Fair player yes but you dont practise fair play to UDSM students. Mzee hujapita hapo juu nini? Ufisadi ndio uko hivyo, it seems umeshakucorrupt na wewe. Tunahitaji mapinduzi ya nchi nzima, sasa lazima yaanzie kwenye grass root level. UDSM students wanahitaji support. Alaa, hujui demokrasia nini?Hawa wanafunzi wanafikiria migomo migomo tuuuuuuuu. Someni nyie watoto sisi tunawalipia masomo yenu alaaah!!
Samahani wanaJF leo nitapingana na madai ya UDSM. Uzuri ninauzoefu mkubwa juu ya wanafunzi wa vyuo vya bongo na serikari zao kwakuwa nimeshiriki kikamilifu. Tukiacha matatizo madogomadogo, wanafunzi wa vyuo vikuu bongo ni very complex individuals.
Hapa wanalalamika kutopewa uhuru wa kuchagua viongozi wao. Lakini report hii pia inasema walipewa nafasi ya kuchagua viongozi wao kwa njia ya mtandao. Kimsingi njia hii ndio inayotumika vyuo vya ulaya nafikiri hii ndio njia inayopaswa kutumika vyuo vyote bongo kwani ni cost effective in terms of both time and money.
Swala la kuhoji uhalali wa Chuo kufuta Daruso, nadhani wanatakiwa kutambua kuwa Daruso ilikuwa enacted kutoka kwenye Prospectus ya Chuo. Hivyo kwa namna yoyote ipo chini ya chuo na chuo kinamamlaka ya kuintervene baadhi ya mambo. Kimsingi ni kama taasisi yoyote ya serikari, ndio maana Daruso ipo intitled kupata ruzuku Chuoni.
Ujumbe wangu kwa wanafunzi wa UDSM, kuna mambo ambayo ni haki ya mwanafunzi mfano conducive learning environment i.e. adequate lecture theaters & lecturers, class facilities, computers and internet access and full furnished libraries among others. Hivi ni vitu ambavyo wanaweza negociate na ikibidi kuandamana ili vipatikane. But kuna issues kama exams regulations, bylaws, accommodation, transport, etc. Haya si majukumu ya msingi ya chuo japo chuo kinaweza facilitate hivyo hawapaswi kugomea.Hali kadhalika uongozi wa wanafunzi ni mpango wa chuo kuweza kuwasiliana kirahisi na wanafunzi na kushirikisha wadau wake (wanafunzi) katika baadhi ya maamuzi. Hivyo chuo kinaweza amualolote juu ya DARUSO. Mbona vyuo vya ulaya wanafunzi hawagomigomi kama bongo kunanini hapo???
Wana JF naomba nitumie fursa hii kuwasalimu wote, naamini kuwa afya zenu ni nzuri na mnaendelea kuchapa kazi kama kawaida kila mmoja katika nafasi yake.Nimeanza na salamu kwa kuwa ni muda mrefu kidogo sijaonekana kwenye hili jukwaa letu.
