Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma vs Binafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma vs Binafsi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ngoshwe, Nov 13, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Wana JF, sina nia ya kuponda products za vyuo vikuu binafsi, ila kuna tofauti kubwa sana hasa katika utendaji kazi kati ya wanafunzi wanaomaliza vyuo vikuu vya umma na wale wanaotokea vyuo vikuu binafsi. Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika ajira niliyonayo sasa. Kwa mujibu wa majukumu niliyonayo, nimekuwa nikikutana na watendaji wa umma tofauti na wengine wamefanya kazi chini yangu. Hata hivyo, ukichunguza uwezo wa kufaulu, inaonekana kuwa wale waliotoka vyuo binafsi wengi wamefaulu kwa viwango vya hali ya juu ukilinganisha na wanaotokea vyuo vya umma. Lakini kwenye utendaji, inakuwa vigumu sana kwa baadhi ya wanaotokea vyuo binafsi kuelewa mambo haraka tofauti na ufaulu wao kitaaluma unavyoonyesha. Sijui tatizo lipo wapi!!!
   
 2. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Walikuwa wanadesa sana vyuoni!!!.
   
 3. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Kaka vyuo binafsi vipo kibiashara zaidi na swala la taaluma hiyo ni kimpango wako mwanachuo utakavyo jiweka ukiwa mtafutaji utatoka na taaluma kama zezeta utatoka kama ulivyoingia chuo,kutokana na hili kuondoa wanafunzi chuo kwa tatizo kama la kufaulu kwa mwanafunzi chini ya kiwango ni kama kudoloresha MTAJI hivyo watawapa GPA nzuri za kuvutia ila kumbe haziwastahili.

  Kingine hemu tuwe wawazi kwenye hili,hapa Tanzania vipanga(vichwa) wengi wanaishia vyuo vya umma na hivyo binafsi wanaenda kwa wingi wale waliofaulu kwa kiwango cha chini SOURCE:prospectus cut-off point.Hapa utaona wale wote watoto wa kishua waliopata mguu nje mguu ndani(nusura ya div 4) ndio wanajazana huko.Ila vyuo vya umma kutokana na michuano zinaingia div 1 na div 2 hapa sanasana udsm,ardhi,muhimbili na mzumbe.Ila vingine unakuta div 3 za kutosha sanasana vyuo vyenye ngazi ya taasisi kama ifm,iaa na tia.

  Kwa kumalizia ni vizuri muhitimu akahukumiwa kutokana na usahili na vyeti visipewe kipaumbele sana katika kumjua muhitimu yupi ni fake na yupi ni real.NAWASILISHA.
   
 4. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,134
  Likes Received: 10,487
  Trophy Points: 280
  Mod jamani mbona husikii kilio cha watuuuuu!!! tuliashasema thread zinazohusu ubora wa vyuo ziondolewe.
   
 5. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Tanzania ni nchi changa na ina mapungufu mengi sana tena mengi yapo kwenye elimu maana taifa lenye wasomi ndio linaloimarika,wewe unadhani jukwaa la elimu limeundwa kuongelea ishu za kitchen party? Hii thread haina malengo ya kukashfu chuo ila imeanzishwa ili wanajukwaa tujadili kuhusu uwezo wa vyuo binafsi ili jamii ijue uhalisia wa hivyo vyuo katika kuzalisha wataalamu.
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  zipo thread za kuondoa si hii.

  Hapa mtoa mada amekuwa too general. Sio mbaya. Lazma tujadili ili tuweze kufikia malengo. Mtoa mada hajatetea chuo kimojokimoja. Tatizo liko wapi hapo?
   
 7. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Kwa mawazo yangu.

  1. Ubora wa waalimu: waalimu wengi wazuri wapo vyuo vya serikali. Vyuo vya binafsi vingi vinategemea waalimu kutoka vya serikali.

  2. Uchanga wa vyuo: vyuo vingi vya binafsi bado ni vichanga. Havina infrastructure za kutosheleza wanafunzi wote.

  3. Beusiness oriented: vyuo vingi vya binafsi wapo kimaslahi. Pesa mbele Elimu baadae.

  4. Nature ya wanafunzi wanaodahiliwa. Kabla ya Tcu kuchukua jukumu la kuwapangia wanafunzi chuo, mwanafunzi alikuwa ana uwezo wa kwenda chuo anachotaka. Ilikuwa vigumu sana kumpata mtu aliyefaulu vizuri kwenye vyuo binafsi.

  5. Mazingira ya kujisomea.

  N.B. Mawazo yangu binafsi, naruhusu kukosolewa ila kistaarabu.
   
 8. N

  Ng'wanhale Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It is true because I have a real example @ our university(the name in blackets) most of our lectures forces us to use resources which are produced with them by forcing that if u didn't buy that resource u will get supplimentary in u're exam. This is bad behaviour b'se it makes the colie to be domant in everything. What I want to say the government under the TCU should take care and make sure that what is going on, on every universities should be relevant to the government universities by looking the RESOURCES, AVAILABILITIES OF THE PROFFESORS, THE COURSES WHICH IS PRODUCED THERE e.t.c.
   
 9. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Aiseeeeeeeeee!
   
 10. K

  Kanyigo JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  unaitaji ligi na Mwl nyerere campus zamani mlimani...
   
 11. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Serikali ilikurupuka sana,hvo vyuo vya binafc vingeanza kutoa diploma na certificates kwanza kabla ya kuhamia kwenye degree!ona sasa,sa hvi pesa nyng zinatumika kuwafadhili watu ambao bado watakuja kuwa mzigo kwa taifa.
   
