Wanafunzi wa vyuo vikuu msikubali kupewa panado kama tiba pekee kwa ugonjwa huu wa maleria ya mikopo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Kutokana na sakata la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini kuwa dowa kwa serikari ya awamu ya tano nchini. Waziri wa Elimu sayansi na teknolojia nchini Prof Joice Ndalichako amejitokeza katika vyombo vya habari siku ya jana na kutoa msimamo wa wizara yake.

Msimamo huo umekuja mara baada ya wanafunzi wa UDSM na viongozi wa serikali ya wanafunzi DARUSO kuamua kwa kauli moja kuto kusaini pesa za mikopo zilizotolewa vyuoni mpaka pale watakapopata ufafanuzi na msimamo wa wizara kuhusu hatma ya wanafunzi waliokosa mkopo na hata wale waliopata mikopo kidogo kwa kisingizio cha matumizi ya mfumo mpya wa utowaji wa mikopo kulingana na uwezo wa mwanafunzi uliotumiwa katika vipengele vyote vya mkopo.

Mara baada ya fukuto hili waziri anawapa majibu wanafunzi kupitia TBC kuwa
"Kutokana na malalamiko yao sasa anaiagiza bodi kutowa boom kiasi cha 8500 kwa sasa na vigezo hivi vipya vitatumika semister inayofata mara baada ya wanafunzi kupewa elimu na kuvielewa vigezo hivi".

TAFSIRI YAKE NI KUWA
kwa sasa bodi watatoa shiling 8500 kwa siku lakini haitakuwa hivyo kwa semister inayoanza mwezi wa tatu mwaka 2017.
Yaani hapo mtarudishwa kutumia mfumo wa mean test unao zingatia asilimia ulizo nazo kwenye vipengele vyote vya nikopo kama boom,field na hata stationaly.
na hii msitaraji kuwa itawahusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza tuu hapana itawahusu ninyi nyote kuanzia mwaka wa kwanza mpaka tatu, nne hata watano kwa wale wanaosoma miaka mitano.

Pili tafsiri ninayopata ni kuwa waziri hana mpango na wala hatarajii kuongeza idadi ya wanufaika wa mkopo mwaka huu wafedha tofauti na wale 24000 aliopanga kuwapa mikopo kwa mwaka huu wa fedha 2016/2017

Waziri hana mpango wowote wa kubadili hata moja ya vigezo alivyotumia kutoa mikopo mwaka huu ikiwemo kigezo cha kuwapa mikopo wanafunzi waliosoma masomo ya sayansi huku wale watoti washule za kata tuliokosa waalim wa sayansi na kusoma masimo ya sanaa tukitupiliwa mbali kabisa.

Waziri hajaweka wazi tafsiri mbovu iliyotolewa na naibuwake kuwa viwango vipya walivyotumia ni kwa mujibu wa muongozo wa bodi, sera ya elimu ya mwaka 2014, mpango wa maendeleo wa mwaka 2025 na hata irani ya uchaguzi ya CCM 2015.
Jambo ambalo ni upotoshaji kwani nimesoma vyote hivyo havielezi kile kinachoelezwa na naibu waziri wa Elimu.

HATUA ZA KUCHUKUA.
viongozi wa serikali za wanafunzi kwa kushirikiaana na mtandao wa wanafunzi nchini TSNP tuunde kamati ndogo ya kufatilia swala hili kiundani kwa kusoma maandiko tajwa hapo juu na kujenga hoja madhubuti za kuzipeleka kwa waziri wa elimu, waziri mkuu na ofisi ya RAis wa jamuhuli ya muungano ya Tanzania.

Pili kuanzia sasa wanafunzi wa vyuo vikuu na viongozi wa tusilieleze wala kulichambua jambo hili kwa hisia na mihemko bali tusome maaandiko tajwa hapo juu na kama wanazuoni tuje na hoja kuntu badala ya kulia na kulalama.

Tatu wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini tuungane kwa pamoja na kuwa na sauti moja kupitia viongozi wetu kisha tutapeana taarifa nini cha kufanya kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

MWISHO

wanafunzi wa elimu ya juu nchini ndio wasomi wa leo na kesho wa taifa hili hivyo lazima tuudhihilishie umma kuwa tunaweza kutatua changamoto zilizo wakabili kwa miaka hamsini sasa tangu uhuru kwa kuanza na chngamoto hii ya mikopo.

Wanazuoni Tunao uwezo wa kumfanya NDARICHAKO na hata kiongozi yeyote wa juu au chini yake kuondoka katika kiti chake na kiti hicho kukaliwa na watu wengine.

Kama swala hili la mikopo litatushinda basi tunakila sababu ya kurudisha kodi za watanzania tulizotumia miaka kadhaa kwa kupata elimu tuliyonayo.

TANZANIA MPYA HAITAJENGWA NA WASOMI KUTOKA KENYA WALA UGANDA ILA SISI

Kushiriki harakati hizi za kuisaka haki ya mnyonge sambaza ujumbe huu umfikie kila mwanachuo.
 
Kuna wale wajinga wa uvccm chuoni
Huwasukumia wasio wa ccm waandamane ili wao wasionwe wabaya na baba zao wa ccm
 
Huu utani sasa umezidi,yani baada ya semester ya kwanza wanarudishwa misri tena???nilishawahi kusema serikali isiendeshe hii bodi kwani ukosefu wa hela serikalini huathiri kwa aslimia zote utoaji wa mikopo kwa wanafunzi ambapo mwisho huja na hoja dhaifu za vigezo na viwango vya utoaji mikopo that are not even practicable.
Hii bodi ikipewa secta binafsi mambo kama haya hayawezi kutokea ila kwa kuwa hawataki ushauri naona dalili ya tukio kubwa hapo mbeleni kati ya wanafunzi na bodi/serikali
 
Tuliambiwa wanafunzi watapata mikopo bila usumbufu tena wote kwa mbwembwe na atakaechelewesha atakiona kumbe hamna lolote leo wamekuja na masharti kibao utazani sio mkopo bora kiongozi aliyepita alikuwa mtu
 
sioni umuhimu wa phd holder hawa km ndalichako,mkulu wa kaya na lipumba coz hawana +ve impact kwa nchi yetu sana sana majanga tu
 
Back
Top Bottom