyolishuhulikia suala hili; wabara wanaliangalia kwa jicho la karibu sana,na iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa dhidi ya wahusika hiyo itakuwa ishara tosha kuwa vitendo vile vilibarikiwa na uongozi wa serikali ya zanzibar nasi itabidi tukae chonjo!
 
Polisi wa Zanzibar ni wanyanyasaji sana,sijui huku tukichoma nyumba za wapemba na maduka yao watatulaumu


Maduka ya Wapemba yanahusika vipi hapa?

Mkiyachoma mtakosa pa kukopa maana Wabara wenzenu hawawakopeshi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom