Wanafunzi Sekondari ya Kibamba wafukuzwa kwa kukosa ada

Kachelenga

Member
Sep 11, 2012
26
6
Wakati Serikali ya CCM ikiamini hakuna mwanafunzi wa shule zake atakaefukuzwa shule kwa kukosa,Leo tarehe 14/09/2015 walimu wa shule ya Sekondary Kibamba wanapingana na Serikali ya CCM kwa kuwafukuza shule wanafunzi na kuwatandika viboko.

Inasemekana walimu wote waliokuwepo Staff room kila mwalimu alimchapa kila mwanafunzi bakora 2,tujiulize hao walimu walikuwa wangapi?Pamoja na kuwafukuza shule hao wanafunzi na kuwachapa bakora zisizo na idadi pia walimu hao walitoa maneno ya kashfa kwa wanafunzi hao.
 
INASEMEKANA... weka accurate facts tukuelewe... (kuhusu hicho kipengele cha fimbo)...
*pia rekebisha kauli yako.. hawajafukuzwa shule ila wamerudishwa nyumbani wakaombe pesa ya ada kwa wazazi na walezi...
***shughuli nyingi za uendeshaji wa shule hutegemea hiyo michango ya ada na mingineyo.. (
 
Kuna shule yangu nlosoma hapa ya kata.....wazazi wenyewe waliridhia kwamba watoto wao wakikosa ada warudishwe nyumbani.....hivi ni sahihi??
 
Waalimu wako frustrated, hawako properly trained, wanadhani matusi na adhabu kwa wanafunzi ndiyo italeta ufanisi wa malengo yao na kuondoa frustrations zao.

Ccm inaposema wanafunzi wasilipe ada, ni dhahiri haiko coordinated. Haina hata ufahamu kwa nini wanafunzi wanalipa ada na hizo ada ni kwa ajili ya financial gapes zipi ambazo shule zinahitaji kuziba.

Sserikali makin iilitakiwa kufanya upembuzi maridadi, ili inapotoa kauli kwamba kuanzia sasa hakuna mtoto kufukuzwa shule ajili ya ada, tayari imeshahakikisha imetatua hitaji la ada kwa shule. Ama kubadilisha mazingira na mfumo wa elimu pasiwe na haja ya hiyo ada au kuhakikisha subsidies za kutosha mahitaji yote ya shule bila ada za wanafunzi.

Ni fursa nyingine kwa wanafunzi na walimu kuifahamu serikali ya ccm na ccm kuropoka ropoka mambo kijuha bila nia wala mkakati sahihi unaotekelezeka. Maisha wa walimu yanazidi kuharibika, elimu na mafunzo duni ya walimu naviongozi wao kiasi cha kuwaumiza watoto as if wao ndio wanajilipia ada. Ccm kutoa matamshi ya kinafisi bila nia, na serikali kutofahamu nini kinatokea na kinachohitajika nchini.

Kikubwa cha serikali na cccm ni kujinafikisha kwa wananchi ili wawekwe tena madarakani lakini si kwa maslahi ya taifa.

Tunapowaambia ccm hailijua taifa ila inachojua ni uwongo na ufisadi kwa manufaa binafsi hamuwelewi. Tumieni kura yenu kwa weledi hapo tarehe 25 October, 2015.
 
INASEMEKANA... weka accurate facts tukuelewe... (kuhusu hicho kipengele cha fimbo)...
*pia rekebisha kauli yako.. hawajafukuzwa shule ila wamerudishwa nyumbani wakaombe pesa ya ada kwa wazazi na walezi...
***shughuli nyingi za uendeshaji wa shule hutegemea hiyo michango ya ada na mingineyo.. (

Kuwatandika fimbo watoto kwa mzunguko ndiyo kunaleta ada? Watoto hawa wanabiashara au ajira gani kwamba wachapwe fimbo ili watoe ada? Wanajlipia ada?

Kama serikali iliahidi kulipa ada kwawatoto kuanzia sasa, kwanini walimu wasiidai hioy serikali kama siyo unafisi na uwoga wa kijinga unaowafanya waisih kwenye frustrations zinazoumiza watoto?

Huu ni wehu!
 
Mbona hilo ni suala la kawaida na njia ya pekee ya kukusanya michango shule nyingi?Bakora kwa wingi then nyumbani baada ya hapo ada zinalipwa na wazazi.sio jambo jipya!
 
Kuwatandika fimbo watoto kwa mzunguko ndiyo kunaleta ada? Watoto hawa wanabiashara au ajira gani kwamba wachapwe fimbo ili watoe ada? Wanajlipia ada?

Kama serikali iliahidi kulipa ada kwawatoto kuanzia sasa, kwanini walimu wasiidai hioy serikali kama siyo unafisi na uwoga wa kijinga unaowafanya waisih kwenye frustrations zinazoumiza watoto?

