Nipo makini kufuatilia mwenendo wa media katika hii kamatakamata ya watuhumiwa wa kutekwa, kuteswa na kuumizwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, na kuteswa wanahabari kwa ujumla wao kwani haijulikani nani atafuatia kung'olewa kucha na jicho baada ya Kibanda. Nataka kuwaiti je, wanahabari baadhi wataendeleza ushabiki wao kwa Chadema badala ya kuwa objective Kama taaluma inavyowataka? Nimeona udhaifu mkubwa kwao kushabikia zaidi Chadema kinyume cha mipaka yao ya kazi. Let's stay tuned
Naomba nitangulie kusema kwanza nina heshimu observation yako juu ya topic hiyo ya waandishi wa habari, "ushabiki" wao kwa CHADEMA (as you suggest), wimbi la utekaji na yote hayo., Lakini LAZIMA iwe wazi tu kwamba waandishi wahabari wana haki, (pamoja na professional ethics zao zinazo wataka kuwa objective) - ya kueleza/ kuonyesha opinion yao kuhusu chochote kile wazi bila kuhitajika kuficha,. haki hiyo hatuwezi kuwapokonya! niyakwao kwa sheria ya tanzania kama wananchi wa tanzania hii.
lakini pia lazima tukubaliane kwamba hatutegemei kwenye nchi yenye vyombo vya habari zaidi ya elfu moja na waandishi professionals kwa maelfu yao, WOTE wawe na mtazamo unao fanana, ni wazi wapo watakao kua na mtazamo flani kuhusu jambo flani na wengine watakuwa na mtazamo mwingine tofauti kuhusu jambo lilelile na hii haimfanyi mwandishi mmoja kuamshabiki wa CHADEMA na mwingine wa chama kingine eti kwasababu tu ya mtazamo wake juu ya swala flani. OF COURSE! ni jukumu na wajibu wa mwandishi yeyote kuhakikisha kuwa anaandika habari kwanza yenye UKWELI mtupu (atleast kwa kiwango atakacho jiridhisha nacho), lakini pia Yenye kusikiliza pande zote (objectivity iwepo), yenye ushahidi na vyanzo vya uhakika, na yenye kujenga jamii badala ya kubomoa., lakini mtazamo wao juu ya jambo lolote haupaswi kutafsiriwa kama ushabiki kama hayo niliyo yasema hapo juu yamezingatiwa.
lakini pia LAZIMA NI SEME HAPA kwamba kama tuta sema "natuone sasa" kama waandishi wataendeleza ushabiki wao kwa CHADEMA atawakiwa wanatekwa na kuteswa TUTAKUA TUNAKOSEA SANA SANA SANA., kwakuwa lugha hii inaonyesha siotu kutokua na kujali, au kutokua na huruma na hawa waandishi wetu lakini kuyafurahia haya yanayoendelea sasa hivi, nakuonyesha WAZI kwamba kumbe kuna watu wa kundi flani ambao wao wangefurahia haya kuwapata waandishi wenye mtazamo positive juu ya CHADEMA na kuonekana vikwazo kwa chama kingine flani,. nahii inatupa mwanga kabisa kwamba huenda watu hao (wanao ona waandishi ni wa shabiki wa CHADEMA) wasi ishie hapo tu ila wakaamua kwenda mbali zaidi na kuanza kuyatekeleza haya tunayo yaona sasa nakisha kupakaza kwa watu wengine ilikuficha ushahidi., Well, nisiende mbali sana, sina nia ya kum
convict mtu yeyote hapa, ila ninacho kisema nikwamba sisi kama wana nchi tunao ipenda Tanzania yetu hii tulipaswa kukataa kabisa haya., bila kujali ni chadema, tlp, cuf ama ccm.
lakini kwa muda sasa inanipashaka kwamba huenda kuna watu wana tumia JF kuendeleza propaganda chafu za vyama vyao. LAKINI HII SIYO SAWA hatakidogo!!.,
Niombe watanzania wenzangu kwapamoja, tuulinde uhuru wa vyombo vya habari na wana habari wetu., kwakua pasipo hawa ukombozi wa taifa letu ni mgumu sana sana sana., mahali popote pale ukombozi wa taifa ulipo hitajika WANAHABARI ndiyo walio fanya kazi kubwa zaidi ya ukombozi., popote pale.
South Africa wakati wa Apartheid na utawala wa the Nationalist Party kilicho kua na mitazamo ya kibaguzi haikukombolewa na Nelson Mandela peke yake kwa mikono yake mwenyewe., ukiwa mchunguzi wa haya utagundua wapo waandishi wa habari walio sacrifice wengine zaidi hata ya Mzee Mandela wakati wa Liberation Struggle ya nchi yao. read about
Michael Harmel a key figure in the underground communist party, a founding member of the Congress of Democrats and an editor of
the magazine liberation.. kulikua na
Benjamin Pogrund of
the Rand Daily Mail.,
Patrick Duncan Editor and Publisher of the
Contact news paper na wengine wengi., Mandela na wenzake wasinge iweza kazi ile bila hawa!!
Ninachokisema hapa nikwamba HAWA NDIYO WAKOMBOZI WA TAIFA HILI (Waandishi wa Habari)., pamoja nakwamba tutasimama wote wananchi pamoja na viongozi wa vyama vyetu katika mapambano dhidi ya UFISADI, UBADHILIFU WA FEDHA, na KUTOKUWAJIBIKA KWA SERIKALI ZETU,. lakini hatutaiweza kazi hii ya ukombozi na ulinzi wa rasilimali za taifa LETU bila ya hawa watu,. hawa hatuwezi kuvumilia kuona wakitumiwa vibaya kwa michezo michafu ya kipropaganda alafu tuka kaa eti tukisema "ngoja sasa tuone kama wataendelea kushabikia CHADEMA".,
Ndugu zangu
Ni hayo.,
Asanteni