Wanafunzi wa Shule ya Kata wazichapa na wahuni wa Chafu 3, Polisi waingilia kati

ndo wapi huko?
 
chanzo cha ugomvi akina kichwa wala miguu katoto kanaenda kupasuka skull na upotevu wa meno ya mbele,
hapo baadhi ya wanafunzi walienda kwa ushawishi tu bila kufikiri hilo jambo lina maslahi gani kwake...
ujana plus utoto na ujinga
 
uyoo dogo mweusi kwenye kirikuu ndo katokea chafu 3???

amekaa kiteja ata kula sijui kama amekula hii week au amefunga????
 
Halafu mwalimu mimi nalaumiwa Kwa kufelisha??

Nifundishe ,niwalee,niwafunze nidhamu na sasa wananiongezea kazi mpya ya uaskari maana wamegeuka waarifu.

Ngoja niandae scheme of work ya term ijayo na niende gym niwe imara kwa vita hizi za wanafunzi.;

Mungu atanilipa tu mimi mwalimu wa Tanzania
 
Na huko ianzishwe kanda maalu maana majina yanasadifu Rorya tu
 
Kitu nilikuwa sifanyi shuleni ni kufuata mkumbo.

Sasa hapo ukifukuzwa shule unapoenda nyumbani na kuungana na wazazi kulima vinyungu huku wenzako wanaenda shule za private ndio akili inakaa sawa.
 
Wanaume wa Dar bhana. Wanafunzi wanapigana na wahalifu hata kuwasaidia ili watokomeze uporaji hamna.
Hata hao wahalifu ni wanaume wa Dar. Au ulidhani wahalifu ni wanaume wa mkoa? Tena mtuachie jiji letu. Wanaume wa mkoa hata kuoga hamuogi siku tatu eti kisingizio ni baridi
 
Hao wanafunzi lelemamaa hao...sisi enzi zetu tungewatandika hao wahuni,makondakta na yeyote yule ambaye angeingilia...
 
Wamepasuana hivi huku viroba vimepigwa marufuku!! nadhani vingekuepo wangeokota mzoga.Alafu hizi shule ndo maana zinashikaga mkia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…