DOKEZO Wanafunzi wanaagizwa kupeleka matofali ikiwa kama adhabu wanapofanya makosa shuleni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna tofauti ya kupewa vifaa ufyatue na kwenda kununua soma uelewe, hela za kununua tofali watoto wanapata wapi?
ndo utoe hela ununue ndio kwani hiyo adhabu amelazimishwa kufanya, kwanza tofali tatu ni chache sana
shemeji yangu yuko advance, ukichelewa rimu mbili
 
tofali inafyatuliwa,si hamtaki viboko?
mi huwa nawaambia kama ya hapa yanakushinda kaangalie maisha kwingine.
sa hivi kuhama ni rahisi sana pia
Elewa tofauti kati ya kufyatua na kununua, kufyatua material na vifaa vipo hiyo sawa, wewe unampa mwanao hela za kununua tofali shule?
 
Kama tofali zinazokusanywa zinatumika kwa matumizi ya shule na sio walimu binafsi napendekeza waongeze idadi ya matofali hata kufikia 30 kwa kila adhabu.
 
Kama tofali zinazokusanywa zinatumika kwa matumizi ya shule na sio walimu binafsi napendekeza waongeze idadi ya matofali hata kufikia 30 kwa kila adhabu.
Kujenga shule ni kazi ya serikali, na hata hivyo shule zenye upungufu serikali ilishajenga madarasa nchi nzima 15000 kwa pesa ya covid. Na bado kuna pesa ya tozo inajenga pia.

Huyo Mwalimu ni mhuni, ubaya ni kwamba anafanya kwa wazazi wasioelewa chochote.
 
Sawa kujenga shule ni kazi ya Serikali ila uongozi wa shule hauzuiwi kufanya maendeleo yanayoinufaisha shule ndio maana zamani kulikua na mashamba ya shule na miradi mingine mbalimbali. Narudia tena kama hiyo adhabu haimnufaishi mwalimu binafsi idadi za matofali ziongezeka tena kwa sasa naoendekeza ziwe 58 kwa kila adhabu
 
ndo hivo nilichelewa siku 6, ko nkafyatua tofali 600.

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Hakuna kitu Kama hicho, hao wanafunzi wasipopeleka tofali hakuna kitu walimu watafanya. Mwalimu kazi yake sio kujenga shule bali kufundisha, hayo mambo ya kpeleka tofali ni upumbavu.
 
Wazazi


Wakichapwa mnalalamika wakipewa adhabu za nje mnalalamika

Waalimu wakazie hapo hapo malezi yamekuwa magumu mno wazazi wanajifanya wana uchungu hawataki watoto waonywe

Mwisho wa siku wanaongeza panya road mtaani
 
Shule yetu ilikua na mashimo ya tofali kwaajili ya wakiukaji sheria,, ukifeli hupigwi una gonga zako tofali 50, usipoenda shule wiki unafatwa nyumbani na fimbo nyingi na shuleni tofali 100,, utovu wa nidhamu mwingine kama kumpiga mwanafunzi mwenzako tofali 100,,

Sasa kuna mwamba alimtongoza ticha wa field akamchoma kwa master,, alafu akampiga monitor mnoko mnoko alivoona makosa mengi akakacha shule miezi miwili siku ya kufatwa home mwamba alipigwa adhabu tofali 1500 na mzazi wake akapitisha adhabu jamaa wiki nzima anapiga adhabu sasa wewe mkuu tofal 3 hadi thread JF.
 
Soma uelewe,sijasema kupiga tofali, mwalimu anamwambia mwanafunzi akanunue tofali hela anapata wapi? Ulishawahi kumpa mtoto tsh 10000 aweke ili alichelewa kumaliza kazi za darasani alipe kama adhabu?
Hii ni sawa na kulipia adhabu kwa pesa badala ya kazi na viboko, hakuna mwongozo wa elimu unaoruhusu mwanafunzi kulipia makosa yao ya kishule kama kutokusaya daftari, kupiga kelele na kuchelewa kwa pesa
 
Watoto wakichapwa, mnalalamika! Wakipewa adhabu mbadala, mnalalamika! Wakiachwa halafu baadaye wakafeli mitihani, mnalalamika!

Ukiona mambo huyawezi, mhamishie shule nyingine! Sawa mzazi.
 
Watoto wakichapwa, mnalalamika! Wakipewa adhabu mbadala, mnalalamika! Wakiachwa halafu baadaye wakafeli mitihani, mnalalamika!

Ukiona mambo huyawezi, mhamishie shule nyingine! Sawa mzazi.
Ndio mwongozo unavyosema mwanafunzi atoe pesa akifanya kosa? Tena kosa la kutokusanya daftari?
Bei ya tofali unaijua? Huyo mtoto anapata wapi 5000 tshs za kwenda kununua tofali na kuzileta shuleni? Au mmekula hela za ujenzi mnatafuta pa kuijazia?
 
Ndio mwongozo unavyosema mwanafunzi atoe pesa akifanya kosa? Tena kosa la kutokusanya daftari?
Kila sehemu kuna sheria na taratibu zinazofuatwa! Huo siyo mwongozo. Ila kwa vyovyote vile bidi ya shule itakuwa imeridhia kutolewa kwa adhabu ya aina hiyo ili kujenga uzio wa shule, baada ya serikali ya ccm kuwekeza nguvu kubwa kwenye kununua Ma V8 ya kutembelea viongozi wake!

Kama huwezi kuvumilia, mhamishie mtoto wako shule nyingine! Maana hakuna namna. Kinyume na hapo, mfunde mtoto wako kufuata sheria za shule kwa ukamilifu.
 
Mambo ya kawaida tumepitia sisi mfano Mkuu high sec miaka ya 2000 tumefanya kazi sana za kujenga misingi ya parade acha kudekeza watoto acha walimu wale watoto wetu kwa misingi ya nidhamu
 
Alafu anatokea bwege mmoja anasema sio sawa
 
Kukimbia tatizo si kulimaliza, hapa ni mwazo wa kufikisha ujumbe kwa mamlaka husika, haiwezekani mwanafunzi ashindwe kuandika kazi au akose swali mzazi ukanunue matofali, kuna adhabu za kufyeka nyasi, kuchimba mashimo, kudeki madarasa na vyoo, hill la mtoto kutozwa pesa haikubaliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…