Mkuu pamoja na kutufahamisha kwamba una uzoefu na serikali za wanafunzi vyuo vikuu vya bongo, kama huo mtazamo wako ndiyo uelewa wako ulivyo, basi hukustahili kuwa kiongozi wa wanafunzi, huenda ulikuwa mamluki. Ushahidi upo wa kutosha kuwa baadhi ya watu wanagombea uongozi vyuoni kutafuta maslahi binafsi na si kuwakilisha maslahi ya wanafunzi.Kuwepo chuo cha elimu ya juu hakuishii kwenye kuingia darasani kukariri 'theories' mbalimbali na kusubiri mitihani. Chuoni ni mahali pa watu kukuza vipaji vyao, vya kisiasa, kiuongozi, kitaaluma, kimichezo, kiutamaduni, n.k, n.k
Na ili uweze kuonyesha kipaji chako ni lazima upewe nafasi ya kufanya hivyo.Kinyume chake ni kutaka kuvigeuza vyuo vikuu viwe sawa na shule za msingi au sekondari, maana kule ndipo watu wanaamrishwa kama vile wako jela.Nakumbuka nilipokuwa sekondari pale Moshi tech. uongozi wa shule ulikuwa unakaa kutathmini na kupendekeza majina ya wanafunzi wanaofaa kuwa viongozi, then yanapelekwa kwa wanafunzi kwa ajili ya kupigiwa kura, utaona kuwa walimu wale waliona umuhimu wa wanafunzi kuchagua viongozi wanaowataka. Kwa kiwango cha chuo kikuu wanafunzi wenyewe wanao uwezo wa kuunda kamati za kuwatathmini wanafunzi wenzao wanaoomba kuchaguliwa kuwaongoza, na hili limekuwa likifanyika miaka nenda rudi.Hili suala la mikopo lisiwafanye watu mkasahau mambo ambayo ni haki ya wanafunzi na wana uwezo wa kuyatekeleza bila matatizo.Uongozi unaowekwa na menejimenti ya chuo unatekeleza matakwa ya menejimenti na hauwezi kutetea maslahi ya wanafunzi.Na ndio maana uongozi wa chuo hauwezi kuwachagulia wafanyakazi wa chuo viongozi wa vyama vyao kama vile RAAWU, UDASA, n.k, hilo ni jukumu na haki ya wafanyakazi au wanataaluma wenyewe.Na hata kwenye senate kunakuwa na uwakilishi wa pande zote yaani wanafunzi, wanfanyakazi/wanataaluma na serikali kwa maana ya wizara.Hivi tujiulize kama tunahubiri ushirikishwaji wa wanachi katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo hadi huko nyanchabakenye kwa wavuvi na wakulima,kwamba wanatakiwa washirikishwe, yaani hatuoni umuhimu wa wasomi kuipata hiyo haki ya kushirikishwa?Kwakuwa kuna mambo mengi tu ya kipuuzi na kimabavu yanayofanywa na menejimenti za vyuo na hawapendi kuulizwa ulizwa au kubughudhiwa wanaona ili kuondoa usumbufu wa kufuatiliwa matendo yao maovu ni kuivunjilia mbali na daruso kisha wateue watu wao.Na kitu kibaya zaidi haki za wanafunzi zinaminy sana vyuoni kama hakuna strong leadership, wengine hudiriki kuwarubuni na hata kuwahonga viongozi wa wanafunzi.
Hata hivyo tujiulize maswali machache kama kweli walipewa nafasi ya kupiga kura online, je miundombinu inatosheleza?na hao waliotakiwa kupigiwa kura ili wawe viongozi ni nani aliyewateua au kuwapitisha kugombea?ni utaratibu gani ulitumika kuwapata wagombea?
Nimalizie kwa kuwasihi wadau wenzangu, tujaribu kufanya utafiti wa kina kuhusu maisha ya vyuo vikuu tanzania kwa sasahivi hususani mlimani, inawezekana wengine mna uzoefu wa miaka ya 80-90 ambako mambo yalikuwa mswano, sasahivi udsm inaendeshwa kisiasa,tena siasa chafu, siasa za mabavu, pale udsm kuna maprofesa wa deokrasia/utawala/uongozi lakini hawajui kutumia taaluma zao kwa maslahi ya umma badala yake wameweka mbele ubinafsi.
Nimeyasema hayo kwa kuwa nina uzoefu wa kutosha katika siasa za vyuo vya elimu ya juu nchini mwetu na nimeshiriki kiasi kikubwa katika harakati za kutetea maslahi ya wanafunzi wa elimu ya juu. Sisemi hivyo kwa kutafuta sifa au kujikweza lakini ukweli ni kuwa nilipata kuwa Raisi wa serikali ya wanafunzi katika moja wapo ya vyuo vya elimu ya juu hapa nchini nikiwa mmoja wa waanzilishi wa TAHLISO tukahangaika hadi ikapata usajili pamoja na mizengwe mingi sana tuliyokutana nayo, ingawa nasikitika kwamba sasahivi taasisi hii inaonekana imepoteza muelekeo.Na kwa nafasi yangu nimeweza kujifunza mambo mengi sana ambayo watu wengine ambao hawajishughulishi kutaka kujua mambo kwa undani huishia kuwalaumu wanafunzi tuu.Kama kuna mtu anaikumbuka ile tume ya mama sinare(mwanasheria) iliyoundwa na dr.Ng'wandu kati ya 2003-2004 ilitoa ripoti ya uchunguzi wake kuhusu matatizo ya vyuo vya elimu ya juu vya umma nchini,alikuwemo muhingo rweyemamu akiwakilisha kundi la wanafunzi, wakati huo akisoma tumaini iringa na akiandikia gazeti la mwananchi.Ripoti yao ilitolewa hadi kwenye magazeti aliyeisoma anajua kilichopendekezwa lakini wizara ya elimu ya juu inafanya mambo mengine kabisa na yale mapendekezo yako kwenye makabati ya mama naomi katunzi na maghembe pale wizarani.
