Wanafunzi wanazidi kuharibika tu

TAECOLTD

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
1,051
Reaction score
1,845
Jana nikiwa kwenye mwendokasi natoka zangu kwenye shughuli zangu nimejichokea nawaza familia plus namna ya kuitafuta grisi, pembeni kulikua na wanafunzi kama wanne hivi wa kiume na kwa muonekano na mazungumzo yao basi ni wa kidato cha kwanza au cha pili.

Basi aina ya mazungumzo yao yaliniacha mdomo wazi ingawa sikutaka wajue kuwa nawasikiliza vizuri, tena wanaongea kwa nguvu tu wenyewe wanajiona wanaongea kwa mafumbo ila mie nimesoma secondary enzi za raisi mkapa plus kukaa na wahuni vijiweni basi maneno ya kihuni na ya mtaani nayajua vyema tu, kwa maelezo yao ni hivi
Pale mbezi Kuna hawa wauza CD mbalimbali zikiwemo za ngumi, Korean dramas na zingine na hawa wauzaji wanakuaga na pilau yaan picha chafu ila hawaweki juu, Sasa basi dogo mmoja akasema yeye anaenda na hela yake akimuonesha muuzaji sababu ya ukata wa maisha haangalii kuwa bado ni katoto kadogo basi anamuuzia ili naye mkono uende kinywani

Mwenzake akamuuliza anaangalia wapi au watu wakishalala, akajibu kuwa wazazi wake wakisafiri au wasipokuwa nyumbani sababu inaonekana wana shift za usiku maybe basi wadogo zake wadogo wakilala basi anajiachia na picha hizo chafu. Wenzake wakmwambia awapeleke anaponunulia wakakubaliana wakifika mbezi mwisho atawapeleka... Sasaaa bwana swala likaja je "umeshafanya" hiyo ni kwa mafumbo hapo, kadogo kakajibu "ndio" mweeh nikaduwaa katoto kadogo kameshagonga? Wakaanza kubishana mara muongooooo muongooooo, mwingine akadakia ye anaenda fanya leo yaan jana hiyo, wakamuuliza nani huyo akasema anajua mwenyewe huku anakuna kuna kitambi... Hahahahahahahahahahahah halafu wanafunzi wakipiga sifuri mnalaumu huku mkitaka kuweka usawa na shule za private

Kizazi cha Sasa hakuna ufuatiliaji kuanzia nyumbani kwa wazazi, ndugu wala shuleni, Sasa watoto wa form 1 tayari wanajua mambo ya ajabu hivyo je form 4 wapoje? Dunia imevaa gagulo kwakweli

Tusipoziba ufa jibu tunalo, Kizazi cha Sasa kimeharibika kweli
 
[emoji23][emoji23][emoji23]daah hawa watoto wa siku hizi ni hatari kweli
Kabisa ndugu yaan hapo nime summarize maana yapo mengi ya ajabu walikua wanaongea yaan hakuna lolote linahusu shule waliloongelea kabisa
 
Wanafunzi sijui ni Wa Dar tu au na mikoani ni majanga.

Huko kwenye mwendokasi wanachambana na watu wazima kisa siti.
Maneno yao ukiwasikiliza mmmh.
Ukiwakuta wamejaa mikadi na coco ni balaa
 
MI NIKAJUA WAMEHARIBIKA WANAFANYA MAPENZI SHULE MADARASANI.HAYO MAMBO MENGINE NI NGUMU MNO KUYAZUIA.KAMA NCHI TULIKWISHA POTEZA DIRA KATIKA SUALA YA MAADILI
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kizazi kijacho hiko mkuu washaandaliwa urithi hao
 
Mkuu Dunia ya leo nishida, wanafunzi darasani wanawaza ngono tu. Nakumbuka kipindi nipo form one kulikuwa na mabinti wanapiga story za ngono na kuambiana hadi style wanazotumia wakati wakilana na wame za watu. It was 14 years ago.. I do no now days,
 
Huyo dogo aliekuwa ana kuna kitambi kakipata wapi? Kashaanza kula beer na nyama?
[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] labda mkuu itakua maana kama wanaweza kupiga shoo kwa umri wao bila shaka na gambe wanasukuma kiuficho ficho aiseee
 
Hahahaha! Wananenepeana hovyo maana hawajitesi kusoma
 
Wanafunzi sijui ni Wa Dar tu au na mikoani ni majanga.

Huko kwenye mwendokasi wanachambana na watu wazima kisa siti.
Maneno yao ukiwasikiliza mmmh.
Ukiwakuta wamejaa mikadi na coco ni balaa
Sijui bora Dar, maana Tabora nishida sana Mkuu
 
Kabisa ndugu yaan hapo nime summarize maana yapo mengi ya ajabu walikua wanaongea yaan hakuna lolote linahusu shule waliloongelea kabisa
Ila tatizo ni utandawazi. Mimi nashauri wanafunzi wote wangekuwaga boarding tu
 
we unawawazia watu mabaya tu kwani we uliyemaliza form four ukapata division 1 mbona still unahustle namaisha ...Swalah la maadiri na mtu kuweza kufany vizur darasani avina uhusiano..wowote....pia uwezi kufananisha shule private na za Umma ..elimu yakununua na yabure aviwez lingana...pia ....sasa unataka watu na maadiri kwa Elimu mbovu. ya bure....Jitafakali....maana hata sisi tunakiongoz kazaa na mke wamtu ila bado anatuongoza vzr.
 
sio bure ww, CPZ zinakuhusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…