Wanafunzi wa kiislam na Haki ya Kuabudu

Intellect

Member
Apr 1, 2011
34
20
Ninasikitishwa sana na wanafunzi wa leo katika taasisi za elimu ya juu kutokana na kuharibu taswira iliyokuwepo juu ya mwanafunzi kama balozi wa wananchi ambao hawana taasisi inayosimamia matatizo yao kikamilifu, hii inajidhihirisha katika matukio ya wanafunzi kuanzisha migomo ambapo mingi inalenga maslahi yao binafsi na sio maslahi ya taifa kwa ujumla. Katika maswala ya msingi kama vile ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za uma nk. wanafunzi wamekua wagumu kuwasilisha hisia za wananchi hata kwa kugoma, ila pesa za mkopo zikicheleweshwa utauona moto wake!
​
Hivi karibuni wanafunzi wa kiislam waligoma kwa kile walichodai haki ya kuabudu, hii ilitokana na kufukuzwa kwa wanafunzi wa shule ya Ndanda kwa kushinikiza ujenzi wa msikiti katika eneo la shule ambapo pia kuna kanisa. Nilidhani wanafunzi hao walipaswa kujua kama haki nyingi katika "Bill of Rights" ndani ya katiba yetu ikiwamo haki ya kuabudu haziko "exclusive" kwamba serikali hailazimiki kuzisimamia katika baadhi ya mazingira. Ikumbukwe kwamba nchi yetu haina dini kwa mujibu wa katiba sambamba na hilo ikumbukwe kuwa shule ya Ndanda ilikua mali ya kanisa katoliki kabla ya uhuru, na ni kwa jitihada za Mwl. Nyerere shule hii na nyingine nyingi zilitaifishwa pamoja na makanisa ndani yake ili kuwapa fursa hata watoto wasio wakristu kupata elimu! Sasa sioni tija ya wanafinzi hawa wa kiislam kuishurutisha serikali kujenga msikiti hapo shuleni ikiwa hata kanisa halikujengwa na serikali!

Ninawashauri wanafunzi hawa wazishurutishe taasisi za dini yao kujenga nyumba ya ibada karibu na shule na ikiwa serikali itatia ngumu hapo wanaweza kugoma kwa mujibu wa sheria!

Mwisho, nadhani wakati umefika kwa wanafunzi kuanza kugomea mambo ya msingi yanayo wagusa wananchi kwa ujumla!
 
kwani wakijengewa msikiti/wakijenga msikiti karibu na shule ni kosa? mbona shule znyingi za serikali zilizokuwa za dini zina misikiti ndani au karibu na shule? i dont see any problems here for them to have labda kama kuna behind the window reasons lakini nina uhakika headmaster hawezi kufukuza wanafunzi kisa wameomba kujengewa nyumba ya ibada kutakuwa na reason nyingine ambayo hawa wanafunzi watakuwa wamefanya
 
Duuuh nilidhani wanagoma hakuna walimu au hawafundishwi kumbe ishu ni hiyo hakika ziro zinawasubiri kwenye mitihani!!
 
kwani wakijengewa msikiti/wakijenga msikiti karibu na shule ni kosa? mbona shule znyingi za serikali zilizokuwa za dini zina misikiti ndani au karibu na shule? i dont see any problems here for them to have labda kama kuna behind the window reasons lakini nina uhakika headmaster hawezi kufukuza wanafunzi kisa wameomba kujengewa nyumba ya ibada kutakuwa na reason nyingine ambayo hawa wanafunzi watakuwa wamefanya

Mkuu SI,
Sijakupata vema, wanafunzi wajengewe msikiti na Serikali au vipi? Na zile shule za kata zisizokuwa na Makanisa/Misikiti Serikali itenge bajeti kujenga, right?
 
Hivi siku ni sahihi serikali ijihusishe na ujenzi wa nyumba za ibada kwenye shule zake? Aaaaaaaaaaa jamani, sasa serikali itakuwa na dini?
 
