Wanafunzi wanusurika kifo kisa dereva kuchati na simu


Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
5,708
Likes
6,424
Points
280
Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
5,708 6,424 280
WANAFUNZI 30 wa shule ya msingi binafsi ya Little Treasure, iliyoko Manispaa ya Shinyanga, wamenusurika kifo baada ya kupata ajali wakati wakirejeshwa nyumbani kutokana na dereva wa basi hilo, Emmanuel Faustine (32), kuchati na simu ya mkononi huku akiendesha.

Ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 9 alasiri katika eneo la Kalogo mjini hapa barabara ya Mwanza.

Basi hilo lenye namba za usajili T183 AFE likitokea shuleni na kusambaza wanafunzi nyumbani kwao na lilipofika eneo hilo, lilitumbukia mtaroni na kusababisha ajali.

Akizungumzia ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga, Kamishina Msaidizi (ACP) Simon Haule, alisema wanafunzi 30 walikuwa wamesalia kwenye basi hilo na hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya kupata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao.

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva ambaye alikuwa akichati na simu wakati akiendesha hatua ambayo ilisababisha kutumbukia mtaroni na kusababisha ajali huku akikimbilia kusikojulikana.

Kamanda Haule alisema kutokana na ajali hiyo, wanafunzi walipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa matibabu.

“Jeshi la Polisi linamsaka dereva wa basi hili ambaye alikimbia mara baada ya kusababisha ajali, ili achukuliwe hatua kali za kisheria na liwe fundisho kwa madereva wengine ambao wamekuwa wakisababisha ajali za lazima na kugharimu maisha ya watu pamoja na kuwapatia ulemavu,” alisema Haule.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa, Dk. Albert Masigati alisema alipokea wanafunzi 30 na baada ya kuwapatia matibabu, 26 waliruhusiwa na kubakia wanne wakiendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko, ambaye aliwatembelea wanafunzi hao hospitalini hapo, aliwapongeza madaktari kwa kufanya kazi zao kwa ufanisi kuokoa maisha ya watoto hao.

Mboneko pia alitoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kuwa makini wanapokuwa barabarani kwa kutii sheria ili kuepukana na ajali zisizo la lazima.
 
N

Nsamaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2016
Messages
4,646
Likes
24,628
Points
280
N

Nsamaka

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2016
4,646 24,628 280
Kwakweli ilikuwa taharuki, mwanangu pia anasoma kwenye shule yaan nilichanganyikiwa sana. Nilipopiga simu kwa mwl wake wa darasa, nashukru Mungu hakuwa amepandishwa kwenye hiyo route ya kwanza. Kalibaki kusubiri route ya pili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
savage94

savage94

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2018
Messages
263
Likes
307
Points
80
savage94

savage94

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2018
263 307 80
Hapana unawasiliana na mwenzako alietangulia kukwambia minara iko wapi..huwez elewa,vinginevyo hela yote ya emergency itaishia njiani
lakn mwishoe wanapoteza umakini barabaran mkuu. kuna siku mambo kama hayo yalitaka tupeane uso kwa uso

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,250,106
Members 481,224
Posts 29,720,833