Wanafunzi wa chuo cha Mkwawa wafunga barabara huko Iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wa chuo cha Mkwawa wafunga barabara huko Iringa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gumzo, Apr 24, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanafunzi wa chuo cha elimu Mkwawa Iringa hivi sasa wameziba barabara kuu ya Iringa -Pawaga barabara inayosimamiwa na wakala wa barabara mkoa wa Iringa (TANROADs) wakishinikiza kuwekwa matuta katika eneo la lango kuu la chuo hicho cha Mkwawa kutokana na ajali za mara kwa mara . Wanafunzi hao zaidi ya 200 wameziba barabara hiyo eneo la Kuingia chuoni huku wakimtaka diwani wa kata hiyo ya Mkwawa Thobias Kikula .a.k.a MC Kikulacho kushirikiana nao kuibomoa barabara hiyo ili kuweka matuta kuanzia sasa.

  Wakizungumza kwa jazba mbele ya diwani huyo wanafunzi hao wamesema kuwa wamelazimika kuziba barabara hiyo baada ya kuwepo kwa matukio ya mara kwa mara kwa wanafunzi wanaovuka barabara hiyo kugongwa kutokana na madereva kuendesha magari yao kwa mwendo mkali zaidi. Hivyo kutokana na ajali hizo wamemtaka diwani huyo kuungana nao katika kuchimba barabara hiyo ya lami ili kuweka matuta kuanzia sasa zoezi ambalo limekuwa gumu kwa diwani Kikulacho kuungana kulitekeleza.
   
 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  wana haki maana maisha ni muhimu sna kuliko chochote lakini kama wanaweka barabara bila kuangalia usalaama wa watu nini kifanyike? kwa hilo nawapongeza sna ili waziri mwenye dhamana aelewe kuna binadamu wanaohitaji kulindwa kwa kila hali
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hizi habari za kulala barabarani ili kushinikiza matuta ni ushahidi tu kwamba vyombo vyetu vya kulinda sheria havifanyi kazi yake ipasavyo. Kuna alama za barabarani ambazo inabidi zifuatwe lakini rushwa inasabisha sheria kuvunjwa na kuendelea kivunjwa kila kukicha. Kuweka matuta barabarani ni kuharibu barabara suluhu ni madereva kufuata sheria na alama a barabarani.
   
 4. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Komaeni na diwani apeleke habari zenu halmashauri,wao watambana meneja wa tanroads mkoa.km barabara ni bora kuliko usalama wa raia itafahamika.
   
 5. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nimeshuhudia magari yakipita kwa spidi ya ajabu sana pale na kila mara huwa najiuliza, "hivi hawa wananchi watembea kwa miguu hawana haki hata kidogo ya kutumia barabara? Nashukuru sana wanachuo kwa kuwa na ujasiri wa kufunga barabara na kuchukua sururu na kuchimba na kuondoa lami na kuweka mawe. Ni dharau kubwa sana kwa dereva kuendesha gari spidi ya 80 hadi 100 katika eneo la makutano ya geti la chuo na barabara kuu, huku wakijua kuwa kuna wapita njia hapo.

  Nisingeshangaa kama hao wanaojiita viongozi wa serikali wakiambulia kichapo, na bahati yao walishtuka na kutokomea maana wangekumbana na nguvu ya umma
   
 6. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Pole, hapo ndio panaitwa Makanyagio? longtime nilipita njia hiyo ya kwenda pawaga, na inamaana kuna lami sas?
   
 7. k

  kalakata Member

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka iringa sasa ni moja kati ya mikoa inayoendelea kwa kasi sana! Hata vile viwanja vya makanyagio vya laki huwezi kupata sasa ni mil 3 mpaka 7 so na rami wameweka sehemu nyingi sana!
   
 8. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  MC Kikulacho ni DIWANI siku hizi?
   
 9. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa chama cha magamba lazima namfanisha na mobimba wa mtera rafiki yake lusinde........ah ah ah...ppz.........pw.
   
Loading...