Wanafunzi 875 warundikwa form IV 2015 St.Mathew Secondary

Bhampupile

JF-Expert Member
Jul 6, 2015
810
636
Kitendo cha uongozi wa shule ya St.Matthew,s secondary school kuwarundika wanafunzi 875 kama wahitimu wa kidato cha nne 2015 kinafaa kulaaniwa kwa nguvu zote.

Mara nyingi wazazi tunawapeleka watoto wetu shule za bweni, na tunakuwa tuko radhi kuwalipia gharama kubwa tukitarajia uongozi wa shule pamoja na waalimu wa shule husika watawasimamia watoto wetu vizuri badala ya wazazi.

Hivi wanafunzi 875 unafuatiliaje maendeleo yao? na je hakuna kikomo kilicho wekwa na Wizara kwa hizi shule Binafsi kuwa na kikomo cha idadi ya wanafunzi wanaopaswa kuwanao kwa kila darasa? Watoto wakija likizo utaona ripoti inaonyesha darasa linawanafunzi 50 kumbe kawagawanya wototo katika madarasa 17 kwa watoto 875.

USHAURI:
Wazazi msipeleke watoto shule hii, angalieni ktk mtandao jinsi tulivyo lizwa Wazazi wenzenu ktk matokeo ya ya kidato cha nne 2015.
 
875? Hii Ni zaidi Hata ya shule tulizopeleka watoto wetu zile za bure . Poleni Jamani wazazi wenzangu Sana hapa ndipo pesa yako inapokuadhibu mwenyewe.
 
feza boys ndio kiboko yao sababu wazungu wanafata utaratibu.. shule za waswahili njaa kali
Ni kama Ilivyo kwa Marian Girls ama St. Francis, wao huchukua wanafunzi 92 tu kwa mwaka kwa darasa moja, lenye mikondo miwili ya wanafunzi 46 kila mkondo. Hawana njaa. Sasa imagine, watoto karibia 4000 hufanyiwa usaili, na huchukuliwa wenye high performance 92, unadhani kuna kupata 0 hapo? St. Matthew ya mtoa mada naijua sana, mtoto wa kaka yangu niliemlea mwenyewe kamaliza pale 2014 A level, ni kweli wanafunzi ni wengia sana. Nyingi ya shule hizi za private huangalia quantity na si quality ya products zao.
 
Miaka minne unalipa tu gharama za kumsomesha mwanao bila kufika mazingira ya shule mkuu? Mikutano ya wazazi ulikuwa unaenda?
Mikutano ya wazazi tulikuwa tunahudhuria na hata ripoti za watoto wanapofunga shule tulikuwa tunafuatilia vzr, lakini si rahisi hivyo kujua weekness za mototo kwa kipindi kifupi cha likizo, na hata ukienda siku za kawaida kutaka kupata maelezo mafupi juu ya maendeleo ya motto wako watakupa lakini kumbe hayana uhakika wa ndani,maana wanafunzi 875 hata mwalimu wa somo atafuatiliaje maendeleo ya kila mwanafunzi kwa idadi hiyo ya watoto ktk darasa moja.

cha msingi ni tahadhari tu kwa wazazi wenzangu ,mwenzio akiumwa na nyoka usimcheke kwa uzembe bali chukua tahadhari ukijua eneo hilo si salama, muhimu ni kukumbushana tunapo peleka watoto katika shule hizi tunatakiwa kuwa waangalifu sn,wenzetu wanapenda fedha zetu kuliko maendeleo ya watoto wetu.
 
Umewasiliana nao wahusika na kuwajulisha kero hii? Naamini unaumia kama mzazi, lkn ni bira ungeanza nao wao kwanza
Sijakuelewa vzr mkuu, kwamba niwasiliane nao juu ya nini wakati tayari matokeo yalisha toka na watoto wetu walichopata ndicho hicho, zaidi nilikuwa nataka kuwakumbusha wazazi wenzangu umuhimu wa kuzichunguza hizi shule kabla ya kupeleka watoto wetu huko, tusifuate matangazo yao ya kwenye Radio Tumaini, Quality ya elimu inayo tolewa si sawa na ile inayotangazwa ktk Radio Tumaini. Hata ungekuwa wew mwalimu wanafunzi 875 unafuatiliaje maendeleo yao kwa idadi hiyo kwa kila mwanafunzi?
 
Ililetwa thread hapa kuwa walimu wa hii shule wanapokelea mshahara dirishani. Au siyo hii?
Itakuwa ni shule hii hii, kuna kipindi tulikuwa kwenye mkutano wa wazazi kuna baadhi ya waalimu walikuwa wanalalamika sn juu ya mfumo wao wa malipo ya mishahara na makato yao ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ilikuwa kila mwalimu unaekutana naye private kutaka kujua maendeleo ya mwanao hakosi kulalamika juu ya utawala wa shule hii.
 
Itakuwa ni shule hii hii, kuna kipindi tulikuwa kwenye mkutano wa wazazi kuna baadhi ya waalimu walikuwa wanalalamika sn juu ya mfumo wao wa malipo ya mishahara na makato yao ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ilikuwa kila mwalimu unaekutana naye private kutaka kujua maendeleo ya mwanao hakosi kulalamika juu ya utawala wa shule hii.

Kuna mgahawa mmoja huwa nakula nao na kunywa nao supu hao walimu wa hii shule.

Wanaonekana wana hali ngumu sana japo wanavaa smart. Inahitaji uwe na roho ngumu kuwakabidhi binti yako.
 
Najaribu kuwaza sipata majibu kabisa!!! That means hilo darasa la form 4 lilikuwa na waalimu 5 wa hesabu, 5 wa Englishi na watatu katika kila somo lililobaki. Maana yake darasa moja lilikuwa na jumla ya waalimu 30 kwa uchache!!

Duc In Altum.
 
Najaribu kuwaza sipata majibu kabisa!!! That means hilo darasa la form 4 lilikuwa na waalimu 5 wa hesabu, 5 wa Englishi na watatu katika kila somo lililobaki. Maana yake darasa moja lilikuwa na jumla ya waalimu 30 kwa uchache!!

Duc In Altum.
Ni vigumu kuamini lakini ukweli uko hivyo, mmiliki wa shule hii kakunja noti kwa wanafunzi 875 kwa form 4 tu kwa 2015, wakati shule zingine idadi hii ya watoto 875 ni idadi ya shule nzima kuanzia form 1 hadi form 6.
 
Chezea Nshomile weye,halafu utashangaa watakavyofaulu vizuri.Hapo na shule ya Tusiime panatakiwa kumulikwa sana
 
unaongelea hile St.Matthews ya Mtembei yule mzee tapeli na mwenye dharau na nyodo hata kwa waliomfanya apate uo utajiri wake.

mwaka 2003 walifutiwa matokeo kwasababu ya wizi wa mitihani na ubabahishaji mwingi maana yule tapeli alinunua magari spesho kama hongo kwa wasimamizi wa mitihani katika hiyo shule yake
ilifikia kipindi walimu wasimamizi walikuwa wanagombea kupangiwa icho kituo ili waondoke na magari ya bure
 
Huyo Mmiliki ana shule nyingine ST'Marks Secondary School, Ujenzi Sec School nazo hizi vipi maendeleo yake pia ufundishaji wa wanafunzi
 
feza boys ndio kiboko yao sababu wazungu wanafata utaratibu.. shule za waswahili njaa kali
Na Feza girls na Shamsiya zote za wazungu.Darasa wanafunzi 48 ,24 each class. Chakula na mazingira ni zaidi ya unavyofikiria.
 
Back
Top Bottom