Wanafunzi wa ADVANCE 107 wakiume kufukuzwa shule..

mosescharles

Member
Sep 11, 2018
5
1
Tarehe 25/08/2018..wanafunz wa kiume wa ADVANCE wote katika shule ya Sekondari DAREDA Babati Manyara.. Walifukuzwa shule kwa sababu ya kudai kuwa waligoma au waliendesha mgomo siku iyo ya sikukuuu ya Eid El Hajj ambapo walidaiwa kuingia darasan kama siku nyingine na kuwaacha waislam na sikukuuu yao..

Lakin baada ya kudai kuongea na mkuu wa shule hiyo aliwaijia juu na kutaka kuwapiga kwa kuita walimu wote na kuagiza vboko vya kutosha.. Ndipo walipoamua kukimbia na kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa manyara.. Na Kuna wengine tisa ambao ilidaiwa kuwa viongozi wa mgomo huo wako kweny hatihati ya kufukuzwa shule..

Sasa sijui njia gan ilitumika kuwajadili wanafunzi hao kama viongozi
 
Ingependeza zaidi uje na ID yako ya zamani
Poleni sana dogo langu alisoma hapo
 
Mleta mada twende taratibu. Kwanza umesema wahusika waliingia darasani siku ya Idd. Pili, ukasema walitakiwa kuchapwa viboko wakakimbia kwenda Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara ambaye ni Ndugu Mnyeti. Tatu, unasema tisa wanaweza kufukuzwa shule. Nne, kichwa cha habari kinasema waliofukuzwa ni 107. Sasa, ni wangapi hasa waliogoma na kufukuzwa? Je, kuingia darasani siku ya sikukuu ni mgomo? Je, walipokimbilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, nini kilitokea au kuamriwa? Hebu fafanua hayo kwanza
 
Niliwaona siku ya mgomo na niliongea nao baadh nikapewa data hizi.. Kwaiyo sielew na ivi kesh kuna kikao cha wazaz na walimu.. Kuhusu ili
 
DAREDA! DAREDA! DAREDA! Hii shule naifahamu sana kwani nimepiga A-level hapo. Hii shule ina changamoto za kiuongozi kwani haiwezekani kila mwaka kuwe na mgomo. Mwaka wetu mgomo ulifanyika ambapo wanafunzi "wa A-level" waligoma kula kwa saa 48 hadi mkuu wa shule alipokuja kuwasikiliza. Hata hivyo kuja kwake hakukuzaa matunda kwani alikuja na moto kuliko nyenzo ya kumaliza mgomo. Hitaji la wanafunzi lilikuwa kuzungumza na OFISA ELIMU na kweli lilifanyika. Changamoto zilizoko pale kwa kutumia uzoefu wangu wa miaka miwili niliyokaa pale ni
1. Uelewano hafifu kati ya wanafunzi wa advance na walimu wanaofundisha O-level. Ikumbukwe kuwa shule hii ina form 1-6 sasa walimu wanaofundisha 1-4 hawana ukaribu na wanafunzi wa 5&6.
2. Walimu wa advance hawana mahusiano mema na walimu wanaofundisha o-level japo wote ni wa shule moja na wanafundisha shule moja.
3. Changamoto za masomo ya sayansi hasa ndiyo huwa msingi wa mgogoro. Pale kuna maabara zote tatu lakini wawezeshaji ndiyo hakuna. Muda wote CBG hufundishwa nadharia kwa masomo ya sayansi lakini vitendo hufundioshwa miezi mitatu ya mwisho kuelekea kuhitimu shule. Hta walimu waliopo ili kufundisha nadharia hasa kwa Chemistry anaparaza tu. Wanafunzi wakihoji huonekana kutokuwa na nidhamu.
4.Wavulana wa advance wanatuhumiwa kujitafunia mabinti wa o-level tena ukizingatia jamii ya hapo (Wairaqw ni mama huruma basi ndo huwa kipozeo cha vijana.)
Kwa miaka niliyokaa shule ile kumetokea migomo mikuu mitatu na yote huhusisha wavulana wa advance.Migomo yote hiyo ilipelekea wengi kufukuzwa jumla. HP ni miongoni mwa waliofukuzwa jumla. Ilipelekea walimu waliokuwa wanachukiwa kupigwa siku walipoingia bweni la wavulana.
Baada ya mgomo huo mkuu wa shule alihamishiwa shule moja iko MAGUGU, wale walimu waliosemekana wanaparaza darasani waliondolewa shuleni hapo na akaletwa mkuu wa shule mwingine kutoka Qameyu.
Sasanajiuliza kama shida ilikuwa wanafunzi hao enzi hizo, walishamaliza. Kma shida ilikuwa uongozi wa juu nao ulisambaratishwa kwani mkuu wa shule alihamishwa. Lakini je, kwanini baada ya miaka mitatu tena tangu mgomo ufanyike mbona umeibuka tena ingawa shule iko na uongozi mpya? Hapo inabidi kutazama kwa jicho la ziada hasa mahusiano kati ya wanafunzi wa o-level, walimu wa o-level, walimu wa advance na wanafunzi wa advance.
Kwa kawaida wanafunzi hugoma pindi mambo yanapozidi kipimo na wao huamua kutafuta sababu dhaifu ili kumwaga yote hadharani. Hii ilitumika hata mwaka wetu kwani mgomo ulilipuka baada ya kuzuiwa kutumia vyombo vya plastiki na mifupa. Zuio lilitolewa asubuhi eti utekelezaji uwe mchana ambapo kila mwanafunzi alitakiwa kutwa na chombo cha bati/ chuma.
All in all DAREDA imenijenga na sasa nimehitimu shahada yangu.
 
Wagome tu..........wakifika na chuo waongeze bidii na machuoni huko kwa watakao fanikiwa kwenda ila bila shaka hao watakuwa wamechukua masomo ya sanaa...mana PCM PCB unapta wap mawazo ya kugoma kwa mambo yalivyo heavy
 
Ulimbukeni wa kuwa A level na kuanzavkuonesha dharau kwa walimu wa o level. Hao mwanafunzi walifika aje A level bila ya kupita o level?
 
Mm nimmojawapo wa waanzilishi wa A-level hapo dareda enzi zetu tulifaidi sana kuwalamba visimi hao wairaq
Ila changamoto zilikuwa nyingi sana hapo tulikaa mwaka mzima bila kula wali tuliishia kula ugali mkibadl ni kande kwa kisingizio cha shule kusahaulika kwenye budget
Uzuri tulikuwa tunasahihisha mitihan ya daeasa la 4 na kujipatia vijisenti
 
Umenikumbusha. Tulipewa kazi ya kusahihisha BRN darasa la saba tukajipatia vijisenti vya kumsumbua boss ( yule mpishi mkuu na mandazi yake ha ha ha ha )
 
Back
Top Bottom