amba.nkya
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 446
- 131
Siku kadhaa zilizopita nilibahatika kumsikia Waziri mwenye dhamana na Elimu ya juu, Prof. Maghembe akitamka kupitia vyombo vya habari. Miongoni mwa mambo aliyotamka ni pamoja na kuwa "wanafunzi wa elimu ya juu wamefunga vyuo na hawaruhusiwi kurudi vyuoni hadi muda wa likizo utakapoisha, hivyo hawatashiriki kupiga kura kwenye vituo walivyojiandikisha wakiwa vyuoni". Pia Waziri huyo alibainisha kuwa "wanavyuo hao hawapaswi kujihusisha na siasa kwani jukumu lao ni kusoma tu".
My Take:
Kama serikali iliona wanavyuo hao hawastahili kupiga kura, kwanini waliruhusiwa kujiandikisha vyuoni? Aidha, serikali haioni kuwa imevunja Katiba kwa kuwanyima wanafunzi hao haki yao ya msingi ya kushikiriki kupiga kura 31.10.10? Nachelea kusema kwamba huu ni woga wa CCM kwani wana hofu kuwa wanafunzi wengi wataipa kura CHADEMA.