John W. Mlacha
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 3,504
- 1,341
Wanafunzi wengi wanafuja posho wanazolipwa
Imeandikwa na Mwalimu Stanislaus Kigosi; Tarehe: 14th July 2011 @ 23:20 Imesomwa na watu: 136; Jumla ya maoni: 0
WANAFUNZI wa vyuo vya juu wamekuwa na madai mengi, mojawapo ikiwa ni kutaka kuongezwa posho.
Nimekuwa nikitafakari kuhusu madai ya wasomi wetu hao, kwamba wanaweza kutafakari vipi juu ya hicho wanachokililia. Sina wivu wala ugomvi na madai yao, lakini napata kigugumizi kuhalalisha madai yao.
Nitatoa ufafanuzi hatua kwa hatua ili tuone ni kwa kiwango gani sasa wasomi wetu, wanakuwa na ubinafsi uliopindukia kiasi hiki. Madai ya wanafunzi wa vyuo vikuu hayajaanza mwaka huu wala si kuwa kizazi hiki cha baada ya uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kumekuwapo madai yasiyo na ukomo.
Nakumbuka kuna siku nilikuwa nikiongea na mmoja wa wanafunzi wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), waliosoma nchi ilipotoka kupata Uhuru, ikiwa na mahitaji makubwa sana ya wataalamu wa fani mbalimbali.
Kutokana na uchache wao, wanafunzi walikuwa wakigharamiwa kila kitu na Serikali. Walikuwa wakipata mlo kamili ambao hata katika familia zao ilikuwa ni simulizi ya kusadikika.
Alichoniambia huyu mkongwe ni hiki; sisi ndio tuliofaidi elimu ya chuo kikuu. Mnaingia chuoni na kukuta kila kitu kipo pale Serikali imewawekea. Nadhani huyu mzee alisahau kuwa ni kodi za Watanzania walizokuwa wakizitumbua.
Jambo la kustaajabisha ni kuwa hata katika mlo wao wakikuta eti mkate umekuja bila siagi, basi walifanya mgomo wa kula na kuingia madarasani. Ni kweli waliishi maisha ya raha mustarehe.
Wakati huo huo hakusita kusema ukweli kuwa vitu hivyo kwa mara ya kwanza katika maisha yake alianza kuvitumia akiwa chuo kikuu. Hakuwahi kuvipata mahali pengine popote. Hivyo ukweli ulio hapo ni kuwa wao kama wasomi waliongozwa na choyo na tamaa ya kula na kusaza wakati sehemu kubwa ya Watanzania wakiwa masikini vijijini.
Kuna siku Mwalimu Nyerere, nasimuliwa, aliwahoji wanafunzi wa UDSM baada ya kugoma kuingia madarasani kwa sababu ya kupungua yai moja katika mlo wao: Je, tuongeze kiwango cha kuwatoza kodi wazazi wenu ili kuweza kupata yai la ziada katika mlo?
Hapa ndipo inapolala hoja ya kuwa asije akatokea mwanafunzi yeyote wa elimu ya juu akadhani kuwa ni Serikali ndiyo inampa fedha; hiyo ni kodi ambayo wakulima na wafanyakazi wa taifa hili tunakamuliwa ili wanafunzi wasome.
Nikumbushe kuwa mnamo 2008 nchi ilishuhudia mgomo wa wanafunzi wa vyuo vikuu, hasa vile vya Serikali, ambao nadhani utaendelea kukaa katika historia ya migomo hapa nchini kwa muda mrefu bila kusahaulika.
Mpaka leo naamini kuwa ule ulikuwa ni mgomo wa haki na wenye kubeba uhalisi wa maisha ya Watanzania wengi. Ulikuwa mgomo ambao wanafunzi walitaka waondolewe mzigo wa ada katika mabega yao na mabega ya wazazi wao.
Wanafunzi hawakudai kupewa fedha ya mfukoni, madai yalikuwa kupata ada kwa asilimia 100. Walitambua kuwa ule ulikuwa ni mkopo na ada inakwenda moja kwa moja chuoni bila kupitia katika mikono ya wanafunzi.
Walikuwa tayari kuendelea kupata fedha ya kujikimu katika kiwango kile kile, lakini walau mzigo wa ada upunguzwe.
Matokeo yake walifukuzwa vyuoni kama waasi. Nami nilikuwamo. Lakini walau tulirudishwa kwa masharti magumu kiasi, na waliofuata baadaye walikuta walau Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imefanya marekebisho ya kuridhisha kwa kiwango fulani, mabadiliko ni vita.
