KERO Walimu wa Shule za Msingi Gmhasa Tumaini iliyopo Ilala wanalazimisha Watoto waende wikiendi wakiwa na hela za mitihani

KERO Walimu wa Shule za Msingi Gmhasa Tumaini iliyopo Ilala wanalazimisha Watoto waende wikiendi wakiwa na hela za mitihani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wazazi na wanafunzi tunalalamikia tabia ya baadhi ya walimu wa Shule za Msingi Gmhasa iliyopo Ilala, Dar es Salaam kuwashinikiza watoto kuhudhuria shule siku za mwisho wa wiki (Jumamosi), pamoja na kuchangishwa fedha za mitihani.

Inadaiwa kuwa baadhi ya mitihani hulipiwa, jambo ambalo linaibua maswali kwa wazazi kuhusu matumizi ya ruzuku ya serikali inayotolewa kwa ajili ya uendeshaji wa shule.

Pia, watoto ambao hawahudhurii masomo ya Jumamosi au kushiriki michango hiyo ya fedha, wanasemekana kuadhibiwa siku ya Jumatatu wanaporejea shule. Hali hii imekuwa ikiwatia wasiwasi wanafunzi na wazazi kwa ujumla.

Wazazi wanaiomba mamlaka husika kulifuatilia suala hili ili kuhakikisha sheria na taratibu za elimu zinazingatiwa, na haki za watoto zinalindwa.
 
Ningekua mwalimu nisingeangaika kabisa, nafundisha vipindi vyangu nasepa ,asiye elewa atajua mwenyewe anaelewa pia atajua mwenyewe
 
Hili la kulipia mitihani, mlinzi, chakula, Tuition, na mengine mbona lipo kila mahali. Tena maeneo mengine wanachangia mchango wa madawati.
 
Wazazi na wanafunzi tunalalamikia tabia ya baadhi ya walimu wa Shule za Msingi Gmhasa iliyopo Ilala, Dar es Salaam kuwashinikiza watoto kuhudhuria shule siku za mwisho wa wiki (Jumamosi), pamoja na kuchangishwa fedha za mitihani.

Inadaiwa kuwa baadhi ya mitihani hulipiwa, jambo ambalo linaibua maswali kwa wazazi kuhusu matumizi ya ruzuku ya serikali inayotolewa kwa ajili ya uendeshaji wa shule.

Pia, watoto ambao hawahudhurii masomo ya Jumamosi au kushiriki michango hiyo ya fedha, wanasemekana kuadhibiwa siku ya Jumatatu wanaporejea shule. Hali hii imekuwa ikiwatia wasiwasi wanafunzi na wazazi kwa ujumla.

Wazazi wanaiomba mamlaka husika kulifuatilia suala hili ili kuhakikisha sheria na taratibu za elimu zinazingatiwa, na haki za watoto zinalindwa.
Vipi hao watoto wenu wasipopewa hiyo mitihani ya mara kwa mara, halafu wakafeli mitihani yao ya mwisho! Lawama mtazipeleka kwa nani? Halafu unayafahamu kwa kina matumizi ya fedha za serikali (capitation) kwenye shule zake?

Na hapo usikute mchango wenyewe ni buku tu! Mngesomesha watoto wenu shule za kulipia si ndiyo mngezimia kabisa! Imagine mahafali tu ya mtoto wako mzazi unatakiwa kuchangia laki na kuendelea!
 
WE mzazi na haobwazazi wenzenu acheni ufala.
1. Hiyo mitihani ina mchango mkubwa sana, haswa kwenye elimu yetu sisi ya kumeza meza.
2. Walimu inawaongezea kakipato, atleast wasiwe wanafundisha na stress.

Mimi nimesoma katika shule ambayo darasa la 7 mitihani ilikuwa j5 na j1.
Madarasa mengine ilikuwa ni kila j1, ile mitihani ilitusaidia sana sisi ambao huwa hatuhangaiki kujisomea kabisa na wale wazee wa kujisomea.
 
Back
Top Bottom