Huu ni wehu!

umenielewa nlichokiandika hapo au umekurupuka!!??..
...HUONI NIMEHOJI SUALA LA VIBOKO KWA KUCHANGIWA NA WALIMU WOTE..(HAUONI KAMA NI ABNORMAL!?).. kwa mantiki kwamba kama imetokea akaweka sample ya ushahidi "hapo ni mwanafunzi" (accurate facts) huoni kama HAPO UFUATILIAJI WA KUWAWAJIBISHA WAHUSIKA UTAKUWA NA PAKUANZIA
 
by the way.. UMEKUWA MGENI NA SERIKALI YAKO.. KWA KILA MAMBO YANAYOGUSA MOJA KWA MOJA MAISHA YA MTANZANIA WA CHINI ..HUINGIZWA SIASA!!...
1* kinadharia mtu/mzazi mvuja jasho ukishamtangazia mtoto wake hatorudishwa nyumbani kisa ada.. (hata mimi nisingetoa) kwa serikali hii inavyotuchakachua
2* NAKUPA ASSIGNMENT UIFANYE KWA MUDA WAKO WA ZIADA..
nadhani unakumbuka ule mchakamchaka na JAMBAJAMBA ya ujenzi wa maabara... fanya uchunguzi wako binafsi JE ZIMEJENGWA!?..ZIMEISHA!?..ZINAFANYA KAZI YAKE STAHIKI!?
.......
shule hazina vitabu.. mahitaji ya vitu kama chaki ambavyo ni muhimu.. (ununuzi wa zana na vifaa vya kujifunzia).. vifaa vya kufanyia mazoezi ya vitendo(practical).. samani.. N.K.
....
HITIMISHO: MCHAWI WETU NI SERIKALI ILIYOPO NA MFUMO WAKE WA UENDESHAJI MAMBO Tabby
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu wanachangia mada ka wao wamesoma nje ya nchi, et kurudishwa mwanafunzi nyumbani kwa kukosa ada leo imekua kitu cha ajabu.... Ebu jiulize wewe hujawahi rudishwa home kwa kukosa ada.

Ni kisi kwa walimu kuwaadhibu wanafunzi kwa kukosa ada, labda kuna makubaliano kati ya wazazi na shule, mana kuna baadhi ya sehemu wazazi wamewekeana mikakati na shule kua mtoto ambaye hajalipiwa ada viboko kwanza then home kufuata hela.....

Alafu wanaposema free education waseme wanamaanisha nn coz inaweza ikawa free kwa ada ila michango mingine kama kawa kiasi kwamba inakua mingi kupitiliza.....
 
Kauli za serikali ya ccm za kisanii tuu

Mathalani kuna walimu wakuu wa shule fulani waliingia matatani kwa kufunga shule kutokana na deni la mzabuni wa chakula kuwa kubwa na mzabuni kugoma kutoa huduma mpaka alipwe sasa katika mazingira kama haya tuelewe nini kama sio sanaa na maigizo ya chama tawala.
 
Mkuu ndiyo hicho ninachokisema. Hakuna serikali makini tatangaza kwamba kuanzia sasa hakuna watoto kufukuzwa ada bila kuwa na namna financial gapes kwenye requirements za shule itajazwa. Huu ni ulaghai na ushenzi wa ccm. Na inatakiwa waalimu na wanafunzi wailjue hili.

Lakini hakuna professional teacher atamchalaza mwanafunzi fimbo eti hana ada as if ukosefu wa ada zako unasababishwa na yeye mwenyewe.

Waalimu nao wapumbavu tu wkao na frustrations ambazo hata hawajui wapi pa kuzilelekeza.

Kama shule zimeambiwa hakuna kufukuza mtoto ajili ya ada, ilikuwa ni jukumu la uongozi kuwasiliana na mamlak hsika za serikali namna ya utelekezaji wa elmu bila watoto kulipa ada au upatikanaji w afedha za uendeshaji kwa muda.

Ujuha ndo unakuja kuwarundikia fimbo watoto!
 
umenielewa nlichokiandika hapo au umekurupuka!!??..
...HUONI NIMEHOJI SUALA LA VIBOKO KWA KUCHANGIWA NA WALIMU WOTE..(HAUONI KAMA NI ABNORMAL!?).. kwa mantiki kwamba kama imetokea akaweka sample ya ushahidi "hapo ni mwanafunzi" (accurate facts) huoni kama HAPO UFUATILIAJI WA KUWAWAJIBISHA WAHUSIKA UTAKUWA NA PAKUANZIA

Keshataja shule husika na wahusika wanaweza kuanzia hapo kama ni wawajibikaji.
 
ccm matapeli ada wazazi wanatoa tokea shule za mzingi serikali inatoa capitation ambayo kwa mwaka takriban km milion 5 mpka 6 tuu sasa hizi hela unaendeshaje shule kwa mwaka mfano tuu kuchapisha mitihani kwa shule za sekondary kwa mwaka. watoke tuuu tumechoka
 
Ndio tatizo la kuchagua ccm hilo.Chagua UKAWA\LOWASSA afute kero hizo.Inawezekana!Kwa mujibu wa kamanda mtumishi wa Mungu Ben Saanane, mlima Kilimanjaro peke yake unatosha kumaza kero hii.
 
Last edited by a moderator:
umenielewa nlichokiandika hapo au umekurupuka!!??..
...HUONI NIMEHOJI SUALA LA VIBOKO KWA KUCHANGIWA NA WALIMU WOTE..(HAUONI KAMA NI ABNORMAL!?).. kwa mantiki kwamba kama imetokea akaweka sample ya ushahidi "hapo ni mwanafunzi" (accurate facts) huoni kama HAPO UFUATILIAJI WA KUWAWAJIBISHA WAHUSIKA UTAKUWA NA PAKUANZIA

ww inaelekea ni mwalimu,unataka ushaidi gani niweke hapa ktk jukwaa,acha kutetea walimu wenzako,hapa sio mahakamani unataka ushaidi,kama unataka kujiridhisha nenda shuleni kibamba lkn sio unatetea walimu wenzako watt wetu wanatabika,hii habari ni kweli kama ilivyo
 
Back
Top Bottom