Lakini tu naomba nitofautiane na madai ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa sasa kutaka kuongezewa fedha ya kujikimu wanapokuwa vyuoni.
Nitapenda kutoa mifano na maelezo ya kina ni kwa nini madai ya wanafunzi wa elimu ya juu, na pengine makundi mengine ya wasomi kutaka kupata sehemu kubwa kuliko watu wengine ambao nao ni raia halali wa taifa hili.
Kwanza ieleweke wazi kuwa wanafunzi wa elimu ya juu kudai kupewa Sh 10,000 kama fedha ya kujikimu kwa siku, maana yake ni kuwa kwa mwezi wanafunzi hawa watakuwa wakijipatia si chini ya Sh 300,000 isiyokuwa na makato yoyote.
Japokuwa hapo kuna madai ya kuwa fedha hiyo ndiyo inayotumika kulipa sehemu ya ada au sehemu ambayo Bodi ya Mikopo inakuwa haijawalipia, vijana wenzangu watambue kuwa fedha hiyo wanayodai ni kubwa mno, hasa tukizingatia kuwa hawazalishi chochote zaidi ya kutumia kilichozalishwa na wengine.
Labda kama hili hawalijui, kuna watu wanalipwa mshahara wa mwezi wa Sh 162,000. Hao ni watumishi wa Serikali wala si wa sekta binafsi. Tukiwa na vigezo kuwa wao wanaishi Dar es Salaam na wamepanga mitaani, hoja hii haina mashiko ya kutosha, kwa sababu kwanza si vyuo vikuu vyote viko Dar es Salaam.
Kuna vyuo viko Iringa, Mbeya, Mwanza na kadhalika. Watu walio katika maeneo hayo nao wakiwa na malalamiko kama ya wenzao wa Dar es Salaam, basi hapo kinachotawala ni uchoyo na hulka ya ubinafsi kwa wanafunzi hawa.
Nikirudi kwa wanafunzi walioko vyuo vya Dar es Salaam, wajaribu kumfikiria mtumishi niliyemtaja anayelipwa mshahara wa Sh 262,000. Anapanga mtaani na ana watoto anaowasomesha.
Hivi kati ya hawa wawili mwanafunzi wa chuo kikuu na huyu mzazi anayelitumikia taifa ni yupi anastahili kuonewa huruma? Bila kuweka ubinafsi wala uchoyo mbele, kimsingi huyu ambaye tayari ni mzalishaji anatakiwa kuonewa huruma na kupewa kipaumbele ili awe na tija kwa taifa.
Ni kweli kuwa fedha wanayopewa wanafunzi wa elimu ya juu ni kidogo, lakini pia anayopewa huyu mtumishi ni kidogo vilevile. Lakini kitu kimoja wanafunzi wengi wa elimu ya juu wanashindwa kuonesha ni nidhamu ya matumizi katika hiyo fedha kidogo wanayopewa.
Ukitaka kujua kuwa wanafunzi wengi wamekosa nidhamu katika fedha hiyo, tazama kipindi ambacho vyuo vinafunguliwa au kipindi ambacho wanafunzi wamelipwa hiyo fedha ya kujikimu.
Matamasha ya bei mbaya yanakuwa yameandaliwa, na wanafunzi hao hawaoni shida kutoa kwenda kuhudhuria. Nakumbuka nikiwa chuoni, kipindi chuo kinapofunguliwa watu walikuwa na kawaida ya kuandaa matamasha hayo, na kinachotokea watu wanafuja sana fedha kwa anasa na starehe za muda mfupi.
Katika mazingira ya kawaida, hata ukimwambia mtu kuwa fedha haitoshi, atabaki akikutazama na asikuelewe, kwani ameshaona jinsi unavyoifuja fedha hiyo.
Nimalizie kwa kusema kuwa, sasa ni wakati wa wanafunzi na kundi zima la wasomi kukaa na kuwafikiria Watanzania masikini wasiokuwa na uhakika wa mlo japo mmoja kwa siku, ili nao waishi kwa amani na matumaini huku kwa pamoja tukiunganisha nguvu dhidi ya ufisadi.
Mwandishi ni Mwalimu katika Shule ya Sekondari Nyumbu iliyoko Kibaha. Pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu na mambo ya vijana katika siasa.
Simu: +255 754 257 251 au +255 714 801 893, Barua pepe: stanislaussenior@yahoo.com
Imeandikwa na Mwalimu Stanislaus Kigosi; Tarehe: 14th July 2011 @ 23:20 Imesomwa na watu: 136; Jumla ya maoni: 0
| ||