beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mwanaghati iliyopo Ukonga Ilala Jijini Dar es Salaam (Kwa Wakurya) wameenda kufanya fujo ktk eneo moja linalofahamika kwa jina la Nyantila kufuati bifu lao la muda mrefu na kikundi kikorofi cha Chafu 3.
Chanzo cha bifu lao hakijajulikana bado, lakini inadaiwa uhasama wao ulifikia hatua ya kuwindana.
- Polisi wanawatafuta wote waliohusika katika fujo hizo.
--------------------------
Story nzima iko hivi;
--------------------------
Kuna mwanafunzi alinyan'ganywa simu na Kaka mkuu wa Mwanaghati. Huyo Mwanafunzi anaishi Nyantila. Huyo mwanafunzi akaenda kumleta Kaka yake ambaye yupo kwenye hilo group. Wakaenda Shuleni Mwanaghati na Mapanga na Visu. Wakafanya Fujo ila walizidiwa nguvu na Walimu wakawakamata. Wakawapeleka Serikali za Mitaa mwishowe wakawaachia baada ya kuomba msamaha.
Kule shuleni ilikuja kujulikana kwamba kweli Kaka mkuu kachukua simu. Shule imemfukuza huyo kaka Mkuu.
Leo shule ya Nyantila ilikuwa inafungwa. Kaka mkuu kaoganise wanafunzi wa Waende kuwapiga walokuja shule kama kulupiza kisasi.
Walipofika Nyantila wakaanza kupambana, Kuna dereva wa Daladala alienda kuamlia waache kupigana ndipo wakampiga jiwe kaamua paji la uso.
Wale Makonda wa Stand Nyantila Wakaanza kupambana na hao wanafunzi hadi wakakimbia. Katika kukimbia mmoja huyo kwenye picha akajificha kwenye nyumba wahuni wa chafu tatu wakamuona. Ndo kumpiga na kuumiza hajiwezi hawezi hata kuongea. Kafikishwa Hospital amezia sasa kawekewa drip. Baadhi ya Wahuni Washakamatwa. Wanafunzi wengi wameumia.
SIKILIZA MAELEZO KUTOKA KWA MASHUHUDA