Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Iringa watokwa na mapovu kwenye orientation

VendoPatrick

Member
Jun 12, 2016
15
45
Habarini ndugu zangu wana JF,

Leo nilikuwa pale OUT branch ya Iringa nikihudhuria orientation course. Ndugu zanguni wanafunzi wengi wameingiwa na hofu kubwa juu ya hatma yao kuhusu msimamo wa Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako wa kufuta foundation course na kutimua wale wote waliokwenye system na degree zao walizozipata kwa njia hiyo.

Mmoja wa wanafunzi alimwomba director wa OUT - Iringa awahakikishie kabla hajaamua kuacha masomo. Muda mwingine walimu watoa semina walikaribisha maswali yahusuyo mada inayotolewa, lakini wanafunzi wakawa wanauliza tu juu ya hatma yao na tamko la waziri wa elimu. Hakika kwa mtizamo wangu wanafunzi wamekata tamaa na mapovu yanawatoka balaa! Sidhani kama mada za walimu kama Dr Chachage zilieleweka vizuri.

Karibu kwa mchango na maoni kwa wanafunzi hawa. Ahsante.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom