Wanafunzi wauawa kwa kupigwa risasi Guinea

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
_94767554_f1c312f2-a8af-436a-bf71-af55aa0b973f.jpg

Takriban watu watano wameuawa nchini Guinea wakati vikosi vya usalama vilipopambana na wanafunzi waliokuwa wakiandana wakitaka mgomo wa walimu kumalizika.

Wanafunzi walijitokeza kwa wingi na kwa hasira wakaanza kuwatupia polisi mawe.

Maafisa walithibitisha vifo hivyo na kuwalaumu waandalizi wa maandamano kwa kupanga kile kilichotajwa kuwa maandamano haramu.

Mfanyakazi mmoja wa hospitali aliliambia shirika la AFP kuwa waliouawa walipigwa risasi kwa karibu na polisi wa kuzima maandamano.

Takriban watu 30 walijeruhiwa wakiwemo maafisa wa vikosi vya usalama. Waalimu nchini Guina wamekuwa kwenye mgomo wakilalamikia mishahara duni.

Chanzo: BBC/Swahili
 
Back
Top Bottom