Wanafunzi wa mwaka wa tatu St. Francis University College of Health wafukuzwa

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,205
15,162
Salaam wakuu,tujitwike madani.

Wanafunzi wote wa mwaka wa tatu (MD) katika chuo cha Saint Francis (chuo shirikishi cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT)) kilichopo Ifakara Morogoro wameachishwa masomo kwa kigezo cha utovu wa nidhamu yaliyoorodheshwa katika barua husika na kutakiwa kuondoka haraka iwezekanavyo. Iliyoambatanishwa ni barua iliyobandikwa notice board.
84921b196c13a33a6139845faa7606f8.jpg

Je,nini maoni yako juu ya hili?
 
Baadhi ya sababu za kuwa discontinued zimeorodheshwa wazi na siyo figisu, ikiwemo kukataa kufanya mtihani wa ENT na na nyingine zimeorodhoshwa hapo juu.

Kwa tafsiri iliyo nyepesi ni kwamba kama upo shuleni na hutaki kufanya mitihani then unategemea uchukuliwe hatua gani zaidi ya kurudishwa kwenu mkafanye mnayotaka nyie na haya ni madhara ya kuingiza siasa mashuleni.

Haya rudini kwa wazazi wenu.
 
Mkuu tusiwahukumu kwa ujumla bila kuapata maoni yao ambayo siyo rahisi kuorodheshwa kwenye barua tajwa.
Pia,sikuona sababu ya kuamriwa kuondoka chuoni kwa muda wa haraka kiasi hicho bila kupewa muda wa kutosha kujikusanya na kuondoka
 
Ukishapoteza sifa ya utambulisho you no longer belonged to that ground mkuu, those measures taken are totally fair. Msicheze na shule vijana wangu
 
Ukishapoteza sifa ya utambulisho you no longer belonged to that ground mkuu, those measures taken are totally fair. Msicheze na shule vijana wangu
Sawa Mkuu wangu chakii lakini sijapenda walivyowageneralize wote naamini hakukosekana wanafunzi wenye nidhamu na nia njema na maisha yao lakini kwa sababu ya watu wachache Kati yao,imewasababishia maumivu.
 
Yani watu wanashabikia kirahisi rahisi tu tena bila ya kutoa hoja. Nilidhani kuna mmoja wapo ambaye anatarifa sahihi juu ya nini kilitokea kumbe hakuna ila kwakuwa tu kuna mtu mwanzo aliunga mkono basi wengi wakafuata mkondo huo huo.
Nakiri sijui chochote kuhusu hilo tukio.lakini sishawishiki kuamini kuwa wanafunzi walikuwa vichaa na kutotii taratibu husika. Vyuo vikuu bongo vimekuwa haviwajibiki vizuri na ndio maana migomo ilikuwa ndio njia.pekee yakuleta mabadiliko hayo. Miaka ya 2006 hadi na tisa kulikuwa na migomo kadhaa UDSM. Licha ya kuwa kulikuwa na kufukuzwa kwa wachache.ila ukweli ni kuwa wengi walofuata walifaidi jasho la watangulizi wao.
Tujaribu kudadisi kwanza kuwa walikuwa wakitaka nini na walitumia njia gani kwa muda gani na walikuwa wakijibiwa nini. Baada ya hapo ndipo tunaweza sema kuwa ni sawa au sio sawa kwa wao kufukuzwa.
 
Baadhi ya sababu za kuwa discontinued zimeorodheshwa wazi na siyo figisu, ikiwemo kukataa kufanya mtihani wa ENT na na nyingine zimeorodhoshwa hapo juu.

Kwa tafsiri iliyo nyepesi ni kwamba kama upo shuleni na hutaki kufanya mitihani then unategemea uchukuliwe hatua gani zaidi ya kurudishwa kwenu mkafanye mnayotaka nyie na haya ni madhara ya kuingiza siasa mashuleni.

Haya rudini kwa wazazi wenu.
Sababu ya kufanya hivyo ni nini maana huo ni upande mmoja umetoa sababu zake kwa aliyesoma SAUT atakuwa anajua ubabe wao na uonevu.
 
Back
Top Bottom