Wanafunzi wafichua siri wanaowalawiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wafichua siri wanaowalawiti

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MziziMkavu, May 21, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Wahusisha wazazi, walezi majumbani
  [​IMG] Ni baada ya kampeni ya `watoto tuache tuseme`


  Tukio la Wanafunzi kufanya vitendo vya kulawatiana katika Shule za Msingi Yombo Buza jijini Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya kubainika baadhi ya wazazi na walezi wanahusika kwa kuwafanyia vitendo hivyo watoto wao majumbani.

  Kubainika kwa hali hiyo kumekuja baada ya uongozi wa Manispaa ya Temeke kuanzisha kampeni maalum inayoitwa 'Watoto tuache tuseme' inayohusisha shule 10, ambapo watoto hao wanapata nafasi ya kuelezea matatizo mbalimbali yanayowapata au kuyaona ndani ya jamii.

  Akizungumzia suala hilo, Afisa Elimu Kilimo, Saveria Kannole, ambaye pia ni Mratibu wa kampeni hiyo, alisema watoto hao wamefichua siri hiyo baada ya kutakiwa kuandika ujumbe kwenye karatasi unaozungumzia maisha yao pamoja na matatizo ndani ya shule yao.

  Alisema kutokana na kupewa nafasi hiyo wanafunzi hao walieleza matatizo yao mbalimbali na baadhi yao walifichua kuwa baadhi ya wazazi wanawalawiti wanaporudi majumbani kwao na kuomba wapewe matibabu.

  Alisema kampeni hiyo ya watoto tuache tuseme imepelekwa shuleni hapo mara baada ya kutokea matukio ya wanafunzi kulawitiana kwenye shule hiyo kama njia ya kuongeza uelewa wa kujifahamu na kutambua thamani yao miongoni mwa wanafunzi hao.

  "Tumegundua na kubaini chanzo cha wale watoto mpaka kufikia hatua ya kulawitiana na kuvuta bangi inatokana na baadhi ya wazazi kutowajibika katika malezi na wengine kuhusika kuwafanyia watoto wao vitendo hivyo vya kinyama," alisema Kannole.

  Alisema imekuwa vigumu kuwakamata wazazi wenye tabia hiyo kutokana na ujumbe walioandika watoto hao kutokuwa na majina wala anuani zao za kuwatambulisha.

  "Kuna mmoja alifichua kuwa akirudi nyumbani mjomba wake anamfanyia vitendo hivyo, lakini tulishindwa kumpata baada ya wanafunzi wenzake kutokuwa tayari kumtaja," alisema.
  Alisema kimsingi hawajachukua hatua ya kuwafukuza shule watoto waliotajwa na wenzao kwamba wanajihusisha na tabia hiyo kutokana na kupingana na sheria ya haki za watoto.

  Kannole alisema kitu walichokifanya ni kuhakikisha wanaunda timu maalumu ya kubadilisha mienendo ya watoto hao pamoja na kuwapa uwezo wa
  kuongea mara wanapoona kuna tatizo.

  Mafanikio yanayopatikana katika mpango huo ni pamoja na watoto ambao hawawezi kujirekebisha kuamua kuacha shule wao wenyewe baada ya kuona wanafunzi wote wamekuwa wazi kwa kuripoti kwa walimu kila kitu wanachokiona.

  Afisa Elimu huyo alisema kampeni hiyo iliyoanza kwa shule 10 ndani ya Manispaa inafadhiliwa na Shirika la watoto Duniani (Unicef) ambapo inahusisha shule za msingi Temeke, Bahati, Wailes, Likwati, Nzasa, Chemchem, Charambe, Kilamba, Chekeni mwasonga na Vumulia ukooni.

  Alieleza kuwa katika shule hizo zilizoanza na mpango huo hakuna kesi zinazohusiana na vitendo viovu kwa wanafunzi kutokana na matukio mengi kabla ya kufanyika kujulikana na kudhibitiwa na walimu.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,478
  Trophy Points: 280
  Waende na kinondoni,
  wasisahau shule za st. mary's.
   
 3. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Wamechelewa tu kujua,lakini tatizo ni kubwa tofauti na wanavyofikiria,vijeba wapo karibu kila shule, na kazi yao ndio hiyo ya kudanganya wenye umri mdogo na kuwaingilia! Hilo zoezi liwe endelevu ikiwezekana liwe la nchi nzima,tusisubiri mpaka wafadhili watusaidie,huku watoto wetu wakiendelea kuharibiwa!
   
 4. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  du! Kweli wakienda kinondoni watakuta wengine wameoana kabisa
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  duh.....
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  una mtoto st.marys?
  uliwahi sikia haya?
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  sheria za kama IRAN zahitajika hapa tanzania kukomesha janga hili
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mmh! Kweli kizazi cha sasa tuombe MUNGU tu.
   
 9. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kweli, wazazi wa sasa nao tuombe Mungu tu.
   
 10. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  ni imani za kishirikiana zinazopelekea mzazi kumlawiti mwanae wa kumzaa, kwa sababu hakuna starehe yoyote anaopata.
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,478
  Trophy Points: 280
  Nilisikia kuwa wale wabeba watoto
  walikuwa wanahakikisha kabinti kadogo kamoja
  kanakuwa kamwisho kwenye bus, hivyo ni lazima
  wakafanya mle kwenye gari,
  baada ya walimu kupitisha vikaratasi kuwa nini hupendi
  kakasema ni 'school bus' walipokachunguza zaidi ndo kakayaweka wazi.

  kesi ilifunikwa.

   
 12. pgasper

  pgasper JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 311
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo ndo ivo
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  duh.....
   
 14. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2012
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,784
  Likes Received: 1,970
  Trophy Points: 280
  Mmmh! Mungu tusamehe waje wako, dunia imekwishnei jamani
   
 15. papason

  papason JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Nchi hii kuna umuhimu wa kuepo mahakama ya kadhi! Kwani dawa ya moto ni moto!
   
Loading...