Wanafunzi mashujaa, wanakumbukwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi mashujaa, wanakumbukwa?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by montroll, Aug 29, 2011.

 1. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Hakuna vita isisyo na wahanga, na katika kila
  ushindi wa kuna walio tolewa kama kafara ili wengi wafaidi.

  Katika harakati za kupigania vyama vingi wanasiasa nguli na shupavu, kama walivyo wanaharakati wengi, waliungana na wanafunzi wa vyuo vikuu na wa taasisi zingine za elimu ya juu.

  Wanafunzi hao wakati huo walikuwa pia na mpambano na serikali dhidi ya uchangiaji wa elimu ya juu.

  Wanafunzi hao walipambana na mapambano yote mawili kwa wakati mmoja, walijitoa muhanga ili wengine wapate afueni, serikali ilwafukuza vyuoni na watawala wa vyuo walipokea maelekezo ya kuwatimua wanafunzi hao kwa uchungu kwani wanfunzi hao hata katika taaluma madarasni walikuwa ni vichwa, ilikuwa ni hazina kwa taifa na jamii kwa ujumla kama wangemaliza masomo yao.
  Wakatimuliwa na CCM wakiwa katika hatua za mwisho za kumalizia masomo yao.
  Wakati huo Mwalimu alikuwa ndio kwanza amen'gatuka urais, alikuwa anajishughulisa na south south comission. Wanafunzi hao katika kutafuta haki walimwendea mwalimu pale kitega uchumi mtaa wa samora,
  Majibu ya mwalimu yalikuwa kwamba, yeye ssiyo head of state, na kwakuwa ni head of state aliye wafukuza basi hakuna mwingine wa kubadilisha maamuzi hayo, kwamba wanafunzi wale:
  akina

  Cleven na wenzake pale UD,
  Kimaro na wenzake Muhimbili,
  Michael Montana na Issa Magid na wenzao pale SUA,
  na wengine wa ARDHI na Mzumbe.

  Nani anawakumbuka hawa?
  Hata wanafunzi vyuoni nao waenziwe kwa michango yao iliyotukuka katika kupigania haki na uhuru wa kweli dhidi ya ukandamizaji wa mkoloni mpya,ccm mpya baada ya Mwalimu.

  Nawakilisha.
   
Loading...