Wanafunzi wote wanaojiunga na elimu ya juu wanapaswa kupewa mikopo

Bin Chuma75

JF-Expert Member
Dec 15, 2012
948
1,000
Ni wakati sasa Serikali kupitia wizara ya elimu inafaa kuliangalia hili swala la mikopo ya elimu ya juu(vyuo vikuu)

Wanafunzi wote wanaomaliza kidato cha sita na kujiunga na vyuo vikuu inapasa wapate mkopo wa kujiendeleza bila matabaka

Kigezo cha kusema waliosoma private school mikopo haiwahusu sio sawa, pengine ndio kasomeshwa private school lakini mzazi au mlezi amefilisika au kapata changamoto nyingine za kimaisha, hivyo hawezi kumuendeleza mtoto na elimu ya chuo, je huyu mtoto si atakosa haki yake ya kujiendeleza kielimu?

Huyu mtoto anaenyimwa mkopo wa kujiendeleza halikuwa kosa lake yeye kusoma private school, ni wazazi au walezi ndiyo walimpeleka huko, anaponyimwa mkopo kwa sababu hiyo ni kumuadhibu mtoto kukosa elimu ya juu kwa sababu wazazi au walezi walimsomesha private school.

Na ikumbukwe huu ni mkopo kwa wanafunzi, sio msaada, ni kwamba watatakiwa kulipa madeni yao yote kwa mujibu wa sheria, sasa kwa nini wasikopeshwe wote wanaohitaji mikopo?

Serikali hii sikivu ni bora iangalie hili jambo kwa jicho lingine, maana sio haki kumnyima mwanafunzi kwa Kigezo cha kusoma private, ingekuwa hivyo basi hata mabenki yasingewakopesha matajiri kwa sababu wao wanapesa nyingi, wangekopeshwa masikini tu.Sent using Jamii Forums mobile app
 

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,997
2,000
Usemayo kwa serikali hii ni ndoto tu, wanakuambia kila mwenye uhitaji atapata halafu hata kabla maombi hayajafika wanakuambia mwaka huu ni 50% ya waombaji ndiyo watapata mkopo. Sijui nani kawaambia wenye uhitaji ni 50% ili kukuumiza wanasema tunanunua ndege kwa fedha yetu taslimu. Wanajua wenyewe vipaumbele vyao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom