Wanafunzi wa vyuo msikubali kurubuniwa

Wanafunzi wa vyuo msikubali kurubuniwa

Chance ndoto

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2017
Posts
4,621
Reaction score
10,847
Wanafunzi hususani wale wa chuo hasa wa mwaka wa kwanza msikubali kurubuniwa au kudanganywa na watu msiowajua au marafiki zenu kwamba kuna ujanja wa kutokulipa ada au kumpa mtu pesa na kukufanyia registration huo ni uong, pia ukila ada itakucost sana usije kudanganyika na vitu vidogo punguza tamaa, fanya malipo, kafanye registration ingia darasani, timiza wajibu wako, fanya quiz, fanya course work yako kua juu, huo ndio urahisi wa maisha yako kama mwanachuo.

semester zilizopita za mwaka wa masomo 2017/2018 imetokea wanafunzi wengi sana kuibiwa kwa njia hiyo, ndio hela utakula ila mwsho wa siku utahitajika kulipa maana chuo kitatambua ujanja wako, sitoendelea kutoa maelezo ila hilo wekeni kichwani katika kipindi chote cha masomo yako.

wito wangu kwa viongozi wa vyuo na wanafunzi mnaoendelea na masomo, jitahidini kusaidia vijana hawa wadogo wasioelewa haraka matatizo ya chuo.

CHANCE NDOTO
 
Mkuu waliambiwa wanapoenda chuo watakutana na watu, viatu na makopo. Sasa wewe unataka wasikutane nao.

Na sisi tutakula wapi mkuu. Acha hizo bhana.
 
Hivi msomi kabisa ambaye amepita kooote Ndio afanye uzembe huo?

Huyo Ni kilaza
 
Back
Top Bottom