Wanafunzi 184 wapewa mimba Bahi-Dodoma

Wanafunzi 184 wapewa mimba Bahi-Dodoma

neema shamuhenya

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
312
Reaction score
216
Wanafunzi 184 wamepata ujauzito katika umri mdogo na kukatisha masomo wilayani Bahi mkoani Dodoma.
Akizungumza wakati wa kuzindua Kampeni ya Mapambano dhidi ya Mimba na Ndoa za Utotoni mjini hapa jana, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Elizabeth Kitundu alisema wasichana hao wamepata ujauzito kati ya mwaka 2015 hadi Julai mwaka huu.
“Miongoni mwao wasichana 85 walikatiza ndoto zao wakiwa sekondari, 71 wakiwa katika jamii na wasichana 28 wakiwa katika shule za msingi,” alisema Kitundu.
Katika sekondari 20 za wilaya hiyo, wasichana wengi waliopata ujauzito wanatoka Shule ya Sekondari Bahi iliyopo mjini ambayo mwaka huu pekee, wasichana watano wameshafukuzwa shule kwa kupata ujauzito shuleni hapo.
Alisema pamoja idadi ya wasichana wanapata ujauzito kupungua mwaka hadi mwaka, bado ni tatizo kubwa Bahi kwani jambo hilo limekuwa likikwamisha maisha ya watoto hao ndoto za mafanikio maishani mwao.
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Rachel Chuwa alisema wanafunzi wa shule za sekondari na msingi wanatakiwa kuyaishi mabango waliyobeba katika maandamano ya kupinga kurubuniwa kupewa mimba kwa kupewa chipsi, lifti na kulazimiwa kuolewa katika umri mdogo.
“Miongoni mwake ni bango ambalo lilisema, ‘Nipe mimba utaona,’ na ‘Mafataki mtapata taabu sana mkitupa mimba wanafunzi,’ akawataka wanafunzi kwenda kuyaishi maneno yao katika maisha ya kawaida kwa kupata mimba,” alisema.
 
Very very sad wallahy.

Dreams cut short just like that.

I weep for the girl child.😕😕
 
Hilo bango lililoandikwa nipe mimba utaona, limeruhusu kugegedwa ila sharti ni kutoa provide mimba au walikuwa wanamaanisha nini
 
hata kama wamekimbilia JF watakamatwa tu hauwezi kuwaharibia future watoto then ukaachwa salama
watu wa Dom ni kawaida yao..wanatia mimba ikishajibu wanatoka nduki,wanakaa hukoo kisha wanarudi tena wanapiga tena mimba hata kale katoto ka kwanza hakajaanza kutembea...hahaaaa wagogo wajomba zangu mko vizuri,kwa kupiga mimba tuu aaahh shikamooni!
 
Back
Top Bottom