Wanafunzi chuo cha St. Joseph kuishtaki TCU

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Akithibitisha kufunguliwa kwa kesi hiyo, Wakili wa wanafunzi hao, Emanuel Muga, ameiambia East Africa Radio kuwa kesi hiyo imefunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya Jaji Eliezer Feleshi na kwamba katika madai hayo, wanafunzi hao pia wametaka masomo kusimamishwa katika chuo hicho mpaka mahakama itakaposikiliza kesi yao ya msingi.

Wakili Muga amesema kesi hiyo namba 311 ya mwaka 2016 inatarajiwa kuanza kutajwa kesho ambapo wanafunzi 316 kati ya 480 ya waliofukuzwa ndio wamefungua kesi wakidai haki ya kisheria kuingilia kati maamuzi yaliyofanywa na serikali

Kwa upande mwingine Wakili Muga amewataka wanafunzi waliofukuzwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma kudai haki yao Mahakamani na kuacha kulalamika kwani Mahakama pekee ndio inatoa haki kwa mtu aliyeonewa
 
Hii habari inaweza kusomeka "vilaza watinga mahakamani" kwenye magazeti pendwa. Tusubiri
 
Back
Top Bottom