Nawasilisha.
Ndotomtaa;
Mwaka wa kwanza nilikuwa Hall Six wa pili Hall 5 wa tatu Hall 6. Revolution square nineenda sana, Kupigwa virungu nilipigwa mara 2. Mara ya 3 nikakataa kwenda kwenye mgomo. Hiyo ilikuwa ni mwaka wa mwisho!
Katika masuala matano wanayodai unakuta mawili ndo ya maana.
Na dhana kuwa kila anayepinga migomo hajapitia channel hiyo ya usomi IFUTE Kabisa.
Asante
Samahani wanaJF leo nitapingana na madai ya UDSM. Uzuri ninauzoefu mkubwa juu ya wanafunzi wa vyuo vya bongo na serikari zao kwakuwa nimeshiriki kikamilifu. Tukiacha matatizo madogomadogo, wanafunzi wa vyuo vikuu bongo ni very complex individuals.
Hapa wanalalamika kutopewa uhuru wa kuchagua viongozi wao. Lakini report hii pia inasema walipewa nafasi ya kuchagua viongozi wao kwa njia ya mtandao. Kimsingi njia hii ndio inayotumika vyuo vya ulaya nafikiri hii ndio njia inayopaswa kutumika vyuo vyote bongo kwani ni cost effective in terms of both time and money.
Swala la kuhoji uhalali wa Chuo kufuta Daruso, nadhani wanatakiwa kutambua kuwa Daruso ilikuwa enacted kutoka kwenye Prospectus ya Chuo. Hivyo kwa namna yoyote ipo chini ya chuo na chuo kinamamlaka ya kuintervene baadhi ya mambo. Kimsingi ni kama taasisi yoyote ya serikari, ndio maana Daruso ipo intitled kupata ruzuku Chuoni.
Ujumbe wangu kwa wanafunzi wa UDSM, kuna mambo ambayo ni haki ya mwanafunzi mfano conducive learning environment i.e. adequate lecture theaters & lecturers, class facilities, computers and internet access and full furnished libraries among others. Hivi ni vitu ambavyo wanaweza negociate na ikibidi kuandamana ili vipatikane. But kuna issues kama exams regulations, bylaws, accommodation, transport, etc. Haya si majukumu ya msingi ya chuo japo chuo kinaweza facilitate hivyo hawapaswi kugomea.Hali kadhalika uongozi wa wanafunzi ni mpango wa chuo kuweza kuwasiliana kirahisi na wanafunzi na kushirikisha wadau wake (wanafunzi) katika baadhi ya maamuzi. Hivyo chuo kinaweza amualolote juu ya DARUSO. Mbona vyuo vya ulaya wanafunzi hawagomigomi kama bongo kunanini hapo???
DARUSO ilifutwa.
Imerudi lini?
Mkuu,Mkuu Mwita sitaki tulumbane sana hapa swala la msingi ni kuwa hoja iliyopo imetolewa na mtau UDSM na haijaonyesha tatizo la miundombinu kama ni sababu ya kugomea uchaguzi. Kimsingi hoja yako haina tofauti na wanafunzi waliokwenye mgomo kwani upeo wao wakuchuja hoja huwa nimdogo wakati wa mgomo nahujikuta wakitamka mambo hata yasioyamsingi. Kasome vizuri hoja ya mdau then review comment yako.