 12. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  KIKWETE, LOWASA, JAIRO, LUHANJO, KAPUYA, MUNGAI, Walisoma vyuo binafsi?
  Nimetaja wachache tu. Mama yangu aliwah kuhudhuria interview moja ya kazi. Wanachuo waliotoka UDSM walitia aibu. Unaambiwa hata hzo barua za maombi ilikuwa shida.
  Potential ya mtu kazini ni mtu mwenyewe, na si chuo alichosoma.
  Nawasilishaa
   
 13. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,335
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Jamani mpigieni makofi kaka HAM-D leo kafunguka vizuri tehe tehe jokes tu kaka
   
 14. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,335
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Today let me teachyu mathematics.Eliminate the blackets to that above comment then put "UDOM"This is the concept of BODMAS. then wait for Ng'wanhale to mark.
  (I don knw why am happy today)
   
 15. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,335
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Another point from HAMY-D naomba kukuuliza kaka leo Umekula nini maana....?
   
 16. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  nimecheka sana na vizungu mlivyojitutumua, nadhabi kuna umuhimu wa kuwa na english test (speaking & writing) ktk usaili
   
 17. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #17
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mantiki sio kwamba wote wanaosoma vyuo vya umma wanafanya vizuri makazini, hali kadhalika sio wote wanaotoka vyuo binafsi wanafanya vibaya, bali kwa asilimia kubwa kuna tatizo sana makazini hasa kwa wahitimu wa vyuo binafsi mkuu. Labda ni staili inayotumika kufundishia. Kuna mmoja ametuleeza kuwa upo wakati wakufunzi wanalazimisha kutumia "notes' kufundishia huko vyuoni bila kujali zinakidhi kwa kiasi gani mitaala iliyopo...lakini pia tatizo limeanza kuonekana hata kwa baadhi ya vyuo vya umma ambavyo vinajiongezea jukumu la kudahiri wanafunzi wengi pasipo kuzingatia mazingira vyuo husika.
   
 18. double R

  double R JF-Expert Member

  #18
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 1,355
  Likes Received: 744
  Trophy Points: 280
  Ni kweli wengi wanaodahiliwa kwenye vyuo vya binafsi matokeo yao ya kidato cha sita hayakuwa mazuri. Historia inaonesha zamani vyuo vilikuwa vya serikali tu na watendaji wengi walikuwa wa nature moja, ila watendaji hao ndio wametufikisha hapa kielimu, kisiasa, kijamii, kiteknolojia. Ni hao watendaji ambao leo wana uwezo wa kuwasomesha watoto wao shule za binafsi ambazo kwa sasa ndio zinafaulisha kwa kiwango cha juu wanafunzi wengi na ni hao wengi ndio wanaokwenda kwenye vyuo vya serikali. Wengi wa wanafunzi ambao wanasoma au wamesoma shule za serikali sasa hawafaulu vizuri ndio wanaishia vyuo hivi vya binafsi. Wakati huo huo kundi la watoto wamatajiri ambao hawakufaulu vizuri huenda kwenye vyuo vilivyo vya taasisi na binafsi.
  Baada ya hayo, wengi waliotoka shule za binafsi walio vyuo vya serikali wanaumia na taratibu za vyuo hivyo na kushindwa kufanya vizuri. Walio vyuo vya binafsi wengine wanafaulu ki uhalisia hali wengine wakipendelewa kwa sababu ni watoto wa fulani, au wanafanyiwa mitihani.
  Kizazi kilicho kazini ndio kina uzoefu wa vyuo vya serikali kutoa wanafunzi bora kwa ufanisi kwa sababu wimbi la shule binafsi lilikuwa bado halijapata soko. Sasa mfumo mzima wa elimu bora umeharibika, jamii itegemee hasara juu ya hasara. Wakati fedha za walipa kodi zikitumika kuwakopesha na kuwasomesha wanafunzi walio na uwezo wa kipesa kwa bei nafuu, watoto wa maskini wanaumia kulipia gharama kubwa za vyuo binafsi na kupoteza muda mwingi katika kutafuta pesa kwa ajili ya gharama hizo huku wazingatii masomo yao.
  Ni kama mtu mwenye ugonjwa wa muda mrefu, atazidiwa na kufa. Mfumo wa elimu bora uko hatihati kufa.
   
 19. C Programming

  C Programming JF-Expert Member

  #19
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 1,766
  Trophy Points: 280
  vyuo vya kibongo vyote uozo mtupu na ubabaishaji......tunasoma kwa nadharia ila practical hamna kitu kama unabisha mtafute mtu anayesoma it au computer science mpe kazi ya kitendo ......yaani utacheka anachokifanya
   
 20. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  generalization yako sio sahihi mkubwa na ningependa uangalie vyuo binafsi kwa umakini kabla ya kutoa maoni humu JF. Mfano ukiangalia vyuo vingi vya umma ndio vinaongoza kwa wanachuo wake kufanya mafunzo ya vitendo mfano pale ardhi kila mwisho wa muhula wanachuo wote wanafanya field na ni kwa mda wa siku 80,ukienda udsm pia courses nyingi ukiondoa za CASS na UDBS(kwa mwaka wa kwanza hawana mafunzo ya vitendo) ila collages zingine wanafanya haya mafunzo.

  Ukija kwenye vyuo binafsi huko ni mwendo wa projects yani wanachuo mpaka wanahitimu hawajawahi fanya haya mafunzo sasa kwa hali ya kawaida tu unatarajia ufanisi kutoka kwa muhitimu huyo? Maana wengi wao mpaka wakae sawa inabidi ofisi itumie nguvu ya ziada ili akae sawa katika hiyo taaluma ambayo kwa ofisi zinazo-recruit vizuri hawezi kupata nafasi muhitimu wa hivyo vyuo binafsi.
   
Loading...