Ninasikitishwa sana na wanafunzi wa leo katika taasisi za elimu ya juu kutokana na kuharibu taswira iliyokuwepo juu ya mwanafunzi kama balozi wa wananchi ambao hawana taasisi inayosimamia matatizo yao kikamilifu, hii inajidhihirisha katika matukio ya wanafunzi kuanzisha migomo ambapo mingi inalenga maslahi yao binafsi na sio maslahi ya taifa kwa ujumla. Katika maswala ya msingi kama vile ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za uma nk. wanafunzi wamekua wagumu kuwasilisha hisia za wananchi hata kwa kugoma, ila pesa za mkopo zikicheleweshwa utauona moto wake!
​
Hivi karibuni wanafunzi wa kiislam waligoma kwa kile walichodai haki ya kuabudu, hii ilitokana na kufukuzwa kwa wanafunzi wa shule ya Ndanda kwa kushinikiza ujenzi wa msikiti katika eneo la shule ambapo pia kuna kanisa. Nilidhani wanafunzi hao walipaswa kujua kama haki nyingi katika "Bill of Rights" ndani ya katiba yetu ikiwamo haki ya kuabudu haziko "exclusive" kwamba serikali hailazimiki kuzisimamia katika baadhi ya mazingira. Ikumbukwe kwamba nchi yetu haina dini kwa mujibu wa katiba sambamba na hilo ikumbukwe kuwa shule ya Ndanda ilikua mali ya kanisa katoliki kabla ya uhuru, na ni kwa jitihada za Mwl. Nyerere shule hii na nyingine nyingi zilitaifishwa pamoja na makanisa ndani yake ili kuwapa fursa hata watoto wasio wakristu kupata elimu! Sasa sioni tija ya wanafinzi hawa wa kiislam kuishurutisha serikali kujenga msikiti hapo shuleni ikiwa hata kanisa halikujengwa na serikali!

Ninawashauri wanafunzi hawa wazishurutishe taasisi za dini yao kujenga nyumba ya ibada karibu na shule na ikiwa serikali itatia ngumu hapo wanaweza kugoma kwa mujibu wa sheria!

Mwisho, nadhani wakati umefika kwa wanafunzi kuanza kugomea mambo ya msingi yanayo wagusa wananchi kwa ujumla!

Hapo inabidi yale maspika yapangiwe muda wa kupiga kelele ama sivyo concentration itakuwa zero...! Ila hata wakipangiwa muda wa kupiga kelele watalalamika wanaonewa!
 
Mkuu SI,
Sijakupata vema, wanafunzi wajengewe msikiti na Serikali au vipi? Na zile shule za kata zisizokuwa na Makanisa/Misikiti Serikali itenge bajeti kujenga, right?

wajenge wenyewe.hakuna wa kuwajengea .serikali inajengaga nyumba za ibada? wamuombe hata lowasa
 
hela wazitoe wapi?hilo ni jukumu la serikali inatakiwa ibalance!kwavile lipo kanisa na msikiti lazima uwepo.kila mmoja awe na uhuru wa kuabudu.....!
 
Hivi siku ni sahihi serikali ijihusishe na ujenzi wa nyumba za ibada kwenye shule zake? Aaaaaaaaaaa jamani, sasa serikali itakuwa na dini?

ni sahihi kabisaa,kwani kikwete akiingia kanisani inamaanisha serikali dini yake ni ukristo?kujenga nyumba za ibada na udini wa serikali ni vitu viwili tofauti.and this is the truth!
 
makanisa yamejengwa na serikali?
 
Anajidai kama vile haijui MoU.
Naungana na mtoa mada hapo juu kuwa adui yenu hamjamjua bado... Maana wewe kwako adui wa muislamu ni MoU, na kuna mmoja humu kasema kanisa la ndanda livunjwe, kwa hiyo kwake kanisa likivunjwa basi adui atakuwa kafa. Nina uhakika wakifanyiwa interview waislamu 20 katika kutafuta jibu la nani adui wa uislamu, majibu utayashangaa
 
Hapa tatizo sio misikiti maana mwanafunzi thabiti anajua shule ameenda kusoma hayo ya kanisa na msikiti ni majaaliwa, wazazi tuapowapeleka watoto shule tunaangalia kama shule inafundisha na malazi yapo sawa.
Kama tunaandamana kisa hamna msikiti au kanisa shuleni inabidi tuulizane na kama hiyo elimu wanayopewa inawasaidia kupambana na changamoto za kwenye jamii yao
.:juggle::A S embarassed:
 
Back
Top Bottom