‘Wanafunzi wanageuza nyumba madanguro’

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
Lilian Lugakingira,
Bukoba

SHULE za sekondari za kata zilizojengwa bila mabweni ya wanafunzi, zinasababisha watoto kuishi katika mazingira hatari, imeelezwa.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia Maendeleo ya Wananchi wa Wilaya ya Karagwe la Karagwe, alipokuwa akizungumza katika semina ya wadau wa Shirika la misaada ya jamii la (SATF), iliyofanyika katika Manispaa ya Bukoba.

Katibu huyo Melania Bitakwate, alisema shule hizo zimejengwa mbali na maeneo ya makazi ya wazazi wa watoto, jambo linalowalazimisha kupanga nyumba zilizoko karibu na shule.

Alisema hata hivyo kitendo hicho, kinatishia maisha ya watoto hao na hasa wa kike ambao wamekuwa wakipata vishawishi na hivyo kupata mimba.

“Nyumba hizo zinageuzwa kuwa madanguro au magheto, watoto wanakuwa na uhuru kupita kiasi, wa kike wanawakaribisha mwanaume na wa kiume wanajiunga na vikundi vya watu waovu kama wavutaji bangi,” alisema Bitakwate.

Alisema serikali inapaswa kufanya jitihada za kujenga mabweni katika shule hizo, ili kuondoa tatizo hilo na kuwawezesha watoto kuishi katika mazingira yanayokubalika.

Kwa upande wao, wanafunzi waliohudhuria semina hiyo, walisema tatizo la watoto kuishi katika mazingira hatari, linatokana na mmomonyoko wa maadili na umri mdogo wa walimu washauri wanaopelekwa katika shule.

“ Wanafunzi wanawadharau walimu washauri, utakuta mwalimu mshauri ana umri wa miaka 21, wakati mwingine hana tofauti na wanafunzi, wanakuwa kama wanalingana hawamsikilizi na ushauri anaoutoa hawautiwi maanani” alisema Egberth Fabian.

Mwalimu Diocres Nestory wa Shule ya Sekondari Kalema,Bukoba Vijijini, alisema serikali haijatimiza wajibu wake wa kuweka walimu washauri na kuwa waliopo wanapatikana kwa jitihada za wakuu wa shule.

Akizungumza katika semina hiyo, Ofisa Mkuu wa SATF, Beatrice Mgaya, aliwataka watoto wanaofadhiliwa na shirika hilo kuongeza bidii katika masomo.

Mwananchi

Uongozi wa shule uko wapi? Maafisa elimu wako wapi? Jumuiya za wazazi zinafanya nini kunusuru kashfa hii ya taifa la kesho?

Watoto wanatumia viungo vyao walivyopewa na mungu. Hapo tatizo liko wap?

Broda co huko karagwe2 yaani mfano mzuri hapahap Dar shule zipo 3 ambazo ninaushahidi na mazingira ya wanafunzi wake kimalazi 1.KISOTA 2.SOMANGIRA 3.ABOUD JUMBE Nazo ni zakata jamani wanafunzi hawa hawana non mutual assistance so kutokana na hayo Elimu ita thaminika kweli

Gharika yaja ndugu zangu...siyo za kata tu hata za zamani k.v Jitegemee wanafunzi wanapanga mageto keko,chang'ombe na kurasini wanamegwa kinominomi

Badala ya kutafuta suluhu ya tatizo hili, Prezida wetu mwenyekiti wa chama cha magamba, alishawahi kutamka kuwa watoto wa kike wanapata mimba kutokana na kiherehere chao!!

Badala ya kutafuta suluhu ya tatizo hili, Prezida wetu mwenyekiti wa chama cha magamba, alishawahi kutamka kuwa watoto wa kike wanapata mimba kutokana na kiherehere chao!!

kwan hujui ka nae huwa anawamega?

wewe kama nan sasa?

kama Mtanzania.. Tujiheshimu, pia lazma tuheshimu utu wa watu wengine. Sio vizuri kumvunjia mtu heshima, ongea kitu ambacho una uhakika nacho.

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom