Afyayaakili
JF-Expert Member
- Sep 12, 2012
- 903
- 1,175
WAZIRI WA ELIMU, NAOMBA TUOKOE HILI KUNDI NGUVU KAZI YA TAIFA YA KESHO.
Kwa hali inavooendelea huu ugonjwa kusambaa haikwepeki lakini ni lazima tupunguze namna ya ueneaji wake na katika jamii yetu ya Kitanzania na ulimwengu kwa ujumla kundi la wanafunzi lipo katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu wa mlipuko.
Wanafunzi wanatumia karibia masaa nane (8) kwa siku kukaa katika mkusanyiko mmoja kiasi kwamba wakipata maambukizi ni rahisi kuyasambaza wanaporudi majumbani na mitaani kwao.
Naomba shule zifungwe libaki kundi la wanafunzi wanaojiandaa na mitihani kama kidato cha sita tu, wengine warudi tu maana hali ishakuwa tete.
Wenzetu miji kama San Fransisco shughuli zimesimama kwa wiki tatu ili kuzuia maambukizi yasisambae sana hii pia kwa Italy na Hispania inatisha wamepata maambukizi mapya 1,000 ndani ya saa 24 ni hatari aisee.
Tunaomba tuchukue maamuzi mapema kabla ya kuzidiwa, kutumia njia hizi sio kwamba tumekubali tumeshindwa na ugonjwa huu bali ni njia nzuri kuwa tunaweza kupambana na ugonjwa huu na tukaushinda.
Tukae salama kila mtu katika kipindi hiki kigumu cha mpito naamini kila kitu kitakuwa sawa soon.