Wanaharakati: Tanesco isiikatie rufaa Dowans

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,551
728,445
Wanaharakati: Tanesco isiikatie rufaa Dowans
Send to a friend
Tuesday, 11 October 2011 20:30


Geofrey Nyang’oro
BAADHI ya wanaharakati katika Jiji la Dar es Salaam, wamelitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), liache mpango wa kukata rufaa ya kupinga tuzo ya Kampuni ya kufua umeme ya Dowans na kwamba suala hilo sasa litaamuliwa na wananchi.Wanaharakati hao pia wameitaka serikali ieleze sababu za kuhamisha mkataba wa Richmond kwenda Dowans.

Akizungumzia mchakato huo wa rufaa ya dhidi ya Dowans, Mratibu wa Masuala ya Bunge wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Albania Marcossy, alisema kitendo cha Tanesco kutaka kukata rufaa kupinga tuzo ya mabilioni ya fedha kwa Dowans ni cha kusitajabisha hasa ikizingatiwa kuwa suala hilo lilipofikia haliwezi kuamriwa kwa kutumia sheria za nchi.

“Nimesikia leo (jana) Tanesco inatarajia kuwasilisha katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, ombi la kutaka kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuridhia malipo kwa Dowans. Hiki ni kitendo cha kustaajabisha, hivi ni kweli kuwa hadi leo Tanesco hajui kuwa kwa mjibu wa mkataba huo, baada ya hukumu kutolewa na tuzo kusajiliwa katika Mahakama kuu ya hapa nchini ,hakuna kukata rufaa,” alisema Marcossy.


Alisema, kwa mujibu wa sheria zilizopo suala hilo limefikia mwisho na hakuna mahakama inayoweza kubatilisha.
“Ndio sababu sisi kwa kutumia katiba ya nchi Ibara ya 27 (1) tunawahamasisha Watanzania ambao ndio wa miliki wa rasmali za nchi kujitokeza kwa wingi kutimiza wajibu wao wa kulinda rasmali zao zisiporwe,”alisema.

Kuhusu maadhimisho ya siku ya kifo cha Baba wa Taifa , Mwalimu Nyerere, wanaharakati wamewataka Watanzania kuingia katika nyumba za ibada kuliombea taifa ili Mungu awajalie uzalendo na ujasir wa kutetea rasimali za nchi yao kama alivyofanya kiongozi huyo.

Mkurugenzi wa Shirila la Sikaka, Irenei Kiria, alisema katika kipindi hicho wanachi watatakiwa kuvaa nguo nyeusi na kujifunga bendera ya taifa kichwani kuashiria maombolezo.Alisema mavazi hayo yanapaswa kulivaliwa kuanzia Oktoba 14 siku aliyofariki muasisi huyo hadi Oktoba 23 alipozikwa.

“Tuvae nguo nyeusi za maombelezo tangu siku aliyofariki hadi kuzikwa kwake, tuingie kwenye nyumba za ibada kumuombea na kukumbuka msimamo wake wa kupinga vitendo vya kifisadi na matumizi mabaya ya rasmali za taifa,”alisema kiria.Wanaharakati hao pia wameitaka serikali kutoa maelezo ya kina kuhusu sababu ya kupuuza ushauri wa kisheria wa kuvunja mkataba wa Kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

“Kwa mjibu wa washauri wa Kimarekeni Hunton &Williams LLP, wakati Tanesco inaingia mkataba na Richmond. Kampuni hiyo haikuwa imesajiliwa achilia mbali kuwa haikuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake chini ya mkataba,”alisema Kiria.

 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,551
728,445
[h=4]Comments [/h]


0 #6 tusikubaliunyonge 2011-10-12 09:11 Nadhani sasa imefikia ambapo lazima watu wakubali kutetea haki zao hata kama ni kwa kumwaga damu. Si halali kwa watu wachache kuumiza wengine bila wao kuchukuliwa hatua. Kwa kukubali unyonge ni kama kujinyonga
Quote

0 #5 Loliondo 2011-10-12 08:58 Hawa wanaharakati nao wanazidi kutuchanganya. Kulingana na Mkataba ulivyoisainia hiyo TUZO lazima ilipwe na hakuna mahakama yeyote inayoweza kutengua.

Wanaharakati wanajaribu kuzunguka mbuyu. Maandamano yanatakiwa yawe na ajenda ya kumshinikiza Kikwete awachukulie hatua wale wote waliotuingiza kwenye ufisadi huu. Wametajwa in black and white ktk repoti ya Mwakyembe.

Kama JK atagoma kuwachukulia hatua basi tuandamane tumshinikize yeye JK atuachie nchi yetu kama walivyofanya wananchi wa Tunisia, Misri etc.

Tuache porojo, vinginevyo hili genge la mafisadi litatumaliza.
Quote

+1 #4 kifaru 2011-10-12 08:41 Mimi naamini hakuna njia nyingine ya kulikomboa taifa letu zaidi ya kuandamana kumtoa kikwete ikulu. Kama rais anafikia mahali anatangaza mbele ya kadamnasi kuwa wanaotaka urais 2015 wafanye kazi sasa hivi, maana yake ni kwamba yeye kazi yake imekwisha, unategemea nini ktk utendaji wake?
Mi nafikiri ili kumuonyesha kuwa hii nchi si ya viongozi bali ni ya wananchi, lazima tumng'atushe kabla ya 2015 ili na wengine wapate akili.
Quote

0 #3 smart 2011-10-12 07:38 mwl nyerere alisha sema u[NENO BAYA] ni jambo usoolijua ukijua u[NENO BAYA] unatoweka,lakin i m[NENO BAYA] ni kipaji ulichonacho hautoki hata kama unaelazwa kila siku hivo basi ktk sakata hili jk umesimama wapi? jifunze kutoka libya na misri mataifa yanayotuzidi kiuchumi na kijeshi pia lakini uma umetake adv.
Quote

+1 #2 joseph Masanja 2011-10-12 01:53 WATANZANIA TULIPOFIKA HAPA TUACHE UTANI NCHI INAANGAMIA HALAFU TANESCO WANASEMA WANAKATA RUFAA WAKATI HIZO PESA TUNAJUA ZINATOKA MFUKO WA TANESCO ZINAINGIA MIFUKO YA ROSTAMU AZIZI NA KIKWETE? HAWA JAMAA VIPI?!
Quote

+1 #1 joseph Masanja 2011-10-12 01:51 HUU MCHEZO ANATUCHEZEA KIKWETE NA GENGE LAKE LA WEZI AKINA ROSTAM AZIZI NA NGELEJA ANAYELINDA MASLAHI YA MWAJIRI WAKE WA ZAMANI ROSTAM AZIZI NA KIKWETE, WANADANGANYA TOTO ATI WANAKATA RUFAA HIVI HAO WANASHERIA WA TANESCO NI WANASHERIA WA KWELI AU WAIGIZAJI TU? WANAUMA NA KUPULIZA JAMANI HII NCHI AIBU TU, HIVI WEWE KIKWETE UNAFANYA NINI HAPO IKULU?
QuoteRefresh